Forbes: Ronaldo mchezaji soka anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani

forbes

Chanzo cha picha, Getty Images

Mtandao wa Forbes umetoa orodha mpya ya wanasoka wnaaolipwa fedha nyingi zaidi duniani kwa mwaka, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wakibadilishana nafasi mbili za juu kutoka orodha ya mwaka uliopita.

Wakali hao wa soka, licha ya kuhamia vipya msimu huu, wameendelea kutawala orodha hiyo ya wanasoka wanaopokea vitita vikubwa duniani, wakijizolea dola $235 million kwa msimu huu.

Masaa 24 kabla ya Cristiano Ronaldo kuikacha Juventus ya Italia na kuhamia Manchester United, msahambuliaji huyo mreno alikuwa mchezaji aliyeuza jezi nyingi katika uga wa michezo, akiongoza orodha ya wachezjai waliohama vilabu vyao katika miaka ya hivi karibuni akiwemo nyota wa NFL Tom Brady mwaka 2020, mkali wa kikapu kutoka ligi ya NBA Marekani , LeBron James aliyeongoza mwaka 2018 na mkali mwingine wa MLB Bryce Harper, aliyekuwa juu mwaka 2019.

Lakini jambo zuri kwa Ronaldo huenda likawa ni kumpiku mshidani wake kwenye soka, Lionel Messi, ambaye wiki chache nyuma alitangaza kuondoka Barcelona na kujiunga na Paris Saint-Germain.

Kuuza kwa jezi zenye jina lake, kunaonyesha alivyo na ushawishi mkubwa duniani — akiwa na wafuasi nusu bilioni kwenye mitandao ya Facebook (149 million), Instagram (344 million) na Twitter (94.3 million)—na hilo limemsaidia kupaa kwenye orodha ya Forbes mwaka huu kama mchezaji soka anayelipwa zaidi duniani.

Ronaldo anatarajia kuingiza dola $125 million kabla ya kodi katika msimu huu wa 2021-22, dola $70 million zikitokana na mshahara wake na marupurupu ya kurejea kwake Man United, ambaye kati ya mwaka 2003 na 2009 aliisaidia kutwa makombe matatu mfululizo ya ligi kuu England pamoja na la ligi ya mabingwa Ulaya.

Fedha zingine za Ronaldo mwenye umri wa miaka 36 zinatokana na mikataba binafsi ya kibiashara na ushirika wa kujtangaza bidhaa kama Nike, Herbalife, Clear na brandi yake inayokuwa kwa kasi ya CR7 anayoitumia kwa bidhaa za manukato, nguo za ndani, miwani, hoteli, sehemu za mazoezi na vitu vingine.

q

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, LeBron James ni miongoni mwa wanamichezo wanaolipwa zaidi kwenye matangazo, lakini hajafua dafu kwa Ronaldo mwaka huu

Katika miaka yake 18 ya kusakata kabumbu Ronaldo ameshinda jumla ya makombe makubwa 32 yakiwemo matano yta ligi ya mabingwa ya Ulaya, taji la UEFA European akiwa na Ureno na mataji saba ya ligi akicheza England, Hispania na Italia, na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kushinda mataji ya aina hiyo katika nchi tatu tofauti.

Mapema mwezi septemba , nyoita huyo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwa timu za taifa akifikisha mabao 111. Bao lake la 110 alilifunga dhidi ya Ireland kwenye mchezo wa kufuzu kombe la dunia. Ronaldo amefanikiwa kujiingizia kitita cha dola zaidi ya $1 billion katika maisha yake ya soka kabla ya kodi, akiwa ni mwanamichjezo wa kwanza kufikjia kiwango hicho.

Ni wanamichezo watatu tu wengine waaoingiza pesa nyingi kupitia biashara: Roger Federer ($90 million), LeBron James ($65 million) na Tiger Woods ($60 million).

Mess mwenye miaka 34 , ambaye baada ya miaka 21 ametimka Barcelona na kujiunga na PSG, atalipwa dola $75 million msimu huu, kiasi kinachomuweka kwenye nafasi ya pili nyuma ya Ronaldo, akitarajiwa kuingiza dola $110 million. Messi mwenye tuzo 6 za mchezaji bora wa mwaka wa dunia aliyeichezea Barca tangu akiwa na miaka 13 , atalipwa dola $35 million kutokana na mikataba binafsi na makampuni ya Adidas, Pepsi, Jacobs & Co. na Budweiser, aliyeingia nao mkataba wa miaka mitatu mwaka jana.

sala

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mo Salah wa liverpool, ameendelea kuwa kinara kwa wanasoka wanaolipwa zaidi Afrika

Kwa ujumla wachezaji soka 10 wanaolipwa zaidi duniani wanatarajiwa kuingia jumla ya dola $585 million msiumu huu kabla ya kodi, ikiwa ni ongezeko la dola milioni $15 za mwaka jana. Mishahara na marupurupu yanafikia jumla ya dola 415 million—ikiwa ni ongezeko la silimia 2.6% zaidi ya mwaka jana licha ya tahadhari za janga la Corona.

Mwezi Mei mwaka jana UEFA, lilieleza kwamba klabu kubwa Ulaya zinakabiliwa na hasara ya dola $8.5 kutokana na janga la corona.

sala

Chanzo cha picha, Google

Maelezo ya picha, Neymar (kushoto), Mbappe (katikati) na Messi (Kulia) nyota watatu wa PSG waliomo kwenye tano bora ya wanaolipwa zaidi duniani

Klabu ya PSG ina wachezaji watano wanaolipwa zaidi duniani akiwemo Neymar, anayeshika nafasi ya tatu nyuma ya Ronaldo na Messi ambaye anaingiza dola $95 million, na Kylian Mbappe, anayweshika No. 4 kwa dola $43 million. Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, 29, yuko nafasi ya 5 kwa dolas $41 million.

Mwaka huu, nyota wa zamani wa Barcelona Andres Iniesta mwenye miaka 37, amerejea na kuwa mchezaji pekee kutoka ligi ya nje ya Ulaya na kushika No. 7 akiingiza dola $35 million baada ya kusaini mkataba wa miaka 2 na klabu yake ya Vissel Kobe ya Japan, klabu ambayo amekuwa akiichezea tangu ahame Barcelona mwaka 2018.