Fenty Beauty: Fahamu Jinsi biashara ya vipodozi ilivyomfanya Rihanna kujiunga na orodha ya mabilionea duniani

Msanii huyo ana thamani ya dola bilioni moja nukta saba

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Msanii huyo ana thamani ya dola bilioni moja nukta saba

Wakati Rihanna alipotoa kibao chake kimoja cha muziki ...Better Have My Money mwaka 2015, ungefikiria alikuwa anazungumzia kuhusu kuweza kupata uwezo wa kutoa kijibao kitakachokuwa namba 1 kama vile kibao cha We Found Love au Diamonds.

Lakini ni mapato anayoyapata kutokana kampuni yake ya vipodozi vya urembo Fenty Beauty ambayo ilihusika katika kumfanya awe bilionea rasmi wiki iliyopita.

Rihanna, mwenye umri wa miaka 33, alizindua kampuni ya Fenty Beauty mnamo 2017 kwa ushirikiano na kampuni ya bidhaa za anasa LVMH (Moët Hennessy Louis Vuitton).

Radio 1 Newsbeat imekuwa ikizungumza na wataalamu wa urembo kuweza kubaini siri ya mafanikio makubwa ya Fenty.

'Utofauti usiokuwa vizuizi'

Rihanna alisema lengo la Fenty lilikuwa ni kumvutia "kila aina ya mwanamke " kwa "aina zote za ngozi".

"Katika kila bidhaa nilikuwa nasema hivi: 'Kuna haja ya kuwa na kitu fulani kwa ajili ya msichana mwenye ngozi nyeusi; kuna haja ya kutengeneza kipodozi kwa ajili ya msichana mweupe sana; kuna haja ya kuwepo kwa kipodozi cha msichana mwenye ngozi ambayo si nyeupe wala nyeusi ,'" aliiambia Refinary29 mwaka 2017.

Hicho ndio kitu kilichojitokeza kwa muandishi wa masuala ya urembo Jessica Morgan.

"Jinsi Rihanna alivyojali utofauti wa ngozi za watu wa tabaka mbali mbali bila vizuizi. Alihakikisha hakuna aina nyingi za bidhaa za aina moja kwa bidhaa zote ambazo zilikuwa zinapatikana kwa kila mmoja ," alisema Bi Morhan mwenye umri wa miaka 28.

Rihanna alisema: Hivyo munataka watu kupenda bidhaa na kutozihisi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rihanna alisema: Hivyo munataka watu kupenda bidhaa na kutozihisi

Kipodozi cha faundesheni cha Fenty sasa kinatoa ofa ya vipodozi vingine vya juu 50 na kimepelekea kile kinachoitwa "athari za Fenty " ambapo nembo nyingine hasimu ziliozokuwa na bidhaa zao nyingi kwa ajili ya vipodozi vyao.

Jessica hutumia faundasheni ya Fenty, na anasema ingawa hakuhisi kilikiwa kizuri wakati ule, yalikuwa ni "mapinduzi" wakati kilipozinduliwa mwaka 2017.

"Niliweza kupata kipodozi halisi kinachoendana na ngozi ya mwili wangu ," anasema.

Kwa Jessica , uzinduzi wa foundation ye fenty ulimrahisishia kazi ya kutafuta itakayompendeza

Chanzo cha picha, INSTAGRAM/JESSICA MORGAN

Maelezo ya picha, Kwa Jessica , uzinduzi wa foundation ye fenty ulimrahisishia kazi ya kutafuta itakayompendeza

Hakikuwa tu kuhusu vipodozi vya ngozi nyeusi tu

"Nakumbuka baadhi ya marafiki zangu ambao walikuwa ni wazungu weupe sana vipodozi viliwafanya waonekane kuwa na ngozi nyororo na faundesheni ilikuwa na rangi ya chungwa kiasi," anasema Chinazo Ufodiama, anayefanya kipindi cha Unpretty cha podcast.

"[Rihanna] alisema: 'Madada zangu wazungu weupe, Pia nina bidhaa zenu sijawasahau.'"

Fenty ilikuwa ni miongoni mwa nembo za kwanza ambazo hazikutangaza vipodozi kwa ajili ya wanawake pekee.

"Wazo kwa ujumla la kutolenga urembo na manukato kwa ajili ya jinsia ya aina fulani limeondoka kusema kweli," anasema mwandishi wa habari za urembo Amber Graffland.

Kupanda na kupanda kwa kampuni ya Fenty Beauty

Rihanna na utajiri wa thamani ya dola bilioni 1.7 za kimarekani (£1.2bn), huku ikikadiriwa kuwa dola bilioni 1.4 zinatokana na thamani ya Fenty Beauty.

Forbes - jarida la biashara ambalo limetangaza kuwa amekuwa bilionea- linasema anamiliki 50% ya kampuni za bidhaa za vipodozi.

Nyota huyu alianzisha kampuni ya Fenty Beauty katika maduka 1,600 katika nchi 17 mwaka 2017.

