Marufuku ya Hijab: Fahamu mbona nchi hizi zinazuia uvaaji wa Burqa na Niqab

Uswizi limekua ni taifa la hivi punde kuzuia uvaaji wa vazi la kiislamu linalofunika uso mzima

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Uswizi limekua ni taifa la hivi punde kuzuia uvaaji wa vazi la kiislamu linalofunika uso mzima

Baraza la mwaziri nchini Sri Lanka limeidhinisha pendekezo la kupiga marufuku uvaaji wa burqa katika maeneo ya umma kwamsingi wa usalama wa kitaifa licha ya mtaalam wa umoja wa mataifa kusema kwamba itakuwani ukiukaji wa sheria za kimataifa .

Hata hivyo Sri Lanka sio nchi pekee ambayo imeamua kuchukua hatua ya kupiga marufuku mavazi hayo ya kiislamu .

Switzerland limekua ni taifa la hivi punde kuzuia uvaaji wa vazi la kiislamu linalofunika uso mzima na kubakisha sehemu ya macho tu linalofahamika kama niqab.

Sera zinazojaribu kudhibiti au kupiga marufuku niqab - na ufunikaji zaidi wa burqa -- zimejitokeza katika nchi kadhaa za Ulaya huku Ufaransa ikiwa nchi ya kwanza barani Ulaya kuweka marufuku ya uvaaji wa vazi hilo mwaka 2010.

Marufuku dhidi ya ufunikaji wa uso mara nyingi hulenga nguo ambazo hazioneshi umbo la uso wa mtu. Hata hivyo marufuku haihusu uvaaji wa barakoa wala kofia za pikipiki, bali zinalenga mavazi ya kidini, kama vile, niqab au burqa. Ndio maana huitwa "marufuku za burqa."

Ufaransa

Marufuku ya Ufaransa dhidi ya uvaaji wa nguo zinazofunika nyuso iliidhinishwa na Mahakama ya Muungano wa Ulaya

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Marufuku ya Ufaransa dhidi ya uvaaji wa nguo zinazofunika nyuso iliidhinishwa na Mahakama ya Muungano wa Ulaya

Marufuku ya Ufaransa dhidi ya uvaaji wa nguo zinazofunika nyuso iliidhinishwa na Mahakama ya Muungano wa Ulaya ya haki za binadamu mwaka 2014, ambayo ilikataa madai kuwa kuonyesha uso wote ni ukiukaji wa uhuru wa kidini. Nchi tofauti za Muungano wa Ulaya ,EU zina sheria na taratibu zake. Baadhi zimeweka marufuku ya uvaaji wa burqa.

Uholanzi

Iwapo utafunika uso wako kwa kitambaa nchini Uholanzi (Netherlands), unakabiliwa na uwezekano wa kulipa faini ya euro takriban 150, sheria hii inalenga uvaaji wa burqa na vitambaa vingine, lakini piakofia ya pikipiki helmeti na balaclava zinapofunika uso wote. Haijawa wazi iwapo mamlaka zitatekeleza sheria hiyo.

Miji mingi imesema kuwa haitatoza faini hiyo.

Uholanzi ilianzisha marufuku hiyo baada ya mjadala uliodumu kwa mika 14. Mwaka 2005 bunge la nchi hiyo liliidhinisha pendekezo la marufuku ya uvaaji wa burqas ambalo lilikuwa limewasilishwa bungeni na wabunge wa mrengo wa kulia -Geert Wilders. Na kuidhinisha sehemu ndogo ya muswada huo mwaka 2016.

Waholanzi wengi wanaiona sera hiyo kama ishara tu. Ni wanawake kati ya 200 na 400 wanaovaa burqa au niqab kila siku katika nchi yenye watu milioni 17.

Denmark

Kilemba kinachofunika uso mzima kimekuwa ni marufuku nchini Denmark tangu tarehe 1, Agosti mwaka 2018. Bunge la Denmark liliidhinisha kuwa sheria marufuku hiyo Mei, 2018 . Watu wanaovunja sheria hiyo hukabiliwa na faini ya hadi euro 134, ambayo inaweza kuongezeka iwapo makossa hayo yatarejelewa.

