Mzozo wa Israeli na Wapalestina: Israeli yaimarisha mashambulizi Gaza huku mzozo ukiingia siku ya tano

Israeli imeimarisha mashambulio katika Gaza, huku wanamgambo wa Palestina waliendelea kufyatua maroketi ndani ya Israeli katika siku ya tano ya makabiliano.
Jeshi la Israeli lilisema kuwa vikosi vyake vya anga na nchi kavu vilihusika katika mashambulio ya Ijumaa lakini havikuingia Gaza.
Video kutoka katika mji wa Gaza zinaonesha picha za usiku za anga lililojaa vimulimuli vya vilipuzi kutoka kwa ndege za kijeshi za israeli, maboti ya silaha na silaha nyingine.
Watu wapatao 119 wameuawa Gaza na wengine wanane wameuawa Israeli tangu mapigano yalipoanza Jumatatu.
Wakati huo huo, umati wa Wayahudi na Waisraeli-Waarabu wamekuwa wakipigana ndani ya Israeli, , na kumfanya rais wake kuonya juu ya vita vya wenyee kwa wenyewe.
Waziri wa ulinzi Benny Gantz aliamrisha "kuimarishwa " kwa vikosi vya usalama kumaliza ghasia za ndani ambayo zimesababisha kukamatwa kwa zaidi ya watu 400.
Polisi wanasema Waisraeli -Waarabu wamehusika na ghasia kwa kiasi kikubwa na wamepinga shutuma kwamba walikuwa wakishuhudia magenge ya vijana Kiyahudi wakizishambulia nyumba za Waarabu bila kuchukua hatua zozote.

Chanzo cha picha, Reuters
Ghasia za wiki hii mjini Gaza na israeli ni mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 2014. Zilikuja wiki kadhaa baada ya kuongezeka kwa hali ya wasi wasi katika eneo la Jerusalemu Mashariki ambapo hatimaye makabiliano katika eneo takatifu la Waislamu na Wayahudi yaliibuka . kikindi cha kijeshi cha Hamas, ambacho kinatawala mji wa rules Gaza,kilianza kufyatua maroketi baada ya kuitahadharisha Israeli kuondoka kwenye eneo takatifu, ambapo Israeli ilijibu kwa mashambulio.
Mjini Gaza, Wapalestina wanaohofia mashambulio ya vikosi vya Israeli wamekuwa wakikimbilia kwenye maeneo yaliyoko karibu na mpakani mwa Israeli. Wakazi waliokuwa wameondoka katika eneo la Shejaiya katika mji wa Gaza City wamesema makombora yamekuwa yakiangukia kwenye nyumba zao.
"Tulihisi kana kwamba tulikuwa katika filamu ya kutisha ," alisema mmoja wa wakazi wa eneo hilo Salwa Al-Attar, ambaye alitoroka makombora na familia yake. "Ndege zilikuwa juu yetu, na makombora ya wanamaji - na usingeweza kutembea. Watoto, wanawake na wanaume walikuwa wanapiga mayowe ."

Chanzo cha picha, Reuters
Jeshi la Israeli lilisema kuwa limefanya mashambulio usiku kucha kuharibu mtandao wa mahandaki wa Hamas "the metro", lakini hakuna jeshi lake lililoingia Gaza. Liliongeza kuwa -katika kipindi cha kuanzia Alhamisi jioni na Ijumaa asubuhi-makombora zaidi ya 220 yalifyatuliwa kutoka ukanda wa Gaza.
Kusini mwa Israeli, mwanamke mwenye umri wa miaka 87 alikufa baada ya kuanguka alipokuwa njiani kujikinga na mashambulio ya mabomu karibu na Ashdod. maeneo mengine ikiwa ni pamoja na Ashkelon, Beersheba na Yavne pia yalilengwa.
Wizara ya afya ya Gaza ilisema watoto 27 walikuwa miongoni mwa watu waliouawa tangu yalipoanza mapigano , na raia wengine wengi wameuawa. Wakazi wengine 600 wa Gaza wamejeruhiwa. Israeli inasema makumi ya wale waliouawa Gaza ni wanamgambo, na baadhi ya vifo vilisababishwa na na roketi zilizokwenda kimakosa kwenye maeneo ambayo hayakulengwa ya Gaza.

