Virusi vya corona: Je kuvua nguo zote unapoingia nyumbani na kusafisha vyakula ulivyonunua kunasaidia kukabiliana na virusi hivi?

lechuga

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Unapofungua maji kwa namna hii: ndio njia salama ya kuosha matunda na mbogamboga wakati huu wa virusi vya corona.

Kuna kitu moja tu ambacho hakijapigwa marufuku hata katika nchi zenye masharti magumu katika kukabiliana na virusi vya corona: kununua chakula.

Iwapo utakwenda kununua vyakula sokoni na kuzingatia umbali uliopendekezwa baina ya mtu mmoja hadi mwingine wa mita mbili.

Na kisha tuchukulie kwamba katika kipindi chote hicho usishike uso wako, wala kusiwe na hata mtu mmoja ambaye atapiga chafya karibu yako au kukohoa.

Ukifika nyumbani, ukaacha kila kitu ulichobeba mlangoni nje na moja kwa moja ukaenda kuosha mikono na sabuni kwa kutumia maji kwa angalau sekunde 20 kama inavyopendekezwa na wataalamu wa afya.

Lakini baada ya hapo, ukashika tena kila kitu ulichokuja nacho na kuelekea jikoni na kuanza kuvitoa kimoja baada ya kingine ili kuviweka sehemu stahiki.

Je bidhaa hizo, vyakula na nguo zenyewe ulizovaa vina uwezo wa kusambaza virusi vya corona?

Taarifa nyingi katika mitandao ya kijamii zinapendekeza kwamba kila kitu kioshwe kwa kutumia sabuni hata matunda pamoja na kutoa viatu ulivyokuwa umevaa na nguo ulizokuwa nazo kuziweka moja kwa moja kwenye mashine ya kuosha nguo.

Mwanahabari wa BBC Mundo anaelezea kile ambacho ni kweli kuhusiana na hili.

Unaweza kufuatilia kwenye ramani ifuatayo kufahamu zaidi kuhusu hali ya maambukizi na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo duniani

Ijapokuwa haijathibitishwa haiwezi kupuuzwa

Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), kuna uwezekano wa kupata covid-19 kwa kuvuta chembe kidogo tu kutoka kwa aliyeathirika wakati anapokohoa au kupiga chafya.

Na pia chembechembe hizo zinaweza kufika kwenye vitu vilivyokaribu. Kwahiyo, WHO inasema kwamba watu wanaweza kupata virusi hivi kwa kushika sehemu zilizoathirika kisha wakashika nyuso zao kwa mikono hadi machoni, kwenye pua na mdomoni.

Hivyobasi, kulingana na maafisa wa afya Marekani na Umoja wa Ulaya, hakuna ushahidi wowote kwamba chakula au chochote kile kilichofungashwa kinaweza kuwa chanzo cha usambazaji wa virusi vipya vya corona.

Marga Hugas, Mwanasayansi mkuu katika Mamlaka ya Usalama wa Vyakula Ulaya mapema Machi alisema hakuna ushahidi wowote katika milipuko ya virusi vya nyuma sawia na vya corona kwamba vyakula vinaweza kuwa kisababishi cha maambukizi.

Hata hivyo, Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa Marekani (CDC) katika mtandao wao Machi 28, kilisema kwamba "Inawezekana mtu akapata virusi vya covid-19 kwa kushika sehemu iliyopata virusi au kitu chenye virusi kisha akashika mdomo wake, pua au pengine macho ingawa hakiamini kwamba hii inaweza kuwa njia kuu ya kusambaza virusi vya corona."

Persona lavándose las manos.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuosha mikono kwa kutumia sabuni kwa angalau sekunde 20 ni muhimu wakati wa kufanya manunuzi na hilo linaweza kurejelelewa baada ya kuweka bidhaa zote kwenye sehemu stahiki nyumbani

Ufungashaji wa chakula

Kwa mujibu wa shirika la Bloomfield, inategemea jinsi chakula kilivyofungashwa kabla ya kununuliwa.

Personas cargan bolsas de papel

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuosha mikono yako unapofika nyumbani baada ya kufanya manunuzi kunapunguza hatari ya maambukizi, kulingana na wataalamu.

Kulingana na utafiti uliochapishwa katikati ya Machi kwenye Jarida jipya la Utabibu Uingereza, Kirusi cha covid-19, kinaweza kuwa hai na kusambaa kwa hadi saa 24 kwenye makaratasi ya maboksi na hadi siku tatu katika mifuko ya plastiki au chuma kisichoingia kutu.

Vyakula

Vipi kwa vyakula ambavyo havijafungashwa kama vile matunda na mboga?

"Bidha ambazo ndio zimetoka shambani na hazijafungashwa ambazo huenda zimeshikwa na mtu mwengine kabla ya kukufikia, zioshe vizuri kwanza kwa maji yanayotiririka na uziache zikauke kwanza," limesema shirika la Bloomfield.

Baadhi wanaweza kufikiria kwamba kutumia sabuni ni hatua muhimu zaidi kiafya kwa matunda na mboga wakati huu wa virusi vya corona, lakini huo sio ukweli.

"Unaweza kula chembechembe za sabuni zilizoingia kwenye bidhaa za vyakula," limeonya shirika la FDA. Na hilo huenda likasababisha kichefuchefu, kutapiaka, na hata kuharisha.

Aidha shirika hilo katika taarifa yake ya hivi karibuni, limesisitiza hatua za kuosha, kutenganisha vyakula, kupika na kuacha vipoe kwanza."

Lakini kiuhalisia hatua hizi huwa zinafanyika sio kwasababu ya janga la corona.

