Virusi vya corona: Apata maambukizi akiwa gerezani

Televesheni ya Iran ilipeperusha mahojiano yake ba Sahar Tabar baada ya kukamatwa mwaka jana

Chanzo cha picha, IRTV

Maelezo ya picha, Televesheni ya Iran ilipeperusha mahojiano yake ba Sahar Tabar baada ya kukamatwa mwaka jana

Nyota wa Iran amepata virusi vya corona akiwa gerezani, kulingana na wakili wake.

Fatemeh Khishvand, mashuhuri kwa jina la Sahar Tabar katika mtandao wa Instagram, baada ya kutuma picha zake mtandaoni ambazo zimeelezwa na wengi kama 'zombie' wa Angelina Jolie.

Bi Khishvand alikamatwa mwishoni mwa 2019 kwa makosa ya uhalifu ikiwemo kukufuru na kuchochea ghasia.

Lakini mkuu wa gereza ambapo anazuiliwa amekanusha madai ya kwamba ameambukizwa virusi hivyo.

"Kuna taarifa zilizotolewa na wakili Fatemeh Khishvand ambazo si za kweli na ninazikanusha," Mehdi Mohammadi, mkuu wa gereza la wanawake la Shahr-e Rey, ameliambia shirika la habari la ISNA la Iran.

Iran imekuwa na idadi kubwa ya vifo kwasababu ya virusi vya corona Mashariki ya Kati, huku idadi mpya zilizotangazwa na msemaji wa wizara ya afya Jumamosi, ikifia zaidi ya 5,000.

Coronavirus

Hatahivyo, kuna wasiwasi kwamba idadi halisi ya waliokufa ikawa juu zaidi ya hiyo.

Wakili wa Bi Khishvand, Payam Derafshan aliandika barua ya wazi kwa mahakama ya Iran, ambayo aliituma kwenye akaunti yake ya Instagram.

Alisema amearifiwa na mama yake Khishvand kuwa mteja wake amehamishwa hadi eneo la karantini ndani ya gereza baada ya kuonesha dalili za virusi vya corona.

Aliongeza kwa Bi. Khishvand - ambaye alikuwa na umri mdogo wakati anashtumiwa hatafanikiwa kutoka na kufuatilia kesi yake akiwa nje kwasababu bado inaendelea.

Machi, Iran iliwaachiliwa huru wafungwa 85,000 akiwemo mhudumu wa shirika la kutoa msaada raia wa Uingereza mzaliwa wa Iran - kama sehemu moja ya kukabiliana na virusi hivyo.

Ukurasa wa Instagram wa Bi Khishvand ulifutwa

Chanzo cha picha, Instagram

Maelezo ya picha, Ukurasa wa Instagram wa Bi Khishvand ulifutwa

Bi Khishvand aligonga vichwa vya habari kimataifa 2017 wakati ambapo picha yake iliyobadlishwa kwenye mtandao wa Instagram iliposambaa mtandaoni. Tangu wakati huo, akaunti yake imefutwa.

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii walionyesha wasiwasi wakati kukiwa na taarifa kwamba amefanyiwa upasuaji wa urembo karibia mara hamsini, alisema kupitia Shirika la habari la Urusi la Sputnik News kuwa picha zake zilibadilishwa kwa kutumia program maarufu.

Anajiunga na orodha ndefu ya watu wenye ushawishi Iran ambao wameshtakiwa.

2018, kijana mmoja alikamatwa kwa kutuma video mtandaoni zinazomuonesha akicheza. Mwaka huohuo, afisa katika mji wa Mashhas alikamatwa baada ya kuchipuka kwa video inayoonesha kundi la wanawake na waume wanacheza katika ukumbi fulani.