Aliyemfuatilia mpenzi wake wa zamani mtandaoni ahukumiwa

Woman holding a phone

Chanzo cha picha, Getty Images

"Nilimuamba aniache, Nikamuomba aendelee na maisha yake na aniache na maisha yangu, lakini haikusaidia lolote ."

Kwa karibu miezi 12, Michael Cook, mwenye umri wa miaka 31, alimfuatilia kisiri kwenye mitandao mpenzi wake wa zamani baada ya uhusiano wao kuisha.

Kila siku alikua anawasiliana nae-huku akitishia kujiua au wakati mwingine akimuomba msamaha-licha ya kwamba mpenzi wake alikua amemuamba aachane nae kabisa.

"Alipokea kwa ujumla barua jumbe zaidi ya 4,000 , alipigiwa simu 300 na mamia ya jumbe za simu pekee kutoka kwake.

"Kusema kwamba jumbe hazikua zenye madhara, lakini haimaaninishi kwamba hazikuwa na athari za kisaikolojia kwangu.

"Nililazimika kubadilisja mfumo wangu wote wa maisha ili kuhakikisha mimi na watoto wangu tunakua salama kutokana na hali hiii. Ninalazimika kuendelea kuishi hivyo , na kusema ukweli maisha yangu hayatakuwa sawa na yalivyokua zamani tena ." alisema muathiriwa.

Jumatau Bwana Cook, kutoka eneo la Litherland mjini Liverpool Uingereza, alihukumiwa kifungo cha wiki 12 gerezani baada ya kukiri kuwa amekua akimfuatilia kwenye mitandao aliyekua mke wake na kuwasiliana pamoja na kumtumia jumbe mpenzi wake wa zamani.

Pia alipewa kibali cha mahakama cha miaka mitano kinachomzuwia kuwasiliana na mpenzi wake wa zamani.

Unaweza pia kusoma:

'Vitisho vya mara kwa mara vya kujiua '

Muathiriwa huyo alitoa ripoti kwa polisi akielezea maisha aliyoyapitia baada ya kuachana na aliyekua mpenzi wake.

" Nilikuwa ninatumiwa jumbe za vitisho vya kujiua mara kwa mara, madai ya kila mara dhidi yangu ya mambo mabaya ,kila wakati alikua akiniwinda na kunituhumu , kila siku, mara nyingi kwa siku.

" Alikua akitumia njia mbali mbali kunifikia, iwe kwa njia ya mitandao ya kijamii, simu, barua pepe, na njia nyingine nyingi ambako aliweza kunipata -mkiwemo PayPal.

"Hii haikukomea hapo, pia alituma jumbe kwa watu wa familia yangu, wapenzi wao na marafiki hata wafanyakazi wenzangu kazini."

Kutokana kuhisi na uoga na kama mtu asiye na usaidizi, muathiriwa aliwasiliana na kituo cha polisi cha - Merseyside Police ambao walianzisha uchunguzi.

Licha ya polisi kuingilia kati, Cook aliendelea kumgtumia jumbe muathiriwa.

"Mienendo yake aliiona kama kitu kinachofaa kama anavyosema 'ananipenda ' na alifikiria kana kwamba nasamehe mienendo yake na kuona kama ni kitu cha kawaida kuwasiliana nami kila mara.

"Tabia hii haifai na mapenzi hayasababishi uwe na madhara ya kihisia na kuathiri afya yako ya mwili ."

Muathiriwa anasema sasa anafahamu kuwa mpenzi wake wa zamani alionyesha habioa sawa na hizo kabla na anataka kuwashauri wanawake kutumia sheria zilizopo zinazowalinda wanawake dhidi ya wa wapenzi wao.

George Appleton and Clare Wood

Chanzo cha picha, Manchester Police handouts

Maelezo ya picha, Clare Wood aliuliwa na na aliyekua mpenzi wake George Appleton, ambaye alikua na historia ya unyanyasaji dhidi ya wanawake

" Ninatoa taarifa hii nikiwa na matumaini kuwa mwanamke yeyote au mwanaume ambaye aliwahi kupitia maisha sawa na yangu kutoka kutokana na mienendo ya mpenzi wake, abaini kuwa hii si sahihi.

" Kama muathiriwa ninafahamu jinsi ilivyorahisi kujilaumu mwenyewe, lakini tafadhari usijilaumu, nenda utafute usaidizi . Usikate tamaa."

Shirika linalowalinda watu dhidi ya mashambulizi ya kimtandao -Stalking charity Protection Against Stalking linasema visa kama hivi ni vya kawaida.

Linasema kuwa limeshuhudia idai kubwa ya visa vya aina hiyo vikiongezeka mara dufu tangu ilipowekwa amri ya kutotoka nje.

"Kufungiwa ndani haimaanishi kuwa unafungiwa na mtu anayekufuatilia bila kufahamu kwenye mitandao na kukukosesha amani ," anasema mshauri nasaha Jan Berry.

" Katika kipindi cha wiki zilizopita tabia ya kufuatilia watu na kuwatumia jumbe zisizofaa imeshamiri na tumefanikiwa kuasaidia wateja kupata agizo la mahakama linalowalinda.

"Ni muhimu kwamba watu watambue tabia ya kufuatiliwa fuatiliwa bila idhini yako ni vibaya na waombe msaada ili wawe salama."

Mkuu wa upelelezi Chief Insp Siobhan Gainer, kutoka kituo cha polisi cha Merseyside nchini Uingereza amesema kuwa kesi dhidi ya Cook inaonyesha wazi jinsi kufuatiliwa kisiri kwenye mitandao kunasababisha mahangaiko na matatizo ya kisaikolojia kwa waathiriwa.

"Tunafahamu kuwa katika kipindi hiki cha amri ya kukaa nyumbani waathiriwa wa visa hivi wanahisi kuwa wasiokuwa na usaidizi zaidi kutokana na kwamba hawawezi kutembea na wakati huo huo ufuatiliwaji wa maisha yao ukiendelea.

" Tunataka kuwahakikishia kuwa tutaendelea kuwasaidia wakati wa kipindi hiki kigumu."

Yeyote anayehisi maisha yake yanafuatiliwa ni dharura kuwasiliana na polisi.