Kampuni hiyo inaripotiwa kupata dola milioni 100 (£72m) katika kipindi cha siku 40 za mwanzo.

Inatengeneza pesa zaidi kuliko nembo nyingine za urembo za watu maarufu kama vile Kylie Cosmetics, KKW Beauty ya Kim Kardashian na ya Jessica Alba Honest Company, kulingana na Forbes.

Utajiri mwingine wa Rihanna kwa kiasi kikubwa hutokana na kampuni yake ya mauzo ya nguo za ndani, Savage X Fenty, wa thamani ya takriban dola milioni 270 (£194m), na mapato yake yatokanayo na muziki na uigizaji.

Jessica, anayeishi mjini London, alikuwa katika moja ya maduka ya Fenty nchini Uingereza wakati kampuni hiyo ilipozinduliwa katika jengo la Harvey Nichols luxury

"Nilikuwa tayari nimeisha pata faundesheni yangu -Nimeipenda sana Bobbi Brown."

Lakini Chinazo, ambaye anatoka katika eneo la Wakefield lakini kwa sasa akiishi katika Hackney, anakiri kuwa na nembo yenye aina tofauti za vipodozi kwa watu tofauti ni jambo bora zaidi.

"Sio kuenda kwenye duka la vipodozi vya urembo na kuanza kujaribu jaribu kila nembo moja moja kujaribu kupata kipodozi kinachoendana vyema na rangi yako ya mwili na ngozi - hilo ni kama limeisha kutokana na ukweli kwamba unaweza kwenda tu katika eneo la mauzo la Fenty na kupata kipodozi kinachoufaa mwili wako."

Maadili yasiyo ya ukatili

Wavuti wa Fenty ni nembo isiyo na ukatili kwa maana kwamba haupimi ubora wa bidhaa zake kutumia wanyama.

Amber anasema "kusema kweli umeongoza katika njia ", ya kuonyesha nembo kubwa zaidi kwamba "hawaifikii " kwa kutochukua hatua haraka.

"Wanunuzi wanahudumiwa zaidi na wana uelewa zaidi kuliko wakati kuliko wakati wowote ule . Hununua popote watakapo na huweka pesa zao pale mioyo yao ilipo - na ni wazi kuwa ina maadili yasiyo ya kikatili, na inazingatia utofauti wa watu wa asili mbali mbali , na ni nembo inayomjali kila mtu," anasema Amber .

Jessica anaongeza kuwa kuwa na nembo isiyo ya ukatili ni mkakati bora wa kulinadi soko la bidhaa kwasababu huisaidia kampuni kuepuka mijadala ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaopenda utata.

'Unajihisi kana kwamba uko sehemu ya genge'

Mkakati wa mtandao wa kijamii wa Fenty pia unaifanya kampuni hii kung'ara miongoni mwa umati wa makampuni mengine, anasema Chinazo.

"Karibu inanikumbusha siku ambapo nilikuwa najiandaa na wasichana wangu kabla ya kwenda kutembea nyakati za usiku na tulikuwa tunapita kwenye maduka ya vipodozi- hivi ndivyo ninavyohisi wakati unaporambaza kwenye mtandao wa Instagram kwenda juu na chini."

Kitu ilichofanya bidhaa hizo kupata soko kubwa ni kutokana zinaweza patikana kwa bei ya rejareja

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kitu ilichofanya bidhaa hizo kupata soko kubwa ni kutokana zinaweza patikana kwa bei ya rejareja

Amber anaafiki kuwa kazi ya mtandao wa kijamii wa Fenty umeifanya ing'ae.

Ushawishi wa Rihanna

Ni vigumu kuepuka nguvu ya kuwa nyota kwa Rihanna katika kuifanya Fenty, kuwa biashara inayoshuhudiwa sasa.

Huku wengi wa mashabiki wamekuwa wakisubiri tangu 2016 kuwasili kwa muziki, ukitazama haraka haraka kwenye ukurasa wa Instagram wa Rihanna wenye wafuasi 103 million unaonesha wengi ni wale wanaofuatilia kampuni ya Fenty kuliko muziki.

Chinazo anasema kwamba ukuzaji mzuri unamfanya mteja kuhisi anashirikishwa katika urembo

Chanzo cha picha, NICOLE HAINES

Maelezo ya picha, Chinazo anasema kwamba ukuzaji mzuri unamfanya mteja kuhisi anashirikishwa katika urembo

"Ninadhani kile ambacho wanapenda kumuhusu kusema kweli ni uhusiano wao na nembo.

Unaweza kuona Rihanna hutumia na kuzungumzia kuhusu bidhaa kwa njia ya uhalisia," anasema Jessica.

Na kama ulipitwa, nakufahamisha kwamba Rihanna ameongeza pia manukato kwenye bidhaa zake za Kampuni ya Fenty.

Inaonekana kuwa kwake bilionea hakujazuia ari yake ya ujasiriamali.