Bwawa la mto Nile:Maji ya mto huu yanatishia kuleta vita kati ya Misri,Ethiopia na Sudan

Bwawa katika picha ya mwezi Septemba mwaka 2019

Chanzo cha picha, Reuters

Mzozo wa muda mrefu kati ya Misri, Sudan na Ethiopia kuhusu bwawa kubwa la umeme linalojengwa kwenye Mto Nile hauoneshi dalili yoyote ya kutatuliwa. Siku ya Alhamisi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litajadili kwa mara ya kwanza, kwani wengine wanahofia inaweza kusababisha mzozo.

Misri na Sudan zote zimelalamika kwamba Ethiopia imechukua hatua ya kujaza bwawa la mto huo.

Misri, inategemea kwa kiasi kikubwa mto Nile kwa usambazaji wake wa maji. Mwaka jana, usambazaji wa maji wa Sudan ulivurugwa na kujazwa kwa bwawa, wakati Ethiopia inaiona kama njia ya kuleta umeme kwa mamilioni ya raia wake.

Transparent line

Katika taarifa mapema wiki hii Misri na Sudani zilituhumu Ethiopia kwa shughuli za ujazaji maji uliokuwa na "nia mbaya" - ikidokeza kuwa bwawa lilikuwa linajazwa kwa makusudi.

Haiwezi kusimamishwa?

Hapana. Kwa kawaida wakati wa msimu wa mvua Blue Nile, kwa asili hujijaza maji, msimu ambao tayari umeanza na unadumu hadi mwezi Septemba.

Kwa kuzingatia hatua ambayo ujenzi uko, "uhandisi, fizikia hakuna njia ya kusimamisha ujazaji sasa" hadi kiwango cha maji kufikia kilele cha ukuta wa bwawa, Mohammed Basheer wa Chuo Kikuu cha Manchester, ambaye amekuwa akitafiti bwawa hilo kwa muongo mmoja uliopita, aliiambia BBC.

Hii ni kwa sababu maji mengi yanaingia kwenye eneo la bwawa kuliko ujazo wa maji ambayo yanaweza kupita kwa njia ya vituo viwili vya wazi kwenye ukuta wa bwawa (mita za ujazo milioni 60-110 kwa siku).

Kuanzia mwanzo wa mchakato mnamo 2011, bwawa hilo limejengwa karibu na Blue Nile wakati linaendelea kutiririka kupitia eneo kubwa la ujenzi.

Wajenzi walifanya kazi kwenye miundo mbinu mikubwa kila upande wa mto bila shida yoyote. Katikati, wakati wa kiangazi, mto huo ulibadilishwa kupitia vinu, au mabomba, ili kuruhusu sehemu hiyo ijengwe.

Sehemu kubwa ya katikati sasa imekamilika na kila mwaka itaongezwa zaidi hadi karibu mwaka 2024 wakati itakuwa katika mita 640 juu ya usawa wa bahari. Sehemu ya chini ya mto kwenye eneo la bwawa ni karibu mita 509 juu ya usawa wa bahari.

Hatua gani inafuata?

Katika mwaka wa kwanza, Bwa la Mto Nile lilihifadhi mita za ujazo bilioni 4 za maji, akichukua hadi urefu wa sehemu ya chini kabisa kwenye ukuta wa bwawa wakati huo.

Kwa wastani, mtiririko wa jumla wa Blue Nile kwenye bwawa la mto Nile ni mita za ujazo bilioni 49, lakini mwaka jana iliona rekodi ya miaka 100 ya kilele cha mtiririko wa maji wa kila siku, ikionesha kwamba ni sehemu ndogo tu ya ujazo wa maji wa kila mwaka kilichozuiwa.

Ingawa uhandisi wa bwawa inamaanisha kuwa hifadhi ingejazwa mwaka jana hata hivyo, Ethiopia iliongeza kasi kwa kufunga njia tatu kati ya nne za mchepuko chini ya ukuta wa bwawa, alisema Bwana Basheer .

Raia wa Ethiopia walifanya maandamano mengi kwa kile ambacho wanaona Misri inaingilia bwawa lao

Chanzo cha picha, AFP

Mwaka huu wazo la awali lilikuwa kuongeza mita za ujazo bilioni 13.5 zaidi lakini picha za satelaiti zilizochambuliwa hivi karibuni na Sudan zinaonesha kwamba ukuta wa bwawa haujajengwa kwa kiwango cha juu kama ilivyopangwa hapo awali, ambayo inamaanisha maji mengi yatapenya.

Hatahivyo, barua kutoka kwa wizara ya maji ya Ethiopia kwenda Sudan iliyotumwa mapema wiki hii ilionesha kuwa bwawa hilo lilikuwa bado liko njiani kuzuia kiwango sawa na vile ilivyopangwa hapo awali.

Katika msimu wa kiangazi hifadhi itapungua kidogo, ikiruhusu ukuta wa bwawa kujengwa na katika mwaka wa tatu maji zaidi yatahifadhiwa.

Ethiopia inasema itachukua miaka minne hadi sita zaidi kujaza hifadhi hiyo kwa kiwango cha juu cha msimu wa mafuriko cha mita za ujazo bilioni 74.

Kati ya kila msimu ujao wa mafuriko hifadhi itashushwa hadi mita za ujazo bilioni 49.

Kwanini Misri haifurahishwi?

Misri inaona bwawa hilo linaweza kutishia uwepo wake. Inategemea maji ya mto Nile kwa kiasi kikubwa hii inamaanisha ina wasiwasi sana juu ya kile kinachoweza kutokea.

Misri inataka dhamana ya ujazo fulani wa maji.

Wakati wa mchakato wa kujaza, Misri inaweza kulipa fidia upotezaji wa maji kwa kutoa maji zaidi kutoka Bwawa la Aswan, lakini wasiwasi unakuja mara tu bwawa litakapofanya kazi kikamilifu.

Sudan na Misri zina wasiwasi juu ya mtiririko wa maji ya Mto Nile katika miaka ijayo ya ukame

Chanzo cha picha, Reuters

Wakati hatua ya kujaza inakwisha, Ethiopia inasita kuunganishwa na takwimu ya kiasi gani cha maji ya kutolewa. Kipaumbele chake kitakuwa kuhakikisha kuwa kuna maji ya kutosha kuendeshea kile kitakacho kuwa bwawa kubwa zaidi la nguvu ya umeme barani Afrika.

Katika miaka ya kawaida, au juu ya wastani, mvua haipaswi kuwa shida, lakini Misri ina wasiwasi juu ya kile kinachoweza kutokea wakati wa ukame wa muda mrefu ambao unaweza kudumu miaka kadhaa.

Katika hali hiyo, ikiwa Ethiopia itazuia maji katika bwawa basi viwango katika bwawa la Aswan High vitaanza kushuka.

Na pia kuna swali juu ya ratiba za kujaza tena mabwawa mengine kwenye Mto Nile kutokana na ukame.

Hali ikoje kwa Sudan?

Katika miezi 12 iliyopita kauli ya Sudan juu ya bwawa imehama kutoka kukaribishwa na kuwa ya kutiliwa shaka.

Bwawa hilo, kwa nadharia, lingeweza kusaidia kudhibiti mtiririko wa Blue Nile na kuifanya Sudan isiwe na mafuriko mengi.

Lakini mwaka jana, Sudan ilishangazwa wakati Ethiopia ilipofunga njia tatu kati ya nne za kugeuza njia ya maji.

Hii ilisababisha viwango vya chini vya mto ambavyo viliharibu vituo vya kusukuma maji vya Sudan kwa ajili ya umwagiliaji na usambazaji wa maji.