Kim Yo-jong: Mwanamke mwenye uwezo mkubwa anayeonekana kuwa mrithi wa Kim Jong-un Korea Kaskazini

Katika kipindi cha miaka iliopita, Kim Yo-jong ameonekana kama mtu muhimu katika uongozi wa Pyongyang.
Ni dadake mdogo kiongozi mkuu wa taifa hilo Kim Jong-un na dadake wa pekee anayeonekana kuwa karibu na uongozi na mwenye uwezo mkubwa.
Kim jong-un kwa mara ya kwanza alijipatia umaarufu wa kimataifa 2018, wakati alipokuwa ndugu wa kwanza wa familia ya Kim kuzuru Korea Kusini.
Alikuwa miongoni mwa wajumbe waliohudhuria mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi yaliokuwa yakifanyika mjini Seoul ambapo Korea Kuisni na Korea kaskazini zilishindana kama timu moja.
Hatua hiyo ya mwaka 2018 ambapo alifanyakazi ya kidiplomasia pamoja na nduguye ilimfanya akutanea na kiongozi wa Korea Kusini Moon Jae - in, Xi Jingpin wa China na rais wa Marekani Donald Trump.
Uhusiano wa karibu na nduguye na majukumu yake makubwa katika ngazi za kisiasa yamemfanya kuangaziwa tena mwezi Aprili 2020 katika kipindi ambapo Kim Jong un alitoweka katika hafla za umma

Chanzo cha picha, Reuters
Wakati bwana Kim alipotoweka mwezi Aprili , maswali kuhusu afya yake yalizuka , na alionekana miongoni mwa watu wenye uwezo wa kumrithi.
Jukumu la bi Kim lilipigwa jeki mwezi Oktoba 2017 wakati alipopandishwa cheo hadi katika kamati kuu ya kisiasa ya chama tawala .
Kabla ya hilo alikuwa na ushawishi kama naibu mkurugenzi wa idara ya propaganda- jukumu ambalo anaendelea kulibeba - na mara nyingi anafanyia kazi muonekano wa nduguye kwa umma nchini humo.
Bi Kim pia amewekwa katika orodha ya watu waliowekewa vikwazo kufuatia madai kwamba anahusika na unyanyasaji wa kibinadamu nchini Korea Kaskazini.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hiyo inamaanisha kwamba raia wa Marekani hawaruhusiwi kufanya biashara yoyote naye. Mali yake yoyote iliopo nchini Marekani itapigwa tanji.
Je ana uwezo kiasi gani?
Ni vigumu kuelewa uwezo wake nchini Korea Kaskazini hivyobasi ni vigumu kubaini mtandao wake wa kisiasa .
Anadaiwa kuolewa na mwana wa Choe Ryong-hae, katibu wa chama tawala mwenye uwezo mkubwa na mtu wa pili kwa uwezo baada ya rais Kim jong-un .
Iwapo ni kweli hilo linampatia hadhi ya juu. Oliver Hotham , wa chombo cha habari cha NK , aliambia BBC kwamba huenda ana umri wa miaka thelathini na… na ushawishi wake mkubwa unatokana na hadhi ya nduguye.
Hivi karibuni, taifa hilo lilihusika kutuma ujumbe wa maneno makali dhidi ya Korea Kusini na kuonekana kama ni namna mpya ya Korea Kaskazini kuingilia masuala ya Korea Kusini, kwa mujibu wa taarifa za NK News.
Mwezi Juni, Kim Yo-jong alitishia kutuma kikosi cha wanajeshi katika ukanda wa mpakani , ikiwa ni sehemu ya kile ambacho Pyongyang ilisema walishindwa kuzuia wanaharakati wanaopinga utawala wake kutuma vijibarua vinavyopinga uongozi wake.
Mwanamke huyo alitoa angalizo pia kuwa ofisi zote ambazo zina uhusiano kati ya nchi hizo mbili na ziko eneo la mpakani katika mji wa Kaesong ambako Korea Kaskazini ilijitoa tangu Machi 2019, zitaondolewa.".
Siku chache baadae, Juni 16, mlipuko mkubwa ulisikika huko Kaesong na moshi ulionekana ukifuka katika eneo hilo.
Maofisa wa Seoul walithibitisha kuwa ofisi ambayo serikali ya Korea Kusini ilitoa karibu dola milioni 8 (£6.3m) ili kufanyiwa ukarabati ndio ilikuwa imelipuliwa.
Nini ambacho kipo nyuma ya familia ya Kim?
Je kuna uhitaji wa kuwa na mrithi wa Kim Jong-un, ili mahusiano katika familia yabaki kuwa mazuri.
Siasa za nchini humo kwa miongo kadhaa wamekuwa wakiogopa ukoo ambao unafahamika kama Paektu kurejea katika utawala wa mwasisi r Kim Il-sung. Kim Jong-un anaaminika kuwa na watoto lakini watoto hao ni wadogo.

Chanzo cha picha, KCNA
Ilhali bi. Kim ni miongoni mwa wanafamilia hiyo, hivyo Chombo cha habari cha taifa kinabidi kipate namna ya rahisi ya kutoa madaraka katika mikono yake.
Lakini kama ni familia hiyo ina maanisha kuwa alikuwa hajachaguliwa, na kiongozi mpya anaweza kumuona kama mpinzani wake ambaye ni hatari kwake.
"Labda kama mwanafamilia mwingine wa Kim atachukua majukumu hayo, basi kwake mambo yatakuwa ni rahisi sana," alisema Fyodor Tertitskiy kutoka chuo kikuu cha of Kookmin Korea Kusini.
"Au kukubali kuchukua uongozi huo wa juu au kupoteza madaraka yote na kuharibu maisha yake pia."
Je ni wadhfa gani unaomfaa katika familia hiyo ilio madarakani?
Kim Yo-jong ni binti mdogo wa hayati Kim Jong-il. Ni ndugu wa mama na baba wa Kim Jong-un na Kim Jong-chol, kaka yake ambaye hakuwahi kudhaniwa kuwa ni kiongozi wa juu katika mfumo wa uongozi wa kisiasa.
Alizaliwa mwaka 1987 , ni mdogo kwa miaka minne wa kaka yake Kim Jong-un. Ndugu hao wawili walisoma na kuishi pamoja huko Berne, Switzerland.
Maofisa wa Shule nchini Switzerland wamesema alilindwa zaidi na kitengo cha walinzi na walezi. Wakati mwingine aliripotiwa kuwa na homa kali na alitolewa shuleni na kupelekwa hospitalini.
Ripoti zinasema kuwa alikuwa na malezi ya kulelewa, na watu wengi wa familia ya Kim hawakuingiliana naye sana
Anafanya nini?
Kutoka mwaka 2014, kazi yake kubwa ilikuwa ni kuilinda taswira ya kaka yake, alikuwa na jukumu muhimu kwenye chama hususan kwenye idara ya propaganda.
Mnamo mwaka 2017 alipandishwa hadhi , hii ikaonekana kuwa amepata nafasi kubwa ijapokuwa majukumu yake ya propaganda yalibakia palepale.
Alidaiwa kusimamia matukio yote ya kaka yake yaliokuwa yakihusu kuonana na jamii pamoja na kuwa mshauri wa kisiasa.
Wakati wa mkutano mkuu wa Hanoi 2019 uliposhindwa kufikia makubaliano na Marekani, ilidhaniwa kuwa huenda angeshushwa katika wadhifa wa juu wa kisiasa, lakini mwanzoni mwa mwaka 2020 akarejea.

Kabla ya mwaka 2014 mwanamke huyo alikuwa akionekana mara chache sana kwenye vyombo vya habari, mwaka 2011 alionekana kwenye msiba wa Baba yake pamoja na kwenye uchaguzi wa kaka yake mwaka 2014.
Bi Kim ameonekana mara chache sana akiwa kwenye picha za Ikulu
IJapokuwa inadhaniwa kuwa aliichukua nafasi kuu ya uongozi tangu mwaka 2008 wakati wa mipango ya mrithi wa Kim Jong-ill wakati afya yake ilipokuwa ikidhoofika.
Jukumu lake kama mrithi wa kaka yake limekuwa likizungumzwa kila wakati kunapokuwa na wasi wasi wa kiafya wa Kim Jong-un.
Kama tu mnamo Aprili 2020, kulikuwa na uvumi kama ule wa mwaka 2014 wakati Kim Jong-un alikuwa amepotea kabisa machoni mwa umma ila akajitokeza tena katika hali nzuri ya afya akisaidiwa na fimbo ya kutembea.