Chanzo cha picha, Reuters
Katika taarifa iliyotolewa mapema leo Ijumaa asubuhi, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alisema operesheni ya jeshi la nchi hiyo dhidi ya wanamgambo wa Palestina itaendelea kwa "muda mrefu kama ni ya umuhimu". Aliongeza kuwa Hamas italipa vikali, kama vile "vikundi vingine vya kigaidi".
Msemaji wa jeshi la Hamas alisema kundi hilo lilikuwa tayari kufundisha wanajeshi wa Israeli "masomo magumu" ikiwa itaamua kuendelea na uvamizi wa ardhi.
Siku ya Alhamisi, jeshi la Israeli liliita wanajeshi 7,000 wa akiba na kupeleka wanajeshi na vifaru karibu na mpaka wake na Gaza. Ilisema kuingia Gaza ilikuwa chaguo moja la kuzingatiwa lakini uamuzi bado haujafanywa.

Chanzo cha picha, Reuters
'Hatukutaka mzozo huu'
Wakati mapigano yalipoingia siku ya tano, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alitaka "kuondolewa mara moja na kukomeshwa kwa mapigano huko Gaza na Israeli".
Ombi lake liliunga mkono la wanadiplomasia wengine - pamoja na mshirika wa Israeli Marekani- lakini maombi hayo kwa viongozi wa Israeli na Wapalestina hadi sasa wameshindwa kuunda makubaliano ya kusitisha mapigano.
Afisa mwandamizi wa Hamas amesema kuwa kundi hilo liko tayari kusitisha mapigano ikiwa jamii ya kimataifa itashinikiza Israeli "kukomesha vitendo vya kijeshi" katika Msikiti wa al-Aqsa uliobishaniwa huko Yerusalemu.ael to "suppress military actions" at the disputed al-Aqsa Mosque in Jerusalem.

Chanzo cha picha, AFP
Hatahivyo, mshauri mwandamizi wa Bw Netanyahu aliiambia BBC kwamba wito wa kimataifa wa kuzuia matukio hayo unahitajika
"Hatukutaka mzozo huu, lakini sasa umeanza lazima uishe na utulivu," alisema Mark Regev. "Hiyo inaweza kupatikana tu kwa Israeli kuchukua Hamas - muundo wao wa jeshi, amri na udhibiti wao."
Israeli pia imeita kampuni 10 za doria za mpaka kusaidia kukabiliana na machafuko mabaya kati ya jamii za Waarabu na Wayahudi kwa miaka mingi.

Bwana Netanyahu amependekeza kuanzisha "kizuizi cha utawala" kwa waandamanaji. Hatua hiyo ya kutatanisha ingeruhusu mamlaka kuwashikilia watu kwa muda mrefu bila kuwashtaki.
Rais Reuven Rivlin alielezea kuzuka kwa ghasia katika miji na majiji kadhaa kama "vita vya wenyewe kwa wenyewe visivyo na maana".
Wakati huo huo, majaribio ya vyama nchini Israeli kuunda umoja kuchukua nafasi ya serikali ya Bw Netanyahu kufuatia uchaguzi wa Machi yanaonekana kuvunjika baada ya kiongozi muhimu wa mrengo wa kulia kukiondoa chama chake nje ya mazungumzo., vyombo vya habari vinasema.
Naftali Bennett sasa anafanya mazungumzo na chama cha Bw Netanyahu cha Likud kujaribu kuunda "serikali pana ya umoja wa kitaifa", kulingana na ripoti.












