Watu 40 wafa maji katika mafuriko DRC

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesababisha mafuriko yaliyowaua makumi ya watu mjini wa Uvira.
Kwa mujibu mamlaka katika eneo hilo,idadi ya vifo imepanda kutoka watu 15 hadi 40 siku ya Jumamosi.
Nyumba 5,500 zimesombwa na maji ya mafuriko hayo yaliyowaathiri watu 77,790.
Kuna hofu idadi hiyo huenda ikaongezeka kwasababu watu wengine mpaka sasa hawajulikani waliko.
Mvua inayonyesha ikiandamana upepo mkali imesababisha mito kufurika na kuleta maafa sio tu katika mji wa Uvira lakini pia sehemu zingine za DRC.

Serekali imeanza pia imewapatia hifadhi walioathiriwa huku shughuli ya kuwatafuta manusura zikiendelea.
Hii si mara ya kwanza mvua kusababisha maafa katika mji huo wa Uvira.

Mwaka jana pia nyumba nyingi zilianguka baada ya kusombwa na maji ya mafuriko ambapo watu 22 walifariki katika maeneo ya Kiliba,Kawizi na Kasenga.













