Wazazi wampata mtoto wao aliyeibiwa miaka 32 iliyopita China

The reunification

Chanzo cha picha, CCTV

Maelezo ya picha, Wakati Li Jingzhi alipomuona mtoto wake wa kiume kwa mara ya kwanza baada ya kutengana kwa miaka 32

Familia moja nchini China ambayo aliibiwa mtoto wao wa kiume katika hoteli mwaka 1988 imempata baada ya miaka 32.

Mao Yin aliibiwa akiwa na miaka miwili, wakati baba yake alipoenda kumnunulia maji wakielekea nyumbani kutoka shule ya chekechea.

Wazazi wake walimtafuta nchini humo kwa muda mrefu huku mama yake akisambaza vijikaratasi zaidi ya 100,000 vilivyokuwa na maelezo kumhusu bila mafanikio.

Familia hiyo ilikutanishwa na polisi katika kikao cha wanahabari siku ya Jumatatu, na mwana wao -ambaye sasa ana umri wa miaka 34 - amesema anapanga kutumia muda wake mwingi kuwa karibu na wazazi wake.

"Nachukua fursa hii kuwashukuru maelfu ya watu waliotusaidia," alisema mama yake kijana huyo,Li Jingzhi.

Nini kilimkuta Mao Yin?

Alizaliwa Februari 23, 1986. Katika mahojiano na gazette la China la Morning Post mwezi Januari - kabla apatikane - mama yake alimuelezea kuwa mtoto "mzuri,mwerevu sana, na mwenye afya".

Mnamo Oktoba 17 mwaka 1988, baba yake, Mao Zhenjing, alikuwa akimpeleka nyumbani kutoka shule ya chekechea katika jiji la Xian mkoani Shaanxi.

Mtoto aliomba maji ya kunywa, kwa hivyo wakasimama katika lango la hoteli. Wakati baba alipokuwa akimpozea maji ya moto, aliangalia kando kidogo na hapo ndipo mtoto alichukuli.

Familia hiyo ilimtafuta mwana wao ndani na nje ya Xian, kwa kutumia vijikaratasi vya matangazo walivyobandik akila sehemu. Wakati mmoja walidhani wamempata lakini ilikuwa taarifa za uwongo.

The reunited family

Chanzo cha picha, CCTV

Maelezo ya picha, Familia baada ya kuungana tena

Bi Li aliacha kazi ili kumtafuta mwanawe -ambapo alisambaza vijikaratasi vya matangazo takriban 100,000 katika zaisi ya mike 10 - bila mafanikio.

Kwa miaka kadhaa aliangaziwa katika vipindi tofauti vya televisheni China akiomba msaada wa kutafutiwa mwanawe, ikiwemo kipinda cha X Factor.

Alifuatilia maelezo zaidi ya 300 ambayo yangelimsaidia ilisema SCMP lakini hiyo pia haikumsaidia katika juhudi zake.

Mwaka 2007, Bi Li alianza kazi ya kujitolea katika kundi llililofahamika kama "Baby Come Back Home", ili kuwasaidia wazazi wengine kuwatafuta watoto wao waliopotea.

Kwa mujibu wa shirika la habari la kitaifa ,alisaidia watoto 29 kuunganishwa na familia zao, wakati yeye binafsi hakujua mtoto wake aliko. Lengo lake ni kuendelea kufanya kazi na kikundi hicho.

Mao Yin alipatikana vipi?

Mwezi Aprili, shirika la habari la kitaifa lilitangaza kuwa, polisi wamepata kidokezo kuwa mwanamume mmoja mkoani Sichuan kusini magharibi mwa China - karibu kilomita 1,000 kutoka Xian -aliwahi kusaili mtoto miaka kadhaa iliyopita.

Polisi walimpata aliyesaili mtoto akiwa na miaka 34-, na uchunguzi wa chembe chembe za vinasaba DNA, ulipofanywa ulibaini kuwa Mao Zhenjing na Li Jingzhi wana uhusiano.

Mao Yin - ambaye alikuwa amepewa jana la Gu Ningning - sasa anaendesha biashara ya kupamba nyumba. Alisema hana "uhakika" kuhusu maisha yake ya siku zijazo, lakini atakuwa na muda na wazazi wake.

Polisi walisema wameambia wakuwa mtoto huyo aliuziwa wananandoa walili ambao hawakuwa na mtoto kwa yuan 6,000 sawa na (£690, $840 pesa za leo).

Bi Li walifahamishwa habari hizo njema Mei 10- Siku ya kinamama China. "Hii ni zawadi nzuri zaidi nimewahi kupata," alisema.

Tuchunguzi wa kutoweka kw amtoto mwaka 1988 bado unaendelea.

Ulanguzi wa watoto China ni mkubwa kiasi gani?

Suala la watoto kutekwa nyara au kuibiwa limekuwa tatizo kubwa China kwa miongo kadhaa.

Hakuna takwimu rasmi, lakini kulingana na tuvuti ya Baby Come Back Home kuna jumble ya taarifa 14,893 zilizochapishwa kuhkuhusu wavulana waliotoweka, na wasichana 7,411.

Mwaka 2015, ilikadiriwa kuwa watoto 20,000 walikuwa wakitekwa kila kila mwaka nchini China.

Mwaka 2009, Wizara ya usalama wa kitaifa China ilikusanya data ya DNA ambayo kuanzia wakati huo imesaidia kupatikana kwa watoto 6,000 waliopotea..

Na kufikia Mei 2016, wizard hiyo ilizindua mfumo unaojulikana kama "Reunion", ambao kufikia Juni 201.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Kwa nini msichana huyu kutoka Nigeria ni nyota wa teknolojia ya siku zijazo