Upasuaji wa kubadili Maumbile Uturuki: Mwanamke aingiwa na hofu baada ya mchakato alioupitia

Kimberley in bandages after her operation

Chanzo cha picha, Kimberley Sadd

Maelezo ya picha, Bi. Sadd alipata maambukizi baada ya kufanyiwa upasuaji mara mbili

Mwanamke mmoja anahitaji kufanyiwa upasuaji wa kuboresha na kubadili maumbile baada kufanyiwa upasuaji nchini Uturuki na kuachwa na kovu kubwa.

Kimberley Sadd, 27, kutoka Ogmore Vale, Bridgend, alifanyiwa upasuaji mara mbili wenye kugharimu £6,000, 2019 na ameonya wengine juu ya kukimbilia kufanyiwa upasuaji nchi za nje unaoonekana kuwa gharama yake ni ya chini.

Daktari wa upasuaji Dean Boyce, kutoka hospitali ya Morriston, Swansea, amesema wagonjwa wanastahili kuangalia zaidi ya mbele na kutafakari yajayo.

BBC Wales imezungumza na kampuni ya Comfortzone, ambayo ilifanya upasuaji wa Bi Saad lakini hawakufanikiwa kupata jibu.

Bi Sadd, ambaye alikuwa na uzani wa karibia kilo 146, amezungumza na kipindi cha Gareth Lewis katika kituo cha BBC Radio Wales, ma kusema kwamba aliamua kufanyiwa upasuaji wa kukuza matiti na kupunguza tumbo baada ya kupunguza kilo 57 na kumuacha akiwa na ngozi ya ziada inayoning'inia.

Alisafiri hadi Uturuki Machi 2019, kwasababu gharama ya upasuaji aliohitaji huko ilikuwa ya chini wakidai kwamba wanatoa ofa hiyo ni ikiinganishwa na huduma sawia na hiyo iliyokuwa inatolewa Uingereza. Ofa hiyo ilionyeshwa katika tovuti ya kampuni ya Comfortzone.

Lakini alichopitia ni tofauti na alichokuwa akitarajia.

"Hospitali ilikuwa ni ya kitambo na ilikuwa vichochoroni," amesema.

"Nilikutana na daktari wa upasuaji asubuhi ya upasuaji. Wakaniweka kwenye lifti na wala sikupimwa uzito kabla ya kudungwa dawa ya kugandisha mwili."

Kimberley Saad

Chanzo cha picha, Kimberley Sadd

Maelezo ya picha, Kimberley Sadd alitakata kufanyiwa upasuaji baada ya kuwa na nyama nyingi zinazoning'inia tumboni baada ya kupunguza uzito wa mwili.

Alisema kwamba upasuaji wa mara ya kwanza haukufanikiwa kuondoa ngozi hiyo na moja ya titi lake lilikuwa linaning'inia.

Bi Sadd alisema kwamba kampuni ya Comfortzone aliamua kumfanya upasuaji kwa mara nyengine, lakini jeraha lake halikupona na juu yake akapata maambukizi.

Pia alikuwa na wasiwasi na usafi wa eneo la wagonjwa waliolazwa alipokuwa baada ya kufanyiwa upasuaji.

"Wauguzi hawakuwahi kuvaa aproni wakati walipokuwa wanambadilisha bendeji," amesema.

"Na vifaa vya baada ya kufanyiwa upasuaji vilikuwa vinaachwa chooni. Yaani huduma yao ilikuwa mbovu.

"Nimekuwa na matatizo tu. Vidonda vimetengenza usaha na makovu yanaendelea kutanuka.

"Nimeenda katika hospitali kuu ya NHS mara tatu tangu nimerejea Uingereza na kupata dawa za kuzuia na kutibu bakteria kwa njia ya mishipa kwenye mkono wangu."

Bi Sadd analipia kufanyiwa upasuaji wa kuboresha na kurekebisha maumbile kwa gharama ya £10,000.

Kimberley Saad

Chanzo cha picha, Kimberley Sadd

Maelezo ya picha, Bi Sadd alikuwa na uzito wa karibia kilo 146 kabla ya kufanyiwa upasuaji

Dean Boyce, kutoka chama cha upasuaji wa kurekebisha maumbile amesema: Huu upasuaji si kama kununua nguo mpya ya kuvaa. Upasuaji huu una hatari zake. Fikiria kuhusu vile mambo yatakavyoenda mrama - iwapo utatumia hospitali za mitaani bila shaka daktari wako atakuwa wa mitaani vilevile.

"Sababu ambayo inafanya watu wengi kukimbilia hospitali za nje ni gharama. Kwa baadhi ya nchi gharama iko chini zaidi lakini jaribu kupiga darubini. Ni mwili wako utakaopitia upasuaji huu na unachohitaji ni kupata huduma bora na salama kadiri inavyowezekana."

BBC Wales imejaribu mara kadhaa kuwasiliana na kampuni ya Comfortzone bila mafanikio yoyote.

Pia unaweza kutazama:

Maelezo ya video, