Madhila wanayopitia wasichana wanaobakwa Ecuador

Cecilia Tombesi
Maelezo ya picha, Cecilia Tombesi

Uamuzi uliotolewa na mahakama ya kikatiba huko Ecuador mnamo mwezi Aprili uliweka wazi ufafanuzi wa kutoa ujauzito kwa waathirika wanawake wa ubakaji na kurejesha tena kumbukumbu wanazolazimika kuzipitia wasichana hao mikononi mwa jamaa zao.

"Hakuna anayeona, hakuna anayesikia wala hakuna anayesema chochote hasa katika maeneo ya kijijini."

Hayo yalikuwa maneno ya mwisho wakati wa mahojiano.

Fuatilia simulizi ya Sarita, mama wa watoto wanne sasa hivi.

"Sikuwa kufikiria kuhusu utoaji mimba. Lakini juu ya kumtupa, ndio," amesema Sarita.

Chanzo cha picha, Matias Zibell/BBC

Maelezo ya picha, "Sikuwa kufikiria kuhusu utoaji mimba. Lakini juu ya kumtupa, ndio," amesema Sarita.

Mara ya kwanza ilikuwa ni kutokana na ubakaji, watoto wawili katikati ni kutokana na uhusiano ambao tu ndio umekamilika na wa mwisho alizaliwa na dada mdogo wa Sarita aliyebakwa na mtu huyo huyo.

Ni rahisi kusahau kuwa umri wake ni chini ya miaka 25 lakini alikoma kuwa miongoni mwa kundi hilo la watoto pale baba yake wa kambo alipombaka kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 10.

"Leo hii naogopa sana giza licha ya kwamba ni mtu mzima," amesema.

Giza hilo linamkumbusha aliyoyapitia wakati ule.

"Waliponishika kwa nguvu na kutaka kunifanya vibaya, nilikataa. Hata kuna kipindi niliwahi kutoroka bila kujua ninakokwenda. Wakanipata na ikawa kama shehere kwao. Nilichapwa (vizuri tu). "

Kukosa uelewa

Aprili 28, mahakama ya kikatiba huko Ecuador iliamua kuruhusu uavyaji mimba katika kesi zote za ubakaji na sio tu kwa waathirika waliokuwa wanawake wenye matatizo ya akili kama ilivyokuwa awali.

Aprili, makumi ya wanawake walikusanyika katika Mahakama ya kikatiba kusubiri uamuzi.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Aprili, makumi ya wanawake walikusanyika katika Mahakama ya kikatiba kusubiri uamuzi.

Uamuzi huo ulisababisha mjadala mkali kati ya wanaounga mkono na wanaopinga uhalalishaji wa uavyaji mimba ambao umekuwa kukifanyika miaka ya hivi karibuni katika nchi za Amerika Kusini.

Lakini pia ilikumbusha Ecuador unyama wanaopitia wasichana waliovunja ungo ambao ni waathirika na dhuluma za kimapenzi, hasa katika maeneo ya vijijini ambapo mara nyingi wanaowatendea unyama huo wanakuwa ni wazazi wao, wajomba, kaka zao, mababu zao au wazazi wa kambo.

Wasichana ambao, kama anavyosema, wakili Ana Vera wa shirika la kutetea haki za ngono na afya ya uzazi kupitia BBC Mundo, "hawana taarifa kuhusu jinsi miili yao inavyobadilika, kwahiyo, huwa hawatambui kinachoendelea hadi pale wanapojishtukia kuwa na ujauzito tena baada ya miezi kadhaa kupita."

"Sikujua kama ni mjamzito. Nilichokuwa nafahamu ni kwamba tumbo langu linaongezeka tu lakini sikuelewa kwanini," Sarita anakumbuka.

Baada ya kujifungua, alimuacha mtoto wake kwenye daraja lakini kwasababu hakuna aliyemuokota, alirejea kumchukua.

Takwimu

Picha hii ilipigwa mwaka 2019 katika maandamano yaliyokuwa yanaunga mkono uavyaji mimba yaliyofanyika nje ya bunge la Ecuador.

Chanzo cha picha, RODRIGO BUENDIA/AFP via Getty Images

Maelezo ya picha, Picha hii ilipigwa mwaka 2019 katika maandamano yaliyokuwa yanaunga mkono uavyaji mimba yaliyofanyika nje ya bunge la Ecuador.

Kulingana na utafiti asilimia 32.7 ni waathirika wa dhuluma za kingono ingawa Ana Vera anaamini kwamba " matukio haya hayaripotiwi kwasababu ya unyanyapaa na mfumo mbaya wa sheria.

Kama ilivyo kwa Sarita, mbakaji ni mwanaume ndani ya nyumba, Waathirika pia huwa hawaripoti visa hivyo kwasababu mara nyingi watendaji wa uovu huo, huwa ndio vyanzo vya mapato nyumbani.

Wakati mwingine huwa hawaaminiwi kwasababu wanachukuliwa kuwa wasichana tu.

"Mama yangu aliamua kunyamaza tu," amesema Sarita.

"Nilipomwambia kilichotokea, nakumbuka kuna kitu alichokuwa anadai kutoka kwa aliyenitendea kitendo hicho, lakini hata ilifika wakati akawa anasema yote yaliyotokea ni makosa yangu.

"Baadaye, katika mahojiano haya, Sarita atasema kuwa ana uhakika kabisa kwamba hata mama yake alinyanyaswa.

Mwaka 2020, wasichana 1,631 waliokuwa kati ya miaka 10 na 14 walijifungua watoto huko Ecuador. Lakini idadi hiyo haijumuishi wale ambao walitoa mimba au waliokuwa na matatizo ya kuwazuia kupata mimba.

Mwaka jana ndio kipindi kilicho shuhudia idadi ndogo ya watu katika kipindi cha miaka 10 lakini pia ndio kipindi ambacho waathirika na waekelezaji wa uhalifu huo walifungiwa pamoja kwasababu ya corona.

Idadi ya walioathirika mwaka huu (2021) bado haijatambulika.

Kushiriki ngono na jamaa yake

Sarita alipata mtoto akiwa na umri wa miaka 13, alibakwa kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 10 lakini alianza kuwa na hofu ya kunyanyaswa kingono na jamaa yake akiwa na miaka 7 pale aliposhuku kwamba baba yake ana mnyanyasa binamu yake.

"Baada ya kufikiria tena, sasa nahisi kuwa ningejua mapema. Lakini watoto husahau kwa urahisi," anasema.

Ingawa hiyo haikuwa sababu ya kutengana kwa wazazi wake haikuwa hiyo badala yake ilikuwa mashambulizi dhidi ya mama yake.

"Nakumbuka mama yangu wakati mchana unawadia alikuwa na hofu sana kwasababu tayari alikuwa amejua nini kitatokea: wakati mwingine angekuja kama amelewa, amevuta na moja kwa moja kuanza kumpiga."

Na baada ya kutengena huku wakirejeleana mara kadhaa, ilifika wakati wazazi wake wakaamua kutengana kabisa. Baba yao akasalia na watoto wawili, mmoja wa kike mmoja wa kiume. Huku mabinti wawili wakienda na mama yake ambaye aliolewa na mwanamume mwengine, Sarita na dada yake mdogo

Baba yake wakambo alibaka wasichana wake na kuwatia mimba wote.

"Nafikiri dada yangu ni mkakamavu kweli, " Sarita anasema, "fikiria, mtu una muita baba yako, na kila siku anakufanyia kitendo hichi, sio haki kabisa."

"Nafikiri wanaume hawa wameharibika akili kwasababu wanaharibu maisha ya mtu."

Kina baba wanaobaka watoto wao

Ecuador, kuzaa na jamaa yako wa karibu kumefanyiwa utafiti kidogo sana kwasababu hakuchukuliwi kama uhalifu, ingawa kunasemekana kuchochea ukosefu wa maadili, amesema mwanasakolojia Fernanda Porras.

Abogada Ana Vera

Chanzo cha picha, Matias Zibell/BBC

Maelezo ya picha, Wakili Ana Vera ana amini kwamba visa vya unyanyasaji dhidi ya wasichana na wanawake "haviripotiwi".

Kwa Ana Vera, ukweli wa kuwa sio mfumo wa afya, wala mfumo wa elimu, au wa haki ulioweza kubaini kwamba wasichana wanne wananyanyaswa yaani Sarita, dada zake wawili na binadmu yake, hilo linaonesha kushindwa kwa taifa kulinda watoto hasa katika maeneo ya vijijini.

Sarita hakuweza kuendelea na masomo baada ya kujifungua na sasa hivi BBC Mundo imebaini kuwa ndio amefungua akaunti yake ya benki kwa mara ya kwanza maishani kwasababu ndio njia pekee ya kupata malipo ya uzeeni ya aliyekuwa mchumba wake.

Kwahiyo hali ya kiuchumi ilijitokeza kuwa kama sababu ya mtu kuchagua kutoa mimba.

"Sikufikiria kuhusu kuavya mimba. Lakini ndio, nilitaka kumtupa mtoto." Sarita amesema.

"Katika maeneo ya vijijini utasikia wasichana wengi wanakunywa dawa za miti shamba nia ikiwa ni kutoa mimba lakini wanaishia kumdhuru mtoto na kujidhuru wenyewe, mwisho wa siku wote wawili wanafariki dunia," anasema.

Kulingana na Sarita:

"Msichana ana haki ya kufanya maamuzi. Wakati mwingine familia haitaki kuchukua uamuzi huo licha ya kila kitu kilichomtokea. Lakini yeye mwenyewe ndiye anayetakiwa kufanya maamuzi."

