Benjamin Netanyahu :Komando aliyebadilika na kuwa Waziri Mkuu

Netanyahu is Israel's longest serving leader - and it's first to go on trial

Chanzo cha picha, EPA

Katika kipindi chake cha miaka 15 kama Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu ameweka historia mara mbili kwa kuwa kiongozi aliyehudumu kwa muda mrefu na ni wa kwanza kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu akiwa madarakani.

Akisifiwa na wafuasi wake kama "Mfalme Bibi" na kama "mtenda miujiza" kwa ustadi wake wa kushinda uchaguzi, kiongozi huyo wa chama cha Israeli mrengo wa kulia cha Likud anakabiliwa na changamoto kubwa wakati anapigania kusalia kwenye siasa huku akiwa anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi.

Mafanikio yake katika uchaguzi yamemfanya kutambulika kama mtu anayeweza kuihakikishia Israeli usalama dhidi ya mahasimu wake huko Mashariki ya Kati.

Amekuwa na msimamo mkali dhidi ya Palestina na kutoa kipaumbele kwa suala la usalama mbele ya majadiliano yoyote ya amani, na pia alionya muda mrefu tu juu ya hatari iliyopo kwa Israeli kutokana na Iran.

Kumbukumbu ya kaka yake aliyeuawa

Benjamin Netanyahu alizaliwa Tel Aviv mwaka 1949. Mwaka 1963 familia yake ilihamia Marekani pale baba yake, Benzion, mwanahistoria mashuhuri na mwanaharakati wa Kizayuni, alipopewa nafasi ya juu katika elimu.

Akiwa na umri wa miaka 18, alirejea Israeli na kujiunga na jeshi kwa miaka mitano alikohudumu kama nahodha katika kitengo cha juu cha makomando cha Sayeret Matkal.

Netanyahu (R) was a captain of the elite Sayeret Matkal commando unit

Chanzo cha picha, GPO VIA GETTY IMAGES

Alishiriki katika uvamizi wa uwanja wa ndege wa Beirut mwaka 1968 na kupigana vita mwaka 1973 vya Mashariki ya kati.

Baada ya kuhudumu jeshini, Bwana Netanyahu alirejea Marekani na kusomea shahada na shahada ya uzamili katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts.

Mwaka 1976, kaka yake Netanyahu, Jonathan, aliuawa na kusababisha uvamizi wa kuokoa wasafiri wa ndege waliokuwa wametekwa nyara na ndege ya Entebbe, Uganda.

Kifo chake kina athari kubwa katika familia ya Netanyahau na jina lake likaanza kujulikana sana Israeli.

Bwana Netanyahu alianzisha taasisi ya kukabiliana na ugaidi kama kumbukumbu ya kaka yake na mwaka 1982 na akawa naibu mkuu wa Israeli katika ujumbe uliokuwa Washington.

Na ghafla, Bwana Netanyahu akawa ameanza maisha mengine. Akiwa mzungumzaji mzuri tu wa lugha ya Kiingereza mwenye lahaja ya Marekani, akawa mtu maarufu katika vituo vya runinga vya Marekani na mtetezi wa kutegemewa wa Israeli.

Bwana Netanyahu alichaguliwa kaa mwakilishi wa kudumu wa Israeli katika Umoja wa Mataifa huko New York mwaka 1984.

Alivyoingia madarakani

Mwaka 1988, aliporejea Israeli, ndipo alipoanza kujiingiza katika siasa za ndani ya nchi hiyo na kushinda ubunge kupita chama cha Likud na kuwa naibu waziri wa mambo ya nje.

Baadaye, akawa mwenyekiti wa chama na mwaka 1996 na wa kwanza kuchaguliwa moja kwa moja kama Waziri mkuu wa Israeli baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa mapema kufuatia mauaji ya Yitzhak Rabin.

Netanyahu is known among his followers as King Bibi

Chanzo cha picha, Getty Images

Bwana Netanyahu pia alikuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi wa Israeli tangu kuanzishwa kwa taifa hilo mwaka 1948.

Licha ya kukosolewa vikali, makubaliano ya amani ya mwaka 1993 kati ya Israeli na Palestina, Bwana Netanyahu alitia saini makubaliano yaliyofikia kukabidhi asilimia 80 ya eneo la Hebron kwa mamlaka ya Palestina na kukubali kujiondoa katika ukingo wa Magharibi hatua iliyosababisha ukosoaji hata zaidi kutoka upande wa mrengo wa kulia.

Na akaondolewa madarakani mwaka 1999 baada ya kuitisha uchaguzi wa mapema miezi 17 kabla, akishindwa na kiongozi wa chama cha Labour Ehud Barak, aliyekuwa komanda wa Bwana Netanyahu.

Hasimu wake wa kisiasa

Bwana Netanyahu alijiuzulu kama kiongozi wa chama cha Likud na kurithiwa na Ariel Sharon.

Baada ya Bwana Sharon kuchaguliwa kuwa Waziri mkuu mwaka 2001, Bwana Netanyahu alirejea serikalini kwanza kama Waziri wa mambo ya nje na baadaye akawa Waziri wa fedha.

Mwaka 2005, alijiuzulu katika maandamano yaliyokuwa yanapinga Israeli kujiondoa eneo la Gaza ambalo ilikuwa inalikalia.

Na nafasi yake kurejea ikajitokeza tena mwaka 2005, kabla tu ya Bwana Sharon - kupata ugonjwa wa kiharusi na kuwa katika hali ya kupoteza fahamu - akajiondoa chama cha Likud ana kuanzisha chama chake kipya cha Kadima.

Matukio ya maisha yake

•1949 - alizaliwa Tel Aviv

•1967-73 - alihudumu kama nahodha komando wa jeshi

•1984 - akawa balozi wa nchi yake kwa Umoja wa Mataifa

•1988 - akaingia bungeni na serikalini

•1996 - akawa Waziri mkuu

•1999 - akapoteza uchaguzi

•2002-03 - akahudumu kama waziri wa mambo ya nje

•2003-05 - akahudumu kama waziri wa fedha; akajiuzulu juu ya suala la Israeli kujiondoa Gaza

•Dec 2005 - akashinda tena kama kiongozi wa chama cha Likud

•2009 - akarejea kwama waziri mkuu

•2013 - akachaguliwa tena kama waziri kuu

•2015 - akashinda awamu ya nne

•2019 - akashitakiwa kwa makosa ya ufisadi, ulaghai na ukiukaji wa uaminifu

•2020 - akaanza awau yake ya tano uongozini; na kukabiliwa na mashtaka

Bwana Netanyahu alishinda nafasi ya kuongoza chama Likud tena na kuchaguliwa kama waziri mkuu kwa mara ya pili Machi 2009.

Alikubali kusitisha ujenzi wa makazi katika ukingo wa magharibi kwa miezi 10 kitu ambacho hakikuwa kimewahi kutokea hapo kabla na kuwezesha mazungumzo ya amani na Palestina lakini majadiliano hayo yakagonga mwamba mwishoni mwa mwaka 2010.

Ingawa mwaka 2009 alikuwa ametangaza kukubali uwepo wa eneo la Palestina mkabala na Israeli kwa masharti, baadaye alibadilisha msimamo.

"Eneo la Palestina halitaundwa, sio kama watu wanavyolizungumzia hili. Halitawahi kutokea," aliambia kituo cha habari cha Israeli mwaka 2019.

Mzozo wa Gaza

Mashambulizi ya Palestina na hatua ya jeshi ya Israeli yamekuwa yakisababisha makabaliano mara kwa mara ndani na kuzunguka ukanda wa Gaza kabla ya baada ya Bwana Netanyahu kurejea ofisini mwaka 2009.

