Je ni kweli kwamba kuvua mpira wakati wa tendo la ndoa bila ridhaa ni ubakaji?

Chanzo cha picha, Getty Images
Miaka miwili iliyopita, Gemma (sio jina lake halisi) alifanya ngono na mwanaume ambaye baadaye alivua mpira wa kiume bila yeye kujua au kuridhia.
Stealthing --inamaanisha 'kuiba', lakini katika kesi hii linamaanisha kuvuliwa kwa kondomu bila makubaliano - pamoja na ubakaji chini ya sheria ya Uingereza.
Hata hivyo, hadi sasa kesi moja tu ya aina hii ilishinda mahakamani, na hiyo ilikuwa mwaka 2019."Sikujua chochote kuhusu 'kuiba' hadi iliponikuta," Gemma aliiambia BBC Radio 1 Newsbeat.
"Niligundua tu kile alichokuwa amekifanya baada ya kutokea, na nilihisi kufadhaika sana.
"Mara moja nilikunywa kidonge cha kuzuia mimba , lakini wakati mwezi uliofuata sikupata hedhi, mara moja nikachukua kipimo cha ujauzito."
Gemma alisema wakati kipimo kilipoonesha kuwa alikuwa mjamzito alipatwa na mshtuko.
'Alisema gharama ya kutoa mimba ni pauni 50'

Chanzo cha picha, Thinkstock
"Nilikuwa na hasira, nikihemkwa na kuchanganyikiwa. Nilimtumia ujumbe mtu huyo lakini hakufikiria ni jambo kubwa na akasema kuwa utoaji wa gharama unagharimu karibu pauni 50 tu - lakini tukio hili lilibadilisha maisha yangu.
"Mwishowe niliamua kuumaliza ujauzito huu, lakini ilikuwa uamuzi mgumu sana - najilaumu, kwa sababu nilikuwa nikitaka mtoto, lakini haya hayakuwa mazingira sahihi."
Gemma aliripoti polisi, lakini kesi yake haikufuatiliwa.
"Nilienda kwa polisi kwa sababu nilibakwa na kwa sababu nilipata ujauzito kwa sababu hiyo."
Alisema polisi baadaye walizungumza na mtu huyo lakini hakukuwa na ushahidi wa kutosha na kwa sababu ya hii "maneno yangu yalikuwa tofauti na mtu huyo, na akakana."

Suala kama hilo lilizungumziwa mwaka jana katika safu ya maigizo ya BBC One, iliyoitwa 'I May Destroy You' .
Katika sehemu ya nne, mhusika mkuu wa safu hiyo, Arabella, anajamiiana na mtu anayevua kondomu bila yeye kujua.
Kama wanawake wengine wengi, Arabella hakugundua kuwa hii ilikuwa aina ya ubakaji hadi aliposikia ikijadiliwa kwenye makala.
'Tunazungumzia ubakaji '
Msemaji wa shirika la kupambana na ubakaji Rape Crisis alisema matukio hayo yamekuwa mambo ya kawaida siku hizi.
"Ni ngumu kubainisha sababu, iwe ni kwa sababu inatokea mara nyingi au kwa sababu watu wanaanza kufahamu suala hili na wanazungumza juu yake wazi zaidi," alisema Katie Russel wa shirika hilo.
Alisema pia matumizi ya neno 'kuiba' haikusaidia.
"Kifungu hiki ni kipya, na wakati mwingine kuunda istilahi mpya inaweza kusaidia watu kugundua ni nini, lakini kwa upande mwingine, inaweza pia kupotosha.
"Neno hili linaonekana kupungua na kusafisha tabia, kwa sababu mwisho wa siku tunazungumzia ubakaji.
"Tunapaswa kuwa wazi kuwa hii ni tendo lisilo la makubaliano la kutolewa kwa kondomu, na hili sio tukio ambalo huwezi kuadhibiwa - ni mbaya sana na inaweza kuwa na athari mbaya, shida za kiafya na kifo, kwa wengine."
Hakuna idadi kamili ya kesi hizi kutoka kwenye taasisi hii au polisi wa Uingereza, kwa sababu kuripoti kwa kesi hii huenda katika eneo la ubakaji. Lakini polisi wa Uingereza waliwasihi waathirika waripoti tukio hili kwao.
Edem Barbara Ntumy alikiri kwamba tukio kama hilo limemtokea.
"Nilikuwa na uhusiano wa kawaida na mtu, na wakati wa kujamiiana aliondoa kondomu bila idhini yangu. Nilimkemea wakati huo, lakini alikanusha na kuwa mkali, kwa hivyo niliamua kuacha kuzungumza naye," anaiambia BBC Newsbeat.
"Sikuyaripoti polisi kwa sababu sikufikiria nitapata matokeo ninayotaka.

