Mkulima wa Australia amechora moyo kwa kutumia kondoo ili kumuonesha mapenzi shangazi yake aliyefariki

Maelezo ya video, Mkulima wa Australia atoa heshima zake kwa kwa marehemu shangazi yake kwa video ya kondoo

Sawa na familia nyingi zilizotengana wakati wa janga la corona, Ben Jackson hakuweza kusema kwaheri kwa shangazi yake mpendwa ambaye alifariki dunia wakati wa janga la corona.

Jackson ambaye ni mkulima nchini Australia alikuwa kilomita 400 (maili 248 ) kutoka katika mji wa New South Wales wakati shangazi yake mpendwa Debby alipofariki dunia kutokana na maradhi ya saratani ambayo alihangaika nayo kwa kipindi cha miaka miwili huko Queensland.

Sheria zilizowekwa za udhibit wa virusi vya corona zilimzuia kuhudhuria mazishi yake.

Kwa hivyo kwa huzuni kubwa aliamua kugeukia kondoo wake na mifugo yake kuonesha upendo, kwa kupanganafaka ardhini kwa umbo la moyo.

Alilenga kuzisambaza nafaka zake ili atakapowaachilia maelfu ya kondoo wake watajipanga na kujaza umbo hilo kubwa la moyo.

Baada ya kufanya majaribio machache ya kitendo hicho na "kubashiri kidojgo", alifanikiwa kuwaona kondoo wamejipanga kwa umbo alilolitaka. Halafu akawcha wanyama hao wazurure.

Matokeo ya mpangilio huo yalinaswa kwenye video na droni- video hiyo ilisambazwa sana baada ya Bw Jackson kuishirikisha kwenye mtandao.

"Hapakuwa na njia yoyote ambayo ingeniwezesha kuamka na kumuona, alisema cheerio, au niende kwenye mazishi ," aliiambia BBC.

"Kwa hiyo nilijihisi kukosa matumaini, bila usaidizi-kusema ukweli sikujua la kufanya. Kwasababu nilikuwa tayari ninawalisha , Nikaamua tu kutengeneza umbo la moyo kubwa ardhini ambao kwa ujumla ni bidii, rangi ambayo niliifananisha na yeye ."

'upendo wa kusisimua'

Bwana Jackson aliwatumia ideo ndugu zake kabla ya mzishi ya shangazi yake siku ya Jumatatu.

Katika ibada ya mazishi, walicheza wimbo wa Simon and Garfunkel , wa Bridge Over Troubled Water, katika video hiyo na mkusanyiko wa picha.

"Ulikuw ni wimbo alioupenda zaidi katika kipindi chote cha maisha yake na … nilipoitazama vile, nilihisi kama nimekata tani ya vitunguu. Nilijawa na hisia za majonzi sana na machozi yalinitiririka ," alisema Jackson.

Katika miaka ya hivi karibuni, Bw Jackson alitengeneza "kazi za usanii kwa kutumia kondoo'' kama vile umbo la ishara na nembo . Marehemu shangazi yake alikuwa shabiki kila mara waubunifu wake.

Shangazi yake ambaye anamuelezea kama mpenda watu na mwanamke "mkarimu sana" mara ya mwisho alikuwa amemtembelea mwezi Mei, anasema. Hiyo ilikuwa kabla ya mlipuko wa Covid kuilazimisha Ausralia kweka sheria ya kukaa nyumbani.

Siku ya Alhamisi, Bw Mr Jackson alikuwa bado chini ya sheria ya kukaa knyumbani ililowekwa kote nchini Australia, kwa hiyo aliendelea kukaa kwake katika eneo la mashambani la Guyra lililopo New South Wales.

Lakini video ya heshima ya kondoo wake kwa shangazi yake imekuwa ikichezwa kwenye vituo vya televisheni nchini Australi na kusambazwa kwa kiasi kikubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Shangazi yake angelikuwa hai angefurahia sana hilo, anasema.

"Angejivunia sana kuona watu wengi sana wakitabasamu na kufurahia moyo nilioutengeneza kwa ajili yake. Ni upendo tu. Hisia za upendo."

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Fedha hizi zitatosha kupambana na janga la Corona Afrika Mashariki?