Nyota wa Liverpool Mo Salah asababisha chuki na gumzo mitandaoni kwa kupiga picha na mti wa Krismasi

Chanzo cha picha, Mo Salah/Instagram
Nyota wa Liverpool azua gumzo lililotanda chuki miongoni mwa mashabiki wake mitandaoni baada ya kuweka picha zinazoonesha ujumbe wa kusherehekea krismasi.
Mashabiki wa mshabuliaji huyo wa Liverpool na Misri Mohamed Salah wameandika ujumbe wa chuki kuonesha kutofurahishwa na kitendo chake kama nyota wa Kiislamu kutuma ujumbe wa krismasi akiwa pamoja na familia yake.
Salah, 28, aliweka picha mtandaoni zinazomuonesha yeye na familia yake wakiwa wamevalia vizuri na kusimama mbele ya mti wa Krismasi, na kwenye ujumbe huo akaweka emoji 2, na hashtag #MerryChristmas.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ujumbe wa Salah kwenye mtandao wa Instagram umepata 'likes' zaidi ya millioni 2.3 huku ujumbe wake kwenye Twitter wenye picha hizo hizo ukiwa na 'likes' zaidi ya 300,000.
Lakini pia ujumbe huo wa Salah umesababisha hasira kwa baadhi ya wafuasi wake Waislamu ambao wamehoji kuwa nyota huyo wa Kiislamu haruhusiwi kusherekea sikukuu ya Krismasi.
Moja ya jumbe zilizojibu ule wa Salah umeandikwa:
"Kama Muislamu hatustahili kusherehekea au hata kupongeza dini zingine wakati wanasherehe zao''.
Shabiki mwingine akamjibu:
"Hii ndio sababu [Nyota wa Arsenal na Misri] Mohammed Elneny ndio mfalme wa Misri na sio wewe" .
Wengine walioghadhabishwa na hatua ya Mo Salah ni kama ifuatavyo:
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Hata hivyo kuna waliojitokeza kumtetea.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Hatma ya Salah wiki hii imekuwa haitabiriki baada ya madai kuwa hakufurahia uwepo wake Liverpool na huenda akahusishwa na uhamisho wa Uhispania.
Hata hivyo, kocha wa Reds Jurgen Klopp amepuuzilia mbali madai hayo katika mkutano na wanahabari Alhamisi, akisema kuwa mchezaji huyo "yuko sawa" wakati timu hiyo inajitayarisha katika Ligi ya Premier na West Brom Decemba 27.
Salah amefunga magoli 16 baada ya kujitokeza mara 21 katika mechi za Liverpool msimu huu.
Kila alipopata goli, Mo Salahi alisujudu, kitendo kinachoashiria yeye ni Muislamu.