Chanzo cha picha, EDEM BARBARA NTUMY
"Natambua kesi za ubakaji zinachukua muda mrefu kuchunguzwa, na vifaa vyako vyote vitachukuliwa na itachukua muda mrefu zaidi kumaliza kesi. Sitaki kupitia hiyo."
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, idadi ya matukio ya ubakaji yaliyoripotiwa nchini Uingereza yameongezeka, lakini idadi ya kesi zinazoenda mahakamani ni nusu tu.Katika taarifa iliyoandikwa, Mwendesha Mashtaka wa Umma alisema, "Tumeazimia kuongeza idadi ya kesi za ubakaji mahakamani.
Waathiriwa wachache sana wanapata haki, na tunafanya bidii kuibadilisha hali hiyo."Edem kwa sasa anafanya kazi inayohusu masuala ya afya ya ngono, na alitaka kutafuta njia nyingine ya kufungua kesi ya aina hiyo ambayo haikuhusisha mfumo wa haki ya jinai.
"Nadhani hii hufanyika mara nyingi sana, na inapaswa kuwa na njia ya waathiriwa kuripoti, bila kuhitaji uchunguzi wa polisi," alisema.
"Nimekubali tukio hilo. Kilichonitia wasiwasi zaidi wakati huo ni ikiwa ningepata ugonjwa wa zinaa, kwa sababu tulikuwa na uhusiano wa kawaida, sio uhusiano wa kutiliwa maanani."
"Ninajisikia hasira sana, kwa sababu ikiwa una uhusiano wa kawaida basi ni muhimu sana kuheshimu mipaka ya mwenzi wako wa ngono, haswa ikiwa unafanya ngono na watu wengine."

Chanzo cha picha, KATE PARKER
Kate Parker ni wakili na Mkurugenzi wa Mradi wa School Consensual, ambayo inafundisha vijana juu ya idhini. Alisema wengi walishangaa kupata aina hii ya ubakaji katika sheria ya Uingereza.
"Kwa sababu katika kesi ya kuibiwa, mmoja wa wahusika amekubali kufanya ngono kwa kutumia kondomu, kwa hivyo ukiondoa kondomu, si kwamba walikubaliana hivyo - na huu ni ukiukaji."
Alisema pia hii inafungua mjadala mpana juu ya kuheshimu mipaka, na inapaswa kufundishwa katika mtaala.
"Hivi sasa, elimu ya ngono inafundishwa katika shule [za Uingereza], lakini masomo juu ya idhini sio lazima. Lakini nadhani ridhaa ni muhimu sana katika elimu ya ngono na vijana hawafundishwi vya kutosha."
"Kuibia kunaweza kuharibu maisha ya mtu"
Kwa Gemma, kuiba kulikuwa kumeharibu maisha yake.
"Ilinibidi kuhama baada ya tukio hilo, kwa sababu kukaa katika jengo moja kuendelea kunikumbusha juu ya kile kilichotokea, nilihitaji tiba ili kuimaliza."
"Kuibia kunaweza kuharibu maisha ya mtu na tunahitaji kuwaambia watu zaidi juu ya hii."