Austria

Vilemba vinavyofunika uso mzima vilipigwa marufuku nchioni Austria tangu mwaka 201 chini ya sheria inayofahamika kama Sheria dhidi ya uvaaji wa vilemba vya uso. Sheria inawaka watu konesha nyuso zao kuanzia kwenye kidevu hadi nywelezinapoishia. Ma eneo hilo halionekani, watakabiliwa na faini ya hadi euro 150.

Bulgaria

Sahar Al-Faifi alisema kuwa alikabiliwa na matusi kwa kuvaa niqab
Maelezo ya picha, Sahar Al-Faifi alisema kuwa alikabiliwa na matusi kwa kuvaa niqab

Sawa na Uholanzi, nchi ya Bulgaria ilianzisha marufuku ya burqa katika mwaka wa 2016. Wavaaji wa kilemba hicho wanakabiliwa na faini ya hadi euro 750 iwapo wataivunja sheria hiyo. Kana wachache wanaruhusiwa wakiwemo wachezaji wa michezo, baadhi wawapo kazini au wawapo katika michezo ya ndani.

Ubelgiji

Ubelgiji imepiga marufuku vilemba vinavyofunika uso mzima tangu Julai 2011. Yeyote anayevunja sheria anakabiliwa na hatari ya kupigwa faini au kifungo cha miaka hadi saba jela. Marufuku inawaathiri watu wachache sana. Kuna takriban watu 300 ambao wanavaa burqa au niqab nchini Ubelgiji, ambako ni nyumbani kwa waislamu takriban milioni moja.

Mijadala kwingineko

Nchi nyingine nyingi za Muungano wa Ulaya zimekwisha jadili , au zinajadili , marufuku ya vilemba vinavyofunika uso, ni pmoja na Ujerumani, Usiss, Estonia, Latvia, Lithuania na Norway. Badhi ya maeneo ya Uhispania yameanzisha marufuku dhidi ya burqa. Italia haijajadili bado juu ya htua hiyo. Nchi hiyo hata hivyo ilipiga marufuku nguo zote zinazofunika utambulisha wa mtu tangu miaka ya 1970.

Waislamu wanasemaje kuhusu marufuku za Burqa na Niqab ?

Sanija Ameti, mjumbe wa Jumuiya ya Waislamu wa Uswizi, ameiambia BBC kuwa kampeni -na mchoro wa wanawake wa kiislamu inayoonyeshwa kwenye mabango- - vimekuwa vikikera.

Mabango yaliyonadiwa na chama cha Swiss People yanaonesha mchoro wa mwanamke aliyevalia niqab nyeusi na maelezo kama "Acha itikadi kali!" na "acha uislamu wa mrengo mkali !"

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mabango yaliyonadiwa na chama cha Swiss People yanaonesha mchoro wa mwanamke aliyevalia niqab nyeusi na maelezo kama "Acha itikadi kali!" na "acha uislamu wa mrengo mkali !"

"Waislamu wengi sana Uswiss watahisi kutukanwa na sio sehemu ya jamii na kusukumwa mahali ambapo sio pao.Hatufanani na hawa wanawake walio katika picha hizi, hatufanani nao," alisema.

Unaweza pia kusoma:

Hatahivyo, jamii nyingine za Waislamu ziliunga mkono marufuku hiyo.

Imam Mustafa Memeti, kutoka jiji la Bern, aliiambia BBC kuwa anafikiria kuwa kilichochochea kampeni ya marufuku ilikuwa "labda ni chuki dhidi ya Uislamu ". Lakini akasema anaunga mkono marufuku hiyo kwasababu inaweza kusaidia kuleta ukombozi wa Waislamu wanawake Katika Uswiss.

Kwingineko duniani marufuku dhidi ya vilembo vya wanawake wa Kiislamu vinavyofunika uso imekuwa ikipingwa na Waislamu hususan nchi za Kiislamu katika mataifa ya Mashariki ya Kati.