Milipuko ya Iran: Nani yuko nyuma ya ‘mashambulio’ hayo katika maeneo muhimu?

Mara baada ya saa sita Usiku tarehe 30 Juni, ujumbe wa barua pepe ulitumwa kwangu. Ulidai kuwa ulitoka kwa kikundi kisichojulikana kinachojiita Homeland Cheetahs.

Kikundi hicho kilisema kuwa kilikuwa kimeshambulia moja ya maeneo makuu ya nyuklia ya Iran katika eneo la Natanz saa chache kabla ya kutuma ujumbe huo , saa nane za mchana kwa saa za eneo hilo.

Ujumbe huo uliokuwa na maelezo marefu , ulidai kikundi hicho kimelipua eneo la mitambo ya nyukilia na kwamba utawala wa Iran hautaweza kuficha hilo.

Kikundi hicho kilisema kuwa kimeundwa na askari wapinzani ndani ya jeshi la Iran na vikosi vya usalama na kwamba wamekua wakipanga mashambulizi kadhaa ambayo hadi sasa serikali ya Iran imeyaficha kwa Umma.

Nilikwenda mtandaoni kuangalia taarifa za mashirika ya habari ya Iran na ushahidi wa kuaminika kwenye mitandao ya kijamii, lakini sikupata taarifa zozote kuhusu mashambulizi popote.

Saa chache baadae, Shirika la Iran la nguvu za Atomiki lilitangaza kwamba kulikua na tukio katika kiwanda cha nyukilia cha Natanz.

Kuandaa aina hii ya taarifa na video huchukua saa kadhaa, kama si siku, za mpango. Yeyote aliyeandika taarifa hii alifahamu fika kuhusu ulipuaji wa kiwanda cha Natanz mapema, jambo linalotoa ushahidi kwa dhana kwamba kitendo hicho kilikua ni njama iliyopangwa.

Lakini pia kuna uwezekano kwamba barua pepe hiyo ilikua na malengo ya makusudi ya kutupotosha juu ya ni nani hasa alikua nyuma yake, na huenda ilikua ni kazi ya mawakala wa kigeni waliokua wakijifanya kuwa ni wapinzani wa utawala wa Iran.

Shambulio 'lililozuiwa'

Jina la kikundi , the Homeland Cheetahs, ni sawa na lile la makundi mengine ya kimtandao ya "Iran" , kama Paka wa uajemi , au makundi ya paka wa furaha - ya wadukuzi wanaoaminiwa kuwa ni sehemu ya jeshi la mtandao la Iran linalofahamika kama - Iranian Revolutionary Guard Cyber Army.

Inawezekana kwamba Homeland Cheetahs walibuniwa ili kukabiliana na Paka wa uajemi ( Persian Cat).

Mwishoni mwa mwezi Mei, idara ya usalama wa mtandao ya Israel, na ile ya Iran - Iran arch-foe - zilisema kuwa nchi ilizuia shambulio kubwa la kimtandao katika mfumo wake wa maji, jambo lililodhaniwa kwa kiasi kikubwa kuwa ilikua ni kazi ya Iran.

Siku kadhaa baadae, kulikua na shambulio la kimtandao dhidi ya bandari na kituo muhimu cha uchumi Shahid Rajaae, kilichopo kusini mwa Iran.

Zaidi ya 50% ya bidhaa za Iran zinazoingizwa nchini na kuingizwa hupitia katika bandari hiyo. Shambulio lilisababisha kupasuka kwa kiasi kikubwa kwa mifereji ya maji inayoelekea kwenye eneo la kuondokea meli katika bandari hiyo.

Maafisa wa Iran walilaumu ukosefu wa umeme kuwa chanzo cha hali hiyo, lakini duru za kijasusi za magharibi ziliamini kuwa ulikua ni ulipizaji kisasi wa Israeli dhidi ya Iran.

Moto na milipuko

Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kumekua na ongezeko la idadi ya matukio ya ajabu ambayo yameharibu maeneo muhimu nchini Iran.

Matukio kadhaa ya moto yalitokea katika viwanda vya nyukilia, maeneo ya hifadhi za mafuta, viwanda vya umeme, viwanda vikuu kote nchini Iran.

Tangu tarehe 26 Juni pekee, kumekuwa na matukio kadhaa, kama vile:

26 Juni: Mlipuko katika kiwanda cha uzalishaji mafuta kinachotengeneza makombora ya ballistic eneo la Khojir, karibu na Parchin, karibu na Tehran;moto katika kiwanda cha umeme katika Shiraz, na kusababisha giza.

30 Juni: Mlipuko katika kliniki ya matibabu mjini Tehran, watu 19 walikufa

2 Julai: Mlipuko na moto katika kituo cha nyuklia cha Natanz

3 Julai: Moto mkubwa uliwaka katika Shiraz

4 Julai: Mlipuko na moto ulitokea katika kiwanda cha umeme cha Ahwaz; gesi ya chlorine ilivuja katika kiwanda cha kemikali cha Karoun cha Mahshahr.

Saeed Aganji, mwandishi wa habari wa Iran mwenye makao yake Finland ambaye amekua akifuatilia matukio nchini Iran, anasema matukio hayo sio ya kawaida na yanaweza kuwa ni ya makusudi.

" Kwa kuyalenga maeneo ya kimkakati na ya kiuchumi , lengo ni kuudhofisha kabisa uchumi wake na kuulazimisha utawala kuacha kudhamini kifedha makundi ya wanamgambo na kujibadili mambo katika Mashariki ya Kati."

Parchin na Khojir ni vituo viwili vya jeshi vinavyoaminiwa kuwa na viwanda vya nyukilia na makombora Mashariki mwa mji mkuu wa Iran Tehran.

Wakaguzi kutoka Shirika la kimataifa la kudhibiti nguvu za Atomiki (IAEA), kwa muda mrefu wamekua wakikataliwa kufikia kituo cha Parchin, ambako Iran inashukiwa kuwa ilifanya majaribio ya vilipuzi ambavyo vina uhusiano na silaha za nyukilia .

Onyo la Iran

Shirika la habari la taifa la Iran- Irna lilisema kuwa moto katika Natanz huenda ulisababishwa na njama " za mataifa hatari, hususan utawala wa Kizayuni [Israel] na Marekani".

Mkuu wa ulinzi wa raia nchini Iran aliapa ''kujibu'' iwapo itagundulika kuwa irani ilikua muhanga wa shambulio la kimtandao.

Jumapili, "afisa wa Mashariki ya Kati wa intelijensia "ambaye jina lake halikutajwa aliliambia gazeti la New York Times kuwa Israel ilisababisha mlipuko katika Natanz.

Siku moja kabla, waziri wa Israeli wa masuala ya kigeni alijibu kwa mafumbo alipoulizwa iwapo Israeli ilikua nyuma ya shambulio, akisema "matendo yetu ndani ya Iran ni bora yaachwe bila kusemwa".

Israel kwa kawaida huwa haiwajibiki na aina hizi za ''mashambulio'' na maafisa wa Iran wameepuka kuilaumu Israeli moja kwa moja. Lakini inaonekana vita vya kimtandao baina ya nchi mbili tayari vimeanza.