Harufu yako inaweza kusema mengi kuhusu siri za mwili wako

Chanzo cha picha, MICHAL BIALOZEJ
Kuna taarifa nyingi kuhusiana na harufu ya mwili ya mtu kisaikolojia na kibaolojia lakini sababu nyingi watu huamua kuzipuuza.
Mfalme Louis XIV, wa Ufaransa France, alikuwa akipenda sana marashi.
Maua yalikuwa ya harufu mbalimbali katika kila chumba, samani na vyenginevyo vilinyunyizwa marashi na pia wageni walinyunyiza marashi kabla ya kuingia kwenye makazi ya kifalme.
Ama ikiwa ni kwasababu usafi wa mtu husika haukuwa katika kiwango alichokitaka kama inavyoweza kuchukuliwa hii leo au pengine alipenda sana kucheza na marashi, kinachoeleweka ni kwamba Louis alipenda sana harufu nzuri.
Harafu ya mwili inaweza kuonesha mengi kuhusu afya yako kama vile uwepo wa magonjwa (Inasemekana harufu ya ugonjwa wa kuhara ni nzuri ikilinganishwa na ugonjwa wa kisukari inayochukuliwa kunuka kama matufaha yaliyooza).
"Harufu inaweza kutoa taarifa kuhusu lishe yako,'' amesema Mahmoud Mohamed, mtaalamu wa harufu na mwanasaikolojia katika chuo kikuu cha Macquarie nchini Australia, amesema. "Kuna mkinzano katika baadhi ya tafiti kuhusiana na hili lakini timu yangu imebaini kuwa kadiri unavyoendelea kula nyama nyingi ndivyo inavyoendelea kutoa harufu nzuri kwa miili yetu."
Matokeo ya Utafiti
Kulingana na utafiti uliofanywa na Mahmoud na timu yake, wanaume huona harufu ya miili ya wanawake inakuwa nzuri zaidi na kuvutia wakati wa kipindi chao cha hedhi hadi mayai yanapokuwa tayari.
Harufu yao inakuwa haipendezi wakiwa kwenye hedhi ikilinganishwa na kipindi mayai yako tayari. Huenda ilikuwa muhimu kwa mababu zetu kujua kipindi ambacho mwanamke ana uwezo mkubwa wa kuzaliana.

Chanzo cha picha, MICHAL BIALOZEJ
Aidha, kiwango cha homoni za testosterone cha wanaume pia huenda kiliongezea harufu
Na wakati harufu inaweza kubadilika kutegemea na lishe na afya ya mtu kikubwa kinachofanya harufu yetu kuwa ya pekee ni jeni au chembe za urithi.
Kila mmoja ana harufu yake ya mwili, huku mwanadamu akipewa uwezo mzuri mzuri wa kunusa harufu.
"Hili ni muhimu kwasababu inaonesha kuwa chembe za urithi zina ushawishi fulani katika namna tunavyonusa", amesema Agnieszka Sorokowska, mwanasaikolojia na mtaalamu wa masuala ya kunusa katika chuo kikuu cha Wroclaw nchini Poland, "kwahiyo, tunaweza kupata taarifa fulani za jenetiki kuhusu watu wengine kwa kuwanusa."
Gharama ya 'Kunukia'
Mwanadamu hutumia madola ya mabilioni kununua marashi katika jaribio la kubadilisha harufu yake halisi ya mwili.
Sorokovska na wafanyakazi wenzake wameonesha kuwa inawezekana kutathmini ya haiba ya mtu kulingana na aina ya marashi aliyochagua.
Na pia kuna uwezekano wageni wa Mfalme Louis XIV huenda walijifunza kitu kumhusu mfalme kwa kunusa tu harufu ya marashi wakati wanaingia.

Chanzo cha picha, MICHAL BIALOZEJ
Kwahiyo, mwanadamu hutumia taarifa za chembe za urithi zilizojificha katika harufu ya mtu kumchagua mpenzi wake? Hapana.
Kulingana na utafiti uliofanywa kwa karibu wachumba 3,7000, kuna uwezekano mkubwa watu wenye harufu mbili tofauti kabisa wakaoana. Tunaweza kuwa tunapenda harufu fulani lakini watu hawategemei harufi wakati wa kumchagua mwenza wako.
Majaribio mengi yaliofanywa ya harufu ya mwili yalihusiana na wanawake kutathmini fulana zinazovaliwa na waume zao.
Pia kuna utafiti mwingine uliofanywa, wanawake walioolewa walileta fulana za waume zao na wanawake wasio na waume wakaleta fulana za rafiki zao na fulana hizo zikachanganywa.
"Mwisho wa siku wanawake hawakuchagua fulana zilizokuwa na harufu wanazopenda," Mahmoud alisema.
Kwa hiyo, harufu ya mwili haikuwa na uhusiano wowote na mwenza wako.
"Kilichobainika mwisho ni kuwa, ikiwa unataka mwenza mwenye chembe za urithi nzuri, basi unachotakiwa kufanya ni kuwa makini na harufu zao za mwili,'' Sorokovska alisema. '' Lakini kwa watu wengi, hicho sio cha msingi tena na wengi hawakizingatii."













