Je, Zimbabwe inaporomoka kwa mara nyengine baada ya mapinduzi?

Chanzo cha picha, AFP
Wanawake watatu mjini Harare, Zimbabwe walikuwa wanabubujikwa na machozi huku wakitetemeka kama wanataka kuzimia kwa njaa.
Walikuwa wamevalia sare za magereza, wakiwa wamekaa katika mazingira mabaya wakisubiri kusikilizwa kwa kesi zao mahakamani iwapo watapata dhamana.
Katika nchi inayogombana sio tu na homa kali ya mapafu lakini pia vita vya kiuchumi na kisiasa - pamoja na uvumi na madai ya njama ya mapinduzi - kesi ya kushangaza na yenye utata ya wanaharakati wa upinzani, Cecilia Chimbiri, Netsai Marova na Joana Mamombe wanaonekana kuelekeza mambo mabaya na ya msingi juu ya mapambano ya sasa ya Zimbabwe: umma umeshapoteza imani yake katika taasisi muhimu.
"Tunaona hali tete ya taifa ambalo lipo kwenye vita na raia wake," Fadzayi Mahere, msemaji wa chama cha upinzani cha Democratic Change (MDC), ambaye alihudhuria kusikilizwa kwa kesi Jumatatu na kusema kwamba udhalilishaji wa wanawake ni sehemu ya mkakati wa kisiasa wa kuhamasisha hofu katika umma.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanasiasa wa MDC wanakabiliwa na mashtaka ambayo walisema uwongo kuhusu kutekwa nyara na unyanyasaji wa kijinsia mwezi uliopita.
Wakizungumza kutoka hospitalini kuhusu shida zao, wanawake hao walisema maafisa wa usalama wa serikali ambao majina yao hayakutajwa wamewatesa.
Lakini mawaziri wa serikali waliwashutumu mara moja kwa madai ya kubuni hadithi zao ili kudhalilisha serikali na kujiondoa kutoka kwa ushiriki wa wanawake wenyewe katika maandamano haramu.
"Wanawake hao watatu walikuwa sehemu ya kikundi cha vijana cha MDC ambayo walikataa sheria za kufunga na kuhusika katika maandamano haramu," katibu wa habari wa serikali Nick Mangwana alisema.
'Kesi inayotisha na kali kisheria'
Naibu waziri mmoja, ambaye baadaye alifukuzwa, alidai kuwa wanawake hao, ambao mmoja wao ni mbunge, walikuwa makahaba.
Hawana wasiwasi wowote juu ya kukiuka wanawake na hakuna shauku ya kuwaadabisha wahusika," alisema Bi Mahere.
Lakini wengine huko Harare wameachwa wakachanganyikiwa, na wakosoaji, juu ya madai hayo, hawawezi kuamua ni nani wa kumuamini.
"Tumekuwa tukidanganywa hapo awali. Hakuna kitu kama inavyoonekana," alisema daktari mmoja wa hospitali, ambaye mara nyingi anawashughulikia waathiriwa wa kuteswa, lakini aliomba asitambulike.

Chanzo cha picha, EPA
Hakuna mapinduzi yoyote katika maandamano hayo, "alisema Waziri wa Mambo ya Ndani, Kazembe Kazembe wiki iliyopita, ambaye akilaumu" uvumi "huo kama dhana kati ya vikosi vya ndani na vya kimataifa.
Maoni yake, yaliolenga kusisitiza, yalionekana kuwa na athari tofauti.
Tunakabiliwa na dhoruba. Dhoruba kali. Serikali inaenda kufeli," alionya mfanyabiashara Shingi Munyeza, wakati wa mkutano wa programu ya zoom na wanaharakati wa mashirika ya kiraia walishtuka juu ya mzozo mkubwa wa uchumi na tishio lililosababishwa na homa kali ya mapafu.
Je! Mapinduzi mengine yanawezekana? hali ya kutatanisha mjini Harare imeongezewa na hatua ya hivi karibuni ya vikosi vya usalama kuteka makao makuu ya upinzani mbali na kuwepo kwa wanajeshi barabarani wakishinikiza amri ya kutotoka nje.
Mmoja wa washirika wa zamani wa Bw Mugabe, ambaye sasa yupo mafichoni nchini Afrika Kusini (na anayetuhumiwa kuchochea uvumi juu ya mapinduzi mengine ya kijeshi ), alisema waziwazi kwamba hali .
"Tuko katika hali mbaya. Mfumo wowote ambao umejengwa kwa misingi dhaifu lazima utayumba.Utawala huu ulijengwa juu ya mapinduzi," alisema waziri wa zamani Saviour Kasukuwere, akikishutumu chama chake cha zamani cha Zanu-PF, kwa kushindwa kutimiza ahadi zake.
'Walilazimishwa kunywa mkojo'
Kwa sasa, Cecilia Chimbiri, Netsai Marova na Joana Mamombe wamerudi jela katika gereza maarufu linalojulikana kama Chikurubi lililopo Harare, wakiwa wanasubiri hukumu yao.
Hakimu amekataa kuwapa dhamana wanawake hao, kwa madai kuwa kuna ushaidi ambao upo dhidi yao ukiwemo wa picha za video na kama wakiachiwa wanaweza kutoroka nje ya nchi.
Wiki iliyopita , akizungumza kwenye simu kutoka hospitali, bi Chimbiri alisema amekuwa akinyanyaswa kingono na kulazimishwa kunywa mkojo na watu ambao hawafahamu na kusisitiza kuwa yeye na wenzake walikuwa na hofu.
"Uhuru wetu hatutaupata kiurahisi," alisema bi.Chimbiri.
Kukataa mlo wa gerezani
Chama cha MDC kilisema kwamba uamuzi wa kuwanyima wanawake hao dhamana una mrengo wa kisiasa na hoja ya kukata rufaa ilikuwa inaandaliwa.
Siku ya Jumanne, wakati wa maombi ya kitaifa rais Mnangagwa aliwataka Wazimbabwe kutubu ili kukabiliana na mlipuko huu wa corona, kupambana na rushwa na watu kutotendewa haki.
"Tusamehe kwa matendo yetu yasiyo na haki au rushwa ambayo imewafanya masikini wahangaike na watu wasio na hatia kufariki.
"Tusamehe kila mmoja wetu na kama taifa kwa ujumla na hata tukifanya dhambi ambazo hatukuzitarajia," alisema.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Wakati huohuo, Amnesty International imelaani kile ambacho imekiita kuwa uminywaji wa uhuru wa kujieleza na uhalifu wa wapinzani wan chi.
Baada ya kufika mahakamani, wanawake hao watatu ambao mmoja alikuwa anatembea kwa shida - walisindikizwa kurudi gerezani.
Wakidai kuwa na hofu kuwa wanaweza kuwekewa sumu ndio maana wamekataa kula chakula cha magereza na wanategemea chakula ambacho mamlaka inaweza kuwaruhusu ndugu zao au wafuasi wao kuwaletea.












