Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020: Kuwa na rais Trump siku aliyoshindwa

Trump akiwasili katika Ikulu ya whitehouse baada ya kucheza gofu

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika kipindi cha miaka minne iliopita , nimemuona rais Donald Trump katika siku nzuri na katika siku mbaya . lakini tarehe 7 mwezi Novemba , siku ambayo alipoteza uchaguzi ilikuwa siku tofauti kabisa.

Akiwa amevalia suruali nyeusi ,na kofia nyeupe ilioandikwa Make America Great Again MAGA , rais aliondoka katika ikulu ya whitehouse dakika chache kabla ya saa nne.

Alikuwa amuhudumia kipindi kirefu cha siku yake akituma jumbe zwa twitter kuhusu udanganyifu aliodai kufanyika katika uchaguzi.

Aliingia katika gari jeusi na kuelekea katika klabu yake ya kucheza gofu , Trump National Sterling , iliopo huko Virginia takriban kilomita 40 kutoka Ikulu ya Whitehouse .

Wakati huo alionesha matumaini . Ilikuwa siku nzuri kwa kucheza gofu na alikuwa anaenda kuhudumia siku hiyo katika klabu hiyo.

Lakini watu waliokwa wakimfanyia kazi waliathiriwa na matokeo hayo.

'Je unaendelejae', nilimuuliza mmoja ya wafanyakazi wake . 'Nashukuru'. alijibu . Alitabasamu. Lakini macho yake yakatazama simu yake.

Machungu ya uchaguzi

Ikulu ya Whitehouse imepitia kiwewe siku baada ya uchaguzi.

Ni Siku ya Jumanne ilikuwa kama siku nyingi. Maeneo mengi ya kukalia na kufanyia kazi katika eneo la West Wing yalikua hayana watu wakati nilipozuri jumba hilo siku ya Jumamosi.

Wafanyakazi kadhaa walikuwa wameambukiuzwa virusi vya corona na walikuwa nje ya afisi. Wengine walikuwa wamejitenga.

Na kuanzia mwendo wa saa tano na nusu , wakati rais alipokuwa katika uwanja wa kucheza gofu , BBC na mitandao mengine ya Marekani ilianza kusema kwamba Biden ndiye mshindi.

Jinsi vyombo vya habari vya Marekani vilivyoripoti ushindi wa Biden

Nilikuwa nimeekti katika mkahawa mmoja wa kitaliano yapata maili moja kutoka katika klabu hiyo niliposikia habari hizo.

Mimi ni mmoja wa wanachama wa vyombo vya habari vya Ikulu ya Whitehouse, idadi ndogo ya wahandishi habari ambayo hutembea na rais.

Sote tulikua tukimsubiri kutoka katika uwanja huo wa gofu. Wengine walishangazwa kwanini rais angeondoka katika klabu hiyo na kwenda katika Ikulu ya whithouse.

Saa zilizpita na masaa pia yakayoyoma.

'Anachukua muda wake', alisema afisa mmoja wa kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa polepole, kwa mwenzake.

Rais hakuwa na haraka ya kuondoka katika klabu hiyo, alikuwa amezungukwa na marafiki zake.

Nje ya lango kuu , wafuasi wake walitupigia kelele na kutushutumu.

Mwanamke mmoja aliyekuwa amevalia viatu virefu vyekundu na kitambaa cha rangi ya buluu kilichosoma: 'wacheni wizi'.

Mtu mwegine aliendesha gari lake ndani ya klabu hiyo na mbele yetu ikipeperusha bendera kadhaa, ikiwemo moja ambayo ilikuwa ikionesha rais huyo amesimama juu ya tangi , kana kwamba ndiye kamanda wa dunia nzima.

Ilionyesha jinsi wafuasi wake wanavyomchukualia na jinsi rais Trump alivyojichukulia katika kipindi chake cha miaka minne.

Hatimaye alitoka katika klabu hiyo na kuanza safari yake kuelekea nyumbani.

Wakosoaji wake walikua wakimsubiri kwa maelfu .

'Utashindwa na tutashinda'

Msafara wa magari wa rais ulipitia Virginia, huku mie nikiwa ndani ya msafara huo katika gari moja ambalo karibia lilishiriki katika ajali katika eneo la Fairfax County Parkway.

Ving'ora vililia. Jinsi tulivyokuwa tukikaribia kufika Ikulu ndio jinsi idadi kubwa ya watu iliongezeka.

Watu walikuwa wakisherehekea kushindwa kwake. Mmoja ya watu alibeba maandishi yaliosema 'utashindwa na tutashinda'

Watu walipiga honi na kusherehekea.

Baadaye tulirudi katika Ikulu ya rais , rais aliingia na mlango taofuti , mlango ambao sio kawaida kwa marais kutumia. Mabega yake yalikuwa chini na uso wake ukiangalia chini.

Aliangaliia juu na kuniona mimi na wengine na kutuonyesha kidole gumba ikimaanisha kwamba mamabo yako sawa.

NI ishara ambayo haikuwa na nguvu kwa kweli , hakuinua mkono wake juu ama hata kuyumbisha ngumi yake kama anavyofanya mara kwa mara.

Akiwa katika Ikulu ya Whitehouse ama hata katika uwanja wa gofu, rais hajawahi kuyumba, aliendelea kudai wizi wa kura na kusisitiza kwamba ukweli utabainika.

Alituma ujumbe wa twitter mapema alfajiri akitangaza kwamba alishinda uchaguzi.

Lakini huyo alikuwa rais Trump katika twitter. Rais niliyemuona alikuwa na muonekano tofauti .

Wakati alipokuwa akielekea katika mlango huo mwendo wa jioni kutembea kwake kwa maringo kulikuwa kumepotea.