Ndoa feki iliyompelekea mwanamume kutapeliwa dola 250,000

James and Irina
Maelezo ya picha, James na Irina
    • Author, Jonah Fisher
    • Nafasi, BBC Kyiv correspondent

Mfanyakazi mmoja wa shirika la misaada raia wa Uingereza alipomchumbia binti kutoka Ukraine, alifikiri kwamba anakwenda kuanzisha maisha mapya huko Odessa, lakini mambo yalikuwa tofauti.

Gari la James lilikuwa limepaki eneo moja linaitwa Villa Otrada. Mfanyakazi huyo mwenye umri wa miaka 52, akiwa na bashasha tele kushuhudia tukio alilolisubiri kwa miezi kadhaa.

Alikuwa na nyuso ya furaha, kumuona mchumba wake, Irina, akimsubiri nje ya mgahawa huo ulioko kando ya fukwe ya bahari ya Ukraine. Binti huyo mdogo kwa tofauti ya miaka 20, alikuwa mrembo akipambwa vyema na kuonekana mrimbwende kwa nywele zake za blonde.

Kando kidogo kulikuwa na watu ambao James aliamini kwamba ni wazazi wa Irina na wageni waalikwa takribani 60, wakiwa wamevalia vizuri na kupendeza.

James alishuka kwenye gari yake na kuanza kupigiwa makofi na kushangiliwa na wageni hao.

Ilikuwa Julai 2017, wakati ambazo msimu wa joto unaanza huko Odessa, huku meza nyingi zikiwa zimepangwa kwenye eneo zuri karibu na fukwe ya Villa Otrada.

Villa Otrada the wedding venue
Maelezo ya picha, Ukumbi wa Villa Otrada, ilipofanyika harusi feki ya Irina na James

Muda mfupi baadae, James na Irina walibadilishana viapo vya ndoa. Kile ambacho ungetegemea kuwa wakati mzuri wa kufurahia ukageuka shubiri. Usiku ule, James alikuwa amejikuta yuko peke yake amelazwa hospitali, akiwa hoi bin taabani kutokana na kinywaji kinachoelezwa kuwekewa dawa. Alifanikiwa kuoa, lakini si kwa mtu waliyempenda, bali kwa mtu mwingine na ilikuwa ndoa feki iliyopangwa.

Mkasa huu umemfanya mtu huyu kupoteza karibu akiba yake yote ya mali, pamoja na utu wake, bila usaidizi wa kisheria kutoka Ukraine.

James sio jina lake halisi. Mpango wake huu wa ajabu hakumweleza mtu yoyote hata familia yake. BBC imethibitisha hilo kupitia nyaraka zake za Benki taarifa zake rasmi, meseji na kuwahoji baadhi ya watu waliohusika moja kwa moja na mpango huo.

Ukraine ni moja ya nchi maskini Ulaya, ikiwa na wastani wa ujira wa dola 350 kwa mwezi. Sekta ya kufatufa wachumba na mahusiano inakuwa kwa kasi nchini humo. Wapo wanaotumia barua pepe, wanaokutana uso kwa uso, ambapo raia wengi kutoka Ulaya wanalipa maelfu ya dola ili kukutana na mabinti au wake watarajiwa wa Ukraini.

Lakini James anasema hakuja Odessa kutafuta mpenzi.

Kama mfanyakazi wa mashirika ya misaada nchini Uingereza, aliombwa na rafiki yake mwaka 2015 kumsaidia kuanzisha mradi wa kusaidia watoto wanaokimbia vita Mashariki mwa Ukraine.

Kufanya kazi nje ya nchi kwa James ni jambo jipya, lakini akaamua kujitosa kwa msaada wa mkalimani anayeitwa Julia. Miezi michache baadae kukiwa hakuna kazi nyingi huko Odessa, Julia alimshawishi James kwamba anaweza kuingia kwenye mahusiano na mmoja wa marafiki zake.

Rafiki huyo ni Irina. Ana miaka 32, alikuwa anatokea Donetsk, moja ya majiji yaliyopo magharibi mwa Ukraine, ambalo kwa sasa linalokaliwa na wapiganaji wanaoungwa mkono na Urusi.

"Alinifahamisha kuhusu ndoa zake mbili zilizopita na kwa nini hakutaka tena kufunga ndoa na mwanaume wa Ukraine" anasema James.

Irina and James
Maelezo ya picha, Irina na James

Licha ya utofauti wao wa miaka 20, James na Irina walifurahia maisha, wakiwa na jamaa wa karibu. Irina alikuwa anazungumza kiingereza kidogo na James hakujua kabisa kirusi wala ki-ukraini, kwa hivyo kama ilivyo kawaida, Julia ndio alikuwa msaada mkubwa wa kuwaunganisha kama mkalimani akilipwa dola 107 kwa siku.

"Lilikuwa jambo la ajabu mtu kurudia kzungumza kila kinachosemwa, lakini tuliendana na kupatana sana," anasema James.

Kwa muda wa miezi sita, walikuwa karibu wakila raha katika maeneo mbalimbali, lakini hawakushiriki tendo la ndoa wala busu, kwa mujibu wa Irina ni kwamba hakuamini kushiriki tendo hilo kabla ya ndoa.

Kumvalisha pete ya uchumba Irina

Miezi minane kabla ya sherehe ya ndoa, wawili hao walivalishana pete ya uchumba katika ukumbi ule ule wa Villa Otrada. Vipande vya video vinaonyesha James na Irina wakicheza muziki taratibu kwa mahaba. Ulikuwa wimbio wa msanii Whitney Houston 'Could I Have This Kiss Forever). Ilikuwa Novemba 2016, ikiwa ni miezi 11 baada ya kuwa wapenzi.

Engagement ring
Maelezo ya picha, Pete ya Uchumba

"Alikua na akili sana na alitaka kutafuta fursa nje ya Ukraine.

James alianza kumlipia ada ya kozi ya lugha ya kiingewreza. Kwa maana ya kwamba imsaidie kwenye harakati zake za kwenda Uingereza.

Anasema James alipozungumza na watu wa Ubalozini, ilionekana ilikuwa ngumu kwa Irina kwenda Uingereza hivyo akaamua kuanzisha maisha Ukraine. "Ingelichukua miaka kuwezekana," anasema James.

James akaamua kuhamia Ukraine kuanza maisha mapya na Irina. Akaacha kazi na kuuza nyumba yake, na kwa ushawishi wa Irina wakaanza kutafuta makazi Odessa.

"Rafiki zangu wa Uingereza walinipongeza, wakiniambia ni hatua kubwa saasa nakwenda kuoa."

Lakini ukweli ndo kwanza matatizo ya James yalikuwa yanaanza.

Makazi ya kuishi

Kuhamisha fedha kutoka Uingereza kwenda Ukraine haikuwa rahisi na haifanyiki moja kwa moja. Kwa sababu ni nchi iliyogubikwa na rushwa na kashfa nyingi za wizi wa fedha, kuna udhibiti mkubwa, hivyo Irina akamshawishi James atume fedha kwenye akaunti ya kampuni ya rafiki yake anaitwa Kristina, ambaye ndiye mratibu wa harusi yao. James akatuma dola $200,000 kwa ajili ya kununua nyumba..

Kristina the wedding planner
Maelezo ya picha, Kristina, muandaaji wa harusi

Baada ya James kutuma fedha kwa Kristina. mambio yakaanz akubadilika. Irina akamfahamisha James kwamba ni ngumu kutoa hizo fedha kama si mume wa Kristina. ni kama kufuata tu utaratibuna itachukua dakika 10 kwa msajili.

James yuko njia panda. huku muda unakwenda na Irina anatishia kufuta mpango wa ndoa yao kama hawatakuw ana nyumba ya kuishi.

"Unataka nionekana mie changudoa mbele ya ndugu zangu.", yalikuwa maneno ya Irina kwa James.

"Nilisukumwa kwa vile kulikuwa na wageni 60 wa familia yake wameshaalikwa na walinambia ni rahisi kumpa talaka Kristina na kumuoa Irina',

Kwa hivyo, Julai 10 2017, kwa msukumo wa mchumba wake Irina, James akamuoa muandaaji wa harusi yao, Kristina Stakhova.

Irina alikuwa na furaha kwa tukio hilo.

Pesa zilitoka na wote Kristina na Irina wakamwambia James kwamba fedha zote dola 200,000 zimetumika kwa ajili ya kununua nyumba. Lakini baadae akagundua kwamba nyumba hiyo imetumia dola 60,000 tu na haikuw ayake ilikuwa nyumba inayomilikiwa kwa pamoja na mkewe wa ndoa feki, Kristina.

"Nilikuwa mjinga," alijiambia James baada ya kugundua hilo.

Siku ya ndoa

Siku moja baada ya kumuoa, Kristina, James akachukua taxi mpaka kwenye ukumbi wa Villa Otrada, akitamani kukamilisha yote kisheria, ikiwemo kumtaliki Kristina kabla ya kumuoa Irina chaguo lake awe mke wake kihalali. Kama kawaida James aligharamia kila kitu. ikiwemo gharama za dola 20,000 za ndoa yake na Kristina.

James akabaini kwamba, ndoa ile ilikuwa feki. Wageni 60 walioalikwa walilipwa kwenda kwenye ukumbi, hata mama yake Irina akajifanya kuwa mama yake na Julia, yule mkalimani. Yaani alikuwa ni James tu aliyeamini ndoa ile ni ya kweli, lakini wageni wote walikuwa wanajua ukweli kwamba ni ndoa feki.

James hakujua pia hata huyo Irina, alikuwa ana mumewe wa halali, alikuwa ameolewa na Andriy Sykov tangu August 2015, miezi mitatru kabla ya kukutana na James.

Kristina pia alikuwa ameolewa na mumewe anayeitwa Denys, ambaye hakuwa na shida kukubali mchezo huo. Taarifa zinasema Kristina alimtaliki Denys wiki tatu kabla hajasaini nyaraka za kuolewa na James. alitaka baada ya ndoa hiyo feki na James, baadae arejeane tena na Denys.

Julia and Irina on a night out with James at the opera
Maelezo ya picha, Julia na Irina wakiwa kwenye moja ya maeneo waliyotoka usiku na James

James anasema anachokumbuka usiku ule wa ndoa yake na Irina, alikuwa anacheza na aliyedhani ni mama yake na Irina, anaamini aliwekewa dawa.

James akajikuta Hospitali. Irina akigoma kwenda naye Hospitali na kesho yake akaanza kumlaumu kwa kunywa kupita kiasi na kumdhaliliusha mbele ya familia yake. Kwa muda Irina akajiweka mbali na James akisema na yeye pia alikuwa na matatizo ya kiafya ambaye James asingeweza kumtembelea.

"Niko Hospitali na huwezi kuja kwa sababu wewe sio mume wangu," Irina alimtumia meseji hii James. "Mkeo kihalali ni Kristina, kwa hiyo anayeruhusiwa kuniona ni mama yangu tu."

James akaendelea kumtua pesa zaidi ya dola 12,000 kugharamia matibabu yake.

Kilichomnusuru ni kupata taarifa za uhakika kwamba nyumba aliyodanganywa inagharimu dola 200,000 ukweli inagharimu dola 63,000 tu.

The apartment in Odessa
Maelezo ya picha, Hii ndiyo nyumba aliyonunua James huko Odessa

James akagundua ametapeliwa karibu dola $250,000, ambayo ni robo tatu ya akiba yake.

Hakuna haki

James aliripoti Polisi tukio hili, lakini mara zote nne alizokwenda na ushahidi wa meseji pamoja na nyaraka za kuhamisha fedha, Polisi wa Odessa walimcheka. Anasema Polisi wa Ukraine na hasa, utapeli wa ndoa feki si jambo la kipaumbele kwao.

Hata hivyo Irina na Kristina walichukuliwa kwa mahojiano, lichas ya ushahisi aliouwasilisha hakuna mashataka yaliyofunguliwa dhidi yao.

BBC iliwatafuta polisi wa Odessa kujibu kuhusu hili lakini walikagoma kutoa maelezo yoyote.

Alichoambulia James ni ile nyumba iliyonunuliwa kwa $63,000 , hafikirii kama inawezekana kurejeshewa dola $200,000 halizotoa.

Mr Papinyan
Maelezo ya picha, Bwana Papinyan

James anasema ameamua kueleza mkasa wake huu kwa BBC kama kutoa funzo ana onyo kwa watu wengine wanaotaka kutafuta wapenzi Ukraine. Robert Papinyan, mpelelezi binafsi amekuw amsaada mkubwa wa kusaidia kupatikana kwa taarifa zaidi za kiuchunguzi kuhusu mkasa huu.

Utapeli wa mapenzi

Kwa mujibu wa Action Fraud, utapeli wa mapenzi unahusisha watu kurubuniwa na kutoa pesa kwa matapeli huku wakiwaaminisha kwamba wako kwneye mahusiano ya kweli. Watu hao wanaweza pia kuwa kwenye uhusiano huo kwa uongo ili kukufanya uwaaamini. Kuwaepuka mara zote fanya yafuatayo;

  • Kuwa mdadisi, dadisi na uchukue tahadhari wakati wote unavyoambiwa kutuma pesa, hasa kama mmekutana kwenye mitandao.
  • Zungumza na familia yako na marafiki kuomba ushauri kama ya kufanya uamuzi wowote.
  • Huenda picha unayoiona kwneye akaunti ya mtandao husika siyo ya kweli, tumia mtandao kujua kama picha hiyo haijachukuliw akutoka sehemu nyingine.
  • Kama umekutwa na mkasa wa aina hii, usione aibu, hauko peke yako,wasiliana na Benki yako kw autaratibu wa kulinda fedha zako na pia toa taarifa kwa wahusika kwa hatua zaidi.