"Ingawa kuna uwezekano mdogo wa virusi kusambaa kupitia vyakula vilivyoathirika au bidhaa, hatua za kawaida za usafi, kama vile kuosha mikono na kanuni za usafi za kuzingatiwa wakati wa kutayarisha chakula, lazima zifuatwe," kwa mujibu wa Taasisi ya Serikali ya Ukadiriaji wa Athari za Majanga.

Pia taasisi hiyo imeongeza kwamba kwasababu virusi haviendani na kiwango cha juu cha joto, hatari ya maambukizi inaweza kupunguzwa zaidi kwa kupasha chakula moto."

Mujer en un mercado en Caracas, Venezuela

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Hakuna ushahidi kwamba vyakula vinaweza kusambaza covid-19, lakini hilo halimaanishi kwamba kufanya manunuzi ni salama.

Katika ulaji wa bidhaa za wanyama, Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) linatenganisha makundi.

"Nyama iliyotokana na wanyama na kupikwa vizuri bado ni salama," hilo limeandikwa upande wa taarifa za kwenye tovuti yao.

Hilo pia ni salama kwa vyakula vya baharini na samaki ambavyo vinafikiwa viwango vya afya vya kiamataifa.

Aidha shirika hilo limeweka bayana kwamba watu wasichinje, kuvalisha, kuuza, kutengeneza au kula protini ya wanyama ambayo chanzo chake ni mnyama wa mwituni au ngome waliokuwa wagonjwa au wale ambao wamekufa kwa ugonjwa usiojulikana.

Ingawa bado haijathibitishwa kwa asilimia 100, kila kitu kinaonekana kuonesha kwamba chanzo cha virusi vya corona ni mji wa China wa Wuhan ambao unauza nyama ya mwituni kwa kiasi kikubwa tu masokoni, ikiwa ni pamoja na paka na popo ambao ni washukiwa wakuu wa chanzo cha virusi vya corona.

Pollo crudo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watu wengi wanatabia ya kusoha kuku mbichi, lakini Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa Marekani kinasema hilo ni hatari kipindi hiki cha janga la Corona.

Vipi kuhusu vyakula vilivyosindikwa?

"Magonjwa ya virusi vya corona yaliotangulia ya SARS na MERS, bado yanaweza kuhimili baridi na yanaweza kuambukiza hata katika nyuzi joto 20 hasi kwa kipindi cha hadi miaka miwili vikiwa katika mfumo wa kuganda kwenye barafu," kulingana na taarifa ya Taasisi ya Serikali ya Ukadiriaji wa Athari za Majanga..

Hata hivyo taarifa hiyo imeendelea kwamba, hadi kufikia sasa hakuna ushahidi kwamba virusi vya of SARS-CoV-2 ya covid-19 vinaweza kusambaa kupitia ulaji wa chakula, ikiwemo kile kilichogandishwa."

Nyumbani

Kuagiza kuletewa chakula nyumbani hatari ya kuambukiza inapungua na hasa iwapo atakaye kileta ataomba kukiacha mlangoni na pia namna kilivyofungashwa.

Kulingana na shirika la Bloomfield, hatari ya maambukizi kwa kutumia chombo aina ya kontena, inaweza kupunguzwa kwa "kumimina chakula hicho kwenye bakuli safi, kutupa vifaa vilivyotumiwa kufungashia kwenye dude la takataka na kuosha mikono yako vizuri kabla ya kuanza kula."

"Pia toa chakula hicho kwenye kontena yake ya awali kwa kutumia kijiko na kukila kwa kutumia kijiko au uma wala sio mikono yako," taasisi hiyo iliongeza.

Wengine wanaweza kuchukua tahadhari zaidi kwa kukipasha moto kabla ya kula.

Maelezo zaidi

Nguo

Bado haijabainika kirusi hicho kinaweza kusalia kwa muda gani kwenye nguo au katika sehemu iliyopata maambukizi.

Hivyobasi, masomo ya mtandao kuhusu covid-19 yaliyotolewa katikati ya Februari na Kituo cha Kuzuia na kudhibiti Usambaaji wa Magonjwa cha Ulaya kilipendekeza kuwa na mazoea ya kuosha sehemu unazotumia kila mara, nguo na vifaa vinavyotumika kama njia moja ya kuzuia maambukizi majumbani.

Kwa nguo, kituo hicho kilieleza kwamba ni lazima zioshwe kulingana na maagizo ya kampuni iliyotengeneza na kuanikwa kwa kiwango cha joto kilichopendekezwa.

Aidha Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha Marekani kimetoa mwongozo mzuri wa namna ya kuosha nyumba ikiwa ni pamoja na kuosha nguo lakini hilo linafanyika iwapo unashuku huenda maambukizi yameingia katika familia. Hili ni sawa na kwamba hii ni hatua ya mwisho mwisho kabisa.

Mapendekezo hayo yaliyotolewa Machi 28 ni pamoja na kuvaa glovu wakati unaosha nguo, na baadae utaosha mikono yako, usikukute nguo kabla ya kuzianika, pia ikapendekezwa kuosha nguo kwa kutumia maji moto kabisa ikiwezekana.

"Nguo za mgonjwa zinaweza kuoshwa kwa pamoja na nguo zingine," kulingana na taarifa iliyotolewa na Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha Marekani (CDC), na tena kwa kutumia sabuni.

Kwa uapnde wa Shirika la Afya Duniani, limeendelea kusisitia unyunyizaji wa kemikali yenye kiwango fulani cha pombe au klorini kwenye nguo huku wengine wakisema kuwa hatua hiyo "unaweza kutoboa nguo na utando telezi ( yaani macho, mdomo, na kadhalika. Lakini pombe au klorini vinaweza kutumiwa wakati wa kuosha sakafu.