Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Utakubali mwanasheria roboti akutetee mahakamani?
Unaweza kutumia roboti kama mwanasheria wako? Kama kitu kisichowezekana , lakini kuna mfumo maalumu unaitwa artificial intelligence (AI) software systems - unaotumia program ya kompyuta ambayo inaweza kutunza, kutoa taarifa na 'kufikiri' yenyewe - mfumo ambao sasa unaonekana kutumiwa sana na jamii ya wanasheria.
Joshua Browder anaelezea program ya DoNotPay kama "mwanasheria wa kwanza roboti".
Roboti hilo linasaidia hata kuandaa barua za kisheria. Unachotakiwa kufanya ni kuliambia kupitia 'chatbot' tatizo lako ni nini ama unataka nini, kwa mfano kama hukubaliani na faini uliyotakiwa kulipa ya maegesho ya magari, litakusikiliza na kukushauri nini ambacho roboti hilo linafikirina na lugha gani nzuri ya kisheria unaweza kutumia.
"Watu wanaweza kuandika hoja zao kwa maneno yao, na program hii yenye mashine maalumu itatafuta ufumbuzi wake kisheria na namna gani ya kusema tena kwa usahihi," alisema.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 ana kampuni yake yenye makazi yake huko Silicon Valley, California, lakini historia ya kampuni hiyo ilianzia huko London mwaka 2015, wakati huo Browder akiwa na miaka 18.
"Nikiwa kijana huko Hendon, London Kaskazini, nilikuwa dereva wa ajabu sana," alisema. "Nilikuwa kila wakati napigwa faini ya kuegesha garti vibaya - wakati huo niko shule ya sekondari, sikuwa na uwezo wa kulipa."
Baada ya kufanya utafiti wa kina na kusaka taarifa mbalimbali Browder alisema akagundua njia nzuri ya kupinga faini hizo. "Kama unajua vitu gani sahihi vya kusema, unaweza kuokoa muda na fedha."
Badala ya kukopi nyaraka zile zile kila wakati, akasema hiyo ni "kazi mujarabu kwa program hiyo". Akaamua kutengeneza toleo la kwanza la program hiyo inaiyoitwa 'DoNotPay' kwa kutumia wiki chache tu mwaka huo wa 2015, "ukweli iliwavutia sana familia yangu".
Tangu wakati huo, program hiyo imesambaa sehemu mbalimbali za Uingereza na Marekani, na sasa inaweza kuwasaidia kuandika barua kuhusu masuala mbalimbali kwa mfano; madai ya bima, maombi ya viza za kitalii, barua za malalamiko ya kibiashara ama malalamiko dhidi ya serikali, kurejesha fedha zako kama umehairisha likizo yako, au kujiondoa uanachama wa eneo la mazoezi (gym).
DoNotPay kwa sasa inawatumiaji wa kulipia zaidi ya 150,000. Licha ya kwamba inakosolewa na baadhi ya watu wanaosema ushauri wa kisheria wa roboti hilo hauko sahihi kwa asilimia 100, lakini mwaka jana iishinda tuzo kutoka American Bar Association kwa mchango wake wa kuongeza huduma za kisheria kuwafikia watu wengi zaidi.
Browder anadai kiwango cha mafanikio cha program hiyo kimeshuka kutoka 80%, hadi 65% kwa faini za kuegesha magari, kwa sababu "'watu wengine wanakuwa wamefanya kweli makosa".
Unaweza kusema wanasheria binadamu unaowajua wanaliogopa roboti hilo kwa kuingilia majukumu yao. Lakini wapo waliofurahishwa na proram hiyo kwa maelezo kwamba inaweza kusaidia kuharakisha uendeshaji wa kesi na kupunguza mzigo wa nyaraka za masuala ya sheria.
Mmoja wa wanasheria hao Sally Hobson, anashughulikia kesi za jinai akifanya kazi na kampuni ya wanasheria ya The 36 Group, jijini London. Hivi karibuni ameanza kutumia program hiyo katika kesi tata ya mauaji. Kesi hiyo ilihitaji uchambuzi wa haraka wa kupitia nyaraka zaidi ya 10,000.
Roboti au Program hiyo iliweza kufanya kazi hiyo kwa haraka kwa muda wa wiki nne tu kuliko angefanya binadamu, na kuokoa karibu dola $70,000.
Wanasheria wanaotumia usaidizi wa roboti hilo wanasema "sasa inakuwa kawaida", anasema Eleanor Weaver, mtendaji mkuu wa Luminance, aliyetengeneza program anayotumia Hobson.
Zaidi ya makampuni ya kisheria 300 katika nchi 55 wanatumia roboti hilo, linalofanya kazi katika lugha 80 tofauti.
"Kihistoria kuna teknolojia nyingi za kupitia na kuchambua nyaraka ambazo ni rahisi tu kwa kubonyeza Control-F kwenye kompyuta yako," anasema Weaver. Akitoa ulinganisho na za sasa, anasema program nyingi za sasa unaweza kuzitumia na kuunganisha maneno na sentensi na kutoa nyaraka iliyokamilika.
Program ama roboti hilo, sio tu linawasaidia wanasheria kupitia vyema nyaraka za ushahidi, lakini pia linawasaidia kuandaa kesi na kutafuta vielelezo vyovyote vya kisheria.
Laurence Lieberman, anayeongoza kampuni moja ya kisheria ya London Taylor Wessing alisema amekuwa akitumia program iliyoboreshwa iliyotengenezwa na kampuni kutoka Israeli inayoitwa Litigate.
"Unaweka muhtasari wa kesi zako na maombi yako, na yenyewe inafanyia kazi na kukuonyesha wahusika muhimu," amesema. "Baada ya hapo Program hii itaziunganisha pamoja na kuweka matukio muhimu na maelezo muhimu ya nini kilitokea na wakati gani kilitokea."
Wakati huo huo, Bruce Braude, afisa mkuu wa masuala ya teknolojia kutoka Deloitte, anasema program ya TAX-I inaweza kuchambua taarifa za zamani za mahakama kuhusu kesi za kodi.
Kampuni hiyo inasema program hiyo ama roboti hilo linaweza kubashiri rufaa itakuwaje kwa asilimia 70%. "Inatoa njia thabiti ya namna gani mafanikio yatakuwa, kitu ambacho unaweza kuamua je uendelee na kesi ama uache," aliongeza Braude.
Kwa sasa program ama roboti hizo zinasaidia kuandika barua za kisheria na kusaidia wanasheria, je kuna siku tutashuhudia mawakili maroboti ama majaji maroboti?
"Nafikiri, kusema ukweli bado hatujawa karibu kufikia hilo," anasema Weaver.
Lakini wataalam wengine kama Prof Richard Susskind, ambaye ni mshauri wmwandamizi kuhusu proramu za aina hii, na yeye hana uhakika na hilo.
Prof Susskind anasema katika miaka ya 1980s alishangazwa aliposikia wazo kuhusu jaji roboti ama jaji wa kompyuta, lakini sasa hashangazwii.
Anaeleza kwamba hata kabla ya mlipuko wa janga la virusi vya corona, "Brazil ilikuwa na mrundikano wa kesi mahakamani zaidi ya 100 million, na hakuna uwezekano wa jaji binadamu na wanasheria wanaoweza kushughulikia mzigo wa kesi zote hizo".
Kwa hiyo program hii inaweza kubashiri maamuzi ya mahakama kwa kiwango cha usahihi cha 95%, na kusema kwamba, roboti hizo zinaweza kutumika kusaidia kupunguza mzigo wa kesi kwa nchi zenye mrundikano mkuwa wa kesi mahakamani.