Vitendo vya utoaji mimba

Uamuzi wa mahakama ya kikatiba ulifanyika baada ya kuwasilishwa kwa madai kadhaa na makundi ya wanaotetea haki za wanawake

Chanzo cha picha, Rafael Rodriguez/NurPhoto via Getty Images

Maelezo ya picha, Uamuzi wa mahakama ya kikatiba ulifanyika baada ya kuwasilishwa kwa madai kadhaa na makundi ya wanaotetea haki za wanawake

Kwahiyo hali ya kiuchumi ilijitokeza kuwa kama sababu ya mtu kuchagua kutoa mimba.

"Sikufikiria kuhusu kuavya mimba. Lakini ndio, nilitaka kumtupa mtoto." Sarita amesema.

"Katika maeneo ya vijijini utasikia wasichana wengi wanakunywa dawa za miti shamba nia ikiwa ni kutoa mimba lakini wanaishia kumdhuru mtoto na kujidhuru wenyewe, mwisho wa siku wote wawili wanafariki dunia," anasema.

Kulingana na Sarita:

"Msichana ana haki ya kufanya maamuzi. Wakati mwingine familia haitaki kuchukua uamuzi huo licha ya kila kitu kilichomtokea. Lakini yeye mwenyewe ndiye anayetakiwa kufanya maamuzi."

Hali ilivyo kijijini

Tajriba ya Vera katika maeneo ya vijijini, ni vigumu sana kupata malalamiko ya kuhusu ubakaji kwasababu hakuna waendesha mashitaka.

Chanzo cha picha, Matias Zibell/BBC

Maelezo ya picha, Tajriba ya Vera katika maeneo ya vijijini, ni vigumu sana kupata malalamiko ya kuhusu ubakaji kwasababu hakuna waendesha mashitaka.

Ana Vera anasema ni vigumu zaidi katika maeneo ya vijijini kuwasilisha malalamiko ya ubakaji hasa kwasababu hakuna waendesha mashitaka na katika visa vya aina hii mara nyingi jamii humgeukia aliyewasilisha malalamishi.

Na pia utofauti unaojitokeza kati ya nchi na mji sio tu wakati wa mwanzo wa ujauzito kwa watoto wadogo lakini pia mwishoni.

Vituo vya afya katika maeneo ya vijijini mara nyingi huwa havina uwezo wa kufanya upasuaji na njia inayopendekezwa hutegemea na ukubwa wa mwili wa mama.

Vilevile, katika maeneo ya vijijini sio tu ni vigumu zaidi kufikia huduma za afya lakini pia taarifa kitu ambacho Sarita anakubaliana nacho.

"Ukilinganisha mtoto wa kijijini na yule wa mjini, wa kijijini anakuwa hana hatia mara elfu moja," anasema.

"Msichana wa mjini anajua kwasababu ameelezewa kila kitu. Ila msichana wa kijijini hajui kipi ni kibaya au kipi kizuri na ikiwa atasema kitu watamkabili vilivyo na itakuwa vyema ikiwa atanyamaza."

"Nafikiri, wakati umewadia kwa wazazi wa kijijini kubadilika."

Mwisho wa mahojiano, Sarita anasema kuwa anachotaka ni kuhama eneo anaolishi na kwenda kuishi kwingineko peke yake.

Anaongea anachokiamini

Kwa Ana Vera, Ecuador ni mfano wa namna mwanamke ama mama alivyo nchini humo.

Chanzo cha picha, Matias Zibell/BBC

Maelezo ya picha, Kwa Ana Vera, Ecuador ni mfano wa namna mwanamke ama mama alivyo nchini humo.

Anasema kuwa wakati mwingine anapendelea watoto wake kuwa karibu naye zaidi ya majirani.

"Wakati mwingini naangilia watu wakubwa wakiwa wanaongea na rafiki zangu wadogo. Kisha nina waambia waende mbali na mimi."

"Najua fikra zangu ndio mbaya," anakubali. "Najua haiwezi kuwa sawa lakini bado hakuna uaminifu. Najiangalia na kusema: 'Kilichonitokea, kimenitokea.'

Namna ya kutokomeza unyanyasaji?

Anaamini kwamba sababu ya kilichomtokea ni kuweza kuzungumza na watoto wake.

"Kile ambacho nimeelezea watoto wangu ni kwamba hakuna ambaye anaweza kuwagusa na ikiwa itatokea ni lazima wamuelezee," anasema.

"Nimemuelezea mtoto mkubwa kuwa hivi karibuni ataanza kupata hedhi na kwamba asiogope kwasababu ni kawaida na hakuna anayestahili kumtongoza au kugusa mwili wake," anaendelea.

"Hadi kufikia sasa naweza kusema siko nilivyokuwa, lakini ni wakati na mimi nijiendeleze zaidi."

"Lazima nimwambie kuwa wanaume haijalishi umri, huwa wanatafuta uhusiano tu wa muda, na baada ya hapo wanaondoka. Wanachotaka ni kuwaumiza moyo tu. Na hilo sio sawa."

"Na kwamba yeye amejaaliwa kuwa na mwenza wake na watoto, lakini yote hayo ni kwa nia njema. Kufikia hapo acha iwe maamuzi ya msichana wala sio ya mwingine."