Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020: 'Nini hufanyika iwapo mgombea atakataa matokeo?'

Trump na Biden

Ni namna gani mgombea anaweza kugomea matokeo? na kwanini baadhi ya kura zina mchango kuliko nyingine?

Haya ni baadhi ya maswali muhimu kuhusu uchaguzi wa Marekani yakijibiwa.

Section divider

Trump anaweza kugomea matokeo ya uchaguzi? -Basel, Israel

Ndio, kampeni zote mbili zimesema zinaandaa kesi baada ya uchaguzi.

Upande wa Trump umekosoa zoezi la kuhesabu kura katika majimbo muhimu ya Nevada, Wisconsin, Georgia, Pennsylvania na Michigan.

Wana haki ya kudai kuhesabiwa tena kwa kura katika majimbo, hasa kama matokeo yamekuwa ya ushindani.

Kumekuwa na kura za posta mwaka huu, na pia inawezekana kuwa uhalali wa kura hizi ukapingwa mahakamani.

Kesi hizi za kisheria zinaweza kwenda hadi Mahakama Kuu ya Marekani - yenye mamlaka ya juu kisheria.

Hii ilitokea mnamo 2000, wakati Mahakama ya Juu iliposimamisha hesabu huko Florida na kutoa uamuzi kwa faida ya mgombea wa Republican George W Bush ambaye alikua rais.

Section divider

Kitatokea nini iwapo watapata kura sare - Chinga, China

Kuna kura 538 za uchaguzi za kunyakua, na idadi maalum ya wapiga kura wanaowakilisha kila jimbo kulingana na idadi ya watu.

Hii inamaanisha sare inawezekana kwa kura 269 kila mmoja, ingawa uwezekano si mkubwa.

Ikiwa hakuna mgombea atakayepata kura nyingi katika uchaguzi, itakuwa ni juu ya Bunge la Congress kuamua.

Itakuwa wabunge wa Congress waliochaguliwa katika uchaguzi wa mwaka 2020 ambao watachukua jukumu hili.

Baraza la Wawakilishi lingepiga kura kuamua rais, na kila ujumbe wa jimbo una kura moja - kura 26 lingehitajika kwa mgombea kuwa rais.

Seneti ingemchagua makamu wa rais, na maseneta wote 100 wakiwa na kura moja kila mmoja.

Section divider

Je! Kura ya kitaifa ina ushawishi gani kwa kura za wajumbe?- Caroline Bonwitt, Gloucestershire, Uingereza

Marais wa Marekani hawapatikani kwa kura ya wingi wa kura kwa ngazi ya taifa, isipokuwa kwa kunyakua kura za majimbo ya kutosha

Mshindi katika kila jimbo hupata kuungwa mkono na idadi ya wajumbe kulingana idadi ya watu katika jimbo husika.

Wajumbe hawa hukutana majuma machache kabla ya siku ya kupiga kura- wajumbe hupatikana ili kuchagua rais

Ili kushinda urais kura 270 za wajumbe zinahitajika.

Section divider

Karibu kila mtu ulimwenguni amechoshwa na 'ujinga huu wa kura ya wajumbe' . Kwa hivyo ni ngumu kiasi gani kufanya uchaguzi wa Marekani bila kura ya wajumbe? - Judy, BC, Canada

Mfumo wa uchaguzi wa Marekani uko kwa mujibu wa katiba, kwa hivyo kuibadilisha itahitaji marekebisho ya katiba.

Hii italazimika kupitishwa na theluthi mbili ya Seneti na Baraza la Wawakilishi, au idadi sawa ya mabunge ya majimbo. Hatua hii itahitaji kuidhinishwa na robo tatu ya majimbo ya Marekani.

Hatua hii ni vigumu kufanikiwa, ingawa kumekuwa na majaribio ya kubadilisha mfumo hapo zamani.

Kuna juhudi zinazoendelea za majimbo mengine kutoa kura zao za uchaguzi kwa mshindi wa kura nyingi, haijalishi ni nani atakayeshinda hapo.

Wajumbe hao ni kina nani, huchaguliwa kwa namna gani na hufanya kazi hii kwa muda gani? -Penny Reid Northumberland, Uingereza

Wajumbe hawa kwa kawaida huteuliwa na vyama vya Republican na Democratic katika kila uchaguzi.

Kuna sheria tofauti za kuwachagua katika kila jmbo, na rasmi huchaguliwa siku ya kupiga kura.

Wajumbe hawa huwa na mahusiano na vyama vya siasa nchini Marekani, kama vile wanaharakati au wanasiasa wa zamani.

Bill Clinton aliteuliwa kuwa mjumbe na Democratic mwaka 2016 na Mtoto mkubwa wa Donald Trump aliteuliwa na Republican.

Bill Clinton

Chanzo cha picha, Reuters

Nani ataamua kuhusu nani awe rais iwapo hakutakuwa na mshindi kupitia kura ya wajumbe? -Robert Pallone, Maryland

Ikiwa hakuna mshindi dhahiri katika kura za wajumbe , itamaanisha kuwa kumekuwa na kufungana katika matokeo ya jumla ilivyoelezwa hapo juu), au kwamba mapingamizi kisheria katika majimbo yenye mzozo hayajatatuliwa, na kwa hivyo wapiga kura wao hawawezi kuchaguliwa.

Ikiwa matokeo ya uchaguzi bado yana mzozo na majimbo fulani hayawezi kuamua ni mgombea gani wa kumpa wapiga kura wao, bunge la Congress litalazimika kuingialia kati.

Katiba ya Marekani imeweka tarehe ya mwisho ya- muda wa rais (na makamu wa rais) kuwa madarakani unamalizika tarehe 20 Januari saa sita mchana.

Ikiwa Congress haijaweza kuchagua mshindi wakati huo, kuna safu ya urithi iliyowekwa kisheria.

Kwanza kwenye safu hiyo ni Apika wa bunge la wawakilishi, kwa sasa Nancy Pelosi, akifuatiwa na mkuu wa Seneti kwa sasa ni Charles Grassley.

Hii haijawahi kutokea hapo awali kwa hivyo haijulikani jinsi, chini ya mazingira haya, itafanyaje kazi.

Section divider

Ni nini kinachofanya kura za majimbo mengine kuwa muhimu kuliko mengine? - S Robertson, Sussex, Uingereza

Wagombea huwa wanafanya kampeni katika majimbo ambayo matokeo hayana hakika - ndiyo sababu watu wanasema kura katika majimbo haya "zina umuhimu zaidi".

Maneo haya hufahamika kama yenye mchuano mkali

Mfumo wa uchaguzi wa Marekani unamaanisha kuwa katika majimbo yote isipokuwa mawili, kiwango cha ushindi hakijalishi, kwani yeyote atakayepata kura nyingi hushinda kura zote za uchaguzi katika jimbo hilo.

Presentational grey line