Mapigano kama hayo ndani tu ya miaka 12 yalizuka tena Mei 2021, na kusitishwa kwa muda kutokana na juhudi za vyama vya upinzani vinavyotaka Bwana Netanyahu ang'atuke madarakani kufuatia mfululizo wa uchaguzi kadhaa ambao haukuwa umekamilika.

Israel has fought four major conflicts with militants in Gaza

Chanzo cha picha, AFP

Ingawa wakati wa mapigano Israeli ilihitajika kuunga mkono Marekani, washirika wake wa karibu, uhusiano kati ya Bwana Netanyahu na Rais Barack Obama ulikuwa changamoto.

Uelewano wao ulikuwa chini pale Bwana Netanyahu alipohutubia bunge la Marekani Machi 2015, akionya dhidi ya "makubaliano mabaya" yaliyotokana na majadiliano ya Marekani na Iran juu ya mpango wake wa nyuklia.

Utawala wa Obama ulishutumu ziara kama wenye kuingilia kati na kuharibu.

Uhusiano wake na Trump

Kuingia madarakani kwa Donald Trump kama rais mwaka 2017 kulipekea uhusiano wa karibu kat ya Marekani na Israeli na ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, Bwana Trump alitangaza kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israeli.

Hatua hiyo ilisababisha hasira miongoni mwa nchi za Kiarabu - ambazo zilikuwa zinaunga mkono madai ya Paalestina ya kumiliki nusu ya eneo la mashariki mwa Jerusalem lililokaliwa na Israeli tangu mwaka 1967 katika vita vya Mashariki ya Kati.

Netanyahu found renewed political support from the US under Donald Trump

Chanzo cha picha, AFP

Januari 2020, Bwana Netanyahu alipongeza hatua ya makubaliano ya amani yaliyofikiwa na Trump kati ya Israeli na Palestina kama "fursa ya kipekee katika karne", ingawa yalikataliwa na Palestina na kuyataja kama yenye kuegemea upande mmoja.

Bwana Netanyahu pia alionana ana kwa ana na Trump juu ya Iran na kufurahishwa na uamuzi wa rais huyo wa kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya Iran mwaka 2018 na kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya kiuchumi.

Kukabiliwa na mashtaka

Baaada ya 2016, Bwana Netanyahu alikabiliwa na uchunguzi wa madai ya ufisadi, ulaghai, na ukiukaji wa uaminifu katika kesi tatu tofauti Novemba 2019.

Netanyahu anadaiwa kukubali zawadi kutoka kwa mfanyabiashara tajiri aliyetaka kupewa upendeleo.

Hata hivyo, Netanyahu amekanusha madai hayo na kusema kwamba yanachochewa kisiasa has ana wapinzani wake.

Alifunguliwa mashtaka Mei 2020, na kuwa waziri mkuu wa kwanza kupitia hali hiyo na kukatalia mbali wito kutoka kwa upinzani wa kutaka ajiuzulu.

Benny Gantz and Benjamin Netanyahu agreed to a coalition to tackle the coronavirus crisis

Chanzo cha picha, AFP

Hata wakati anakabiliwa na madai ya uhalifu, Bwana Netanyahu alinusurika uchaguzi mkuu mara tatu chini ya mwaka mmoja na kushinda awamu ya tano, akikubali kugawanya madaraka na mpinzani wake wa kisiasa Benny Gantz katika mazingira nadra sana ya umoja wa kitaifa ulioundwa kukabiliana na janga la virusi vya corona.

Hata hivyo, umoja huo ulisambaratika miezi minane baadaye na kusababisha uchaguzi wa nne ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Ingawa chama cha Likud kilishinda viti vingi, upinzani miongoni mwa vyama vingine vya mrengo wa kulia lakini kwa ujumla alishindwa kupata ushindi wa kumuwezesha kuwa waziri mkuu moja kwa moja na hivyo basi hatma yake ikawa ni yenye kutiliwa shaka.