Kuna tofauti gani kati ya mavazi ya hijab, niqab na burka?

Composite image of Muslim women wearing headscarves

Chanzo cha picha, AFP/Getty/Reuters

Hijab, niqab, burka kuna aina mbalimbali za mavazi ya kujifunika yanayovaliwa na wanawake wa kiislamu duniani.

Lakini si kila mtu hukubaliana navyo, na nchini Denmark, ulaya, marufuku ya kuvaa ushungi wenye kufunika uso ilianza kufanya kazi tarehe 1 mwezi Agosti

Denmark imeungana na Ufaransa na mataifa mengine baadhi ya Ulaya kupitisha amri hiyo.Waziri wa sheria wa Denmark Søren Pape Poulsen amesema ni lazima tuangalie. ishara ya uso wa kila mmoja wetu.

Wanawake wengine huvaa vilemba kufunika kichwa na nywele, huku wengine wakivaa burka au niqab, ambayo pia inafunika uso wao.

Hizi ni aina mbali mbali za mavazi ya ushungi

Mwanamke akiwa amevaa Hijab
Maelezo ya picha, Mwanamke akiwa amevaa Hijab

Neno Hijab linaeleza kitendo cha kujifunika kwa ujumla.Vazi hili huvaliwa na wanawake wa kiislamu.Vilemba hivi vinakuwa vya mitindo na rangi mbalimbali.Mara nyingi aina hii huvaliwa ikifunika kichwa na shingo lakini uso huwa wazi.

Mwanamke akiwa amevaa Niqab
Maelezo ya picha, Mwanamke akiwa amevaa Niqab

Niqab ni ushungi kwa ajili ya kufunika uso maeneo ya kuzunguka macho huwa yanaonekana,huvaliwa sambamba na kitambaa cha kichwani

Mwanamke akiwa amevaa Burka
Maelezo ya picha, Mwanamke akiwa amevaa Burka

Burka ni ushungi unaofunika uso na mwili, mara nyingi huacha nafasi machoni kidogo kwa ajili ya kuona.

Mwanamke akiwa amevaa Al-Amira
Maelezo ya picha, Mwanamke akiwa amevaa Al-Amira

Al-amira ni ushungi wa vipande viwili vikiwa vinavaliwa na kitambaa mithili ya kofia cha aina ya pamba au polista.

Mwanamke akiwa amevaa Shayla
Maelezo ya picha, Mwanamke akiwa amevaa Shayla

Shayla ni vazi refu,lenye umbo la mstatili maarufu katika maeneo ya Ghuba.Huzungushiwa kuzunguka kichwa kisha kubanwa na pini na kuegeshwa mabegani.

Mwanamke akiwa amevaa Khimar
Maelezo ya picha, Mwanamke akiwa amevaa Khimar

Khimar ni ushungi ambao huning'inia mpaka usawa wa juu ya kiuno.Hufunika nywele, shingo na mabega kabisa lakini uso huonekana vizuri.

Mwanamke akiwa amevaa Chador
Maelezo ya picha, Mwanamke akiwa amevaa Chador

Chador huvaliwa na wanawake wa Iran wanapokuwa nje ya nyumba, ni vazi la kufunika mwili mzima.Mara zote huvaliwa na kilemba kichwani kwa ndani