Mabaki ya roketi ya Uchina ‘kulipuka’ duniani wikendi hii

Chanzo cha picha, Getty Images
Mabaki ya roketi ya China yanatarajiwa kuanguka na kulipuka duniani bila kudhibitiwa kwa namna yeyote wikendi hii.
Bado haijafahamika ni wapi au lini hasa mabaki hayo ya roketi yatalipuka.
Roketi hiyo kwa jina Long March 5B ilizinduliwa mwishoni mwa Aprili kubeba chombo cha kwanza cha China kitakachokuwa kuwa kituo cha anga za mbali siku za usoni kwenda kwenye mzingo wa dunia.
Mwili wa roketi hiyo sasa hivi unazunguka duniani na inakaribia kuungia kwenye anga la chini.
Kufikia Alhamisi, Marekani ilikuwa imesema inafuatilia njia ambayo chombo hicho inapitia lakini haina mpango wa kuidungua.
"Ni matumaini yetu kuwa itaangukia sehemu salama bila kumdhuru yeyote," amesema Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin. "Matumaini yetu ni kwamba itaanguka baharini, au sehemu nyengine kama hiyo."
Pia imeikosoa China ingawa sio moja kwa moja, na kusema "ni muhimu kuhakikisha tunazingatia mambo hayo wakati tunapanga kufanya uperesheni".
Chombo cha habari cha China kinachomilikiwa na serikali siku za nyuma kilipuuzilia mbali hofu ya kuwa chombo hicho kinaweza kulipuka kwenye makazi na kusema kuwa kitaangukia sehemu nyengine ya maji ya kimataifa.
Gazeti la Global Times limemnukuu mtaalam Song Zhongping ambaye aliongeza kuwa mtandao wa China wa kufuatilia anga la mbali atakuwa anafuatilia kwa karibu tukio hilo na kuchukua hatua stahili iwapo kutatokea uharibifu wowote.

Nini kitatokea?
Kwa sasa roketi hiyo inazunguka eneo la chini la dunia kumaanisha kuwa inazunguka karibu na dunia lakini taratibu inasukumwa chini.
"Kuisukuma kutapunguza kasi ya chombo hicho na kufanya kupunguza umbali wake na kuileta karibu anga zito, ambako kutasababishia msukumo zaidi na kupunguza kasi hata zaidi pamoja na kupungua kwa umbali wake," Jason Herrin kutoka shirikala ufuatiliaji wa dunia Singapore, ameliambia shirika la BBC.
"Mchakato huo ukishaanza, chombo hicho kitakuwa kwenye mwenendo wa kurejea duniani tu," amesema.

Chanzo cha picha, Reuters
Roketi hiyo inatarajiwa kwa kiasi kikubwa kulipuka wakati anga linaendelea kuwa zito zaidi takriban kilomita 0 kutoka usawa wa bahari. Sehemu ambazo hazitakuwa zimeungua kabisa zitaanguka duniani.
Ikiwa haya yote yataendelea bila kudhibitiwa, eneo ambalo roketi italipuka na kule ambako vifusi vita anguka hakuwezi kudhibitiwa wala kutabirika.
Roketi ya Long arch 5B iliyorushwa mwaka 2020, pia nayo mwili wake haukuweza kudhibitiwa na baadhi ya mabaki yake yalilipuka sehemu ya kijijini ya Ivory Coast.
Shirika la anga za mbali la China halijasema lolote kuhusu ikiwa roketi hiyo inadhibitiwa au kama itatua bila kudhibitiwa.
'China ilitumai kuwa itabahatika'
Mwanaanga Jonathan McDowell, wa kituo cha Harvard-Smithsonian cha fizikia ya angani, alisema suala la kutua bila kudhibitiwa ni moja ya "matatizo makubwa ya roketi aina ya Long March 5B".
"Roketi ndogo za Marekani na zile za daraja la juu za Ulaya pia hurejea bila kudhibitiwa (na kulipuka kabisa) lakini zile kubwa za Marekani na Ulaya huundwa kwa mfumo ambao haziwezi kuondoka kwenye mzingo wa dunia; yaani huwa zinatupwa kwa njia salama katika eneo la kwanza la mzingo wa dunia," aliiambia BBC.
"China iliamua itatumia muundo rahisi tu na kutumai kuwa itabahatika chombo hicho kurejea tena duniani bila kusababisha madhara yoyote."
Kurejea tena kwa roketi kutoka anga la mbali bila kudhibitiwa kulimaanisha kwamba roketi bado inaweza kudhibitiwa na timu husika, kwa mfano kupitia injini ya roketi. Kawaida mabaki hayo huwa yanaelekezwa eneo maalum kulipuka katikati ya bahari ambako ni mbali sana na watu.
Kwa njia hiyo, njia inayotumika na chombo inaweza kudhibitiwa na kurejea tena duniani kunaweza kuwa kwenye eneo lililotabiriwa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Malengo ya China anga za mbali?
Long March Rocket ya China ilianza safari Aprili 29 kutoka kituo cha anga la mbali cha China Wenchang.
Ilikuwa imebeba kile kitakachokuwa kituo cha kudumu cha anga za mbali kama sehemu ya China kuendelea kuongeza shughuli zake kwenye anga za mbali.
Mipango ya Beijing ilikuwa ni kuwa na angalau safari kama hizo 10 kubeba vifaa vyote kwenye mzingo wa dunia kabla ya kumalizika kwa kituo hicho kufikia mwaka 2022.
China pia ina mipango ya kujenga kituo cha mwezi kwa ushirikiano na urusi. China ilituma mwanaanga wake wa kwanza kwenye anga la mbali mwaka 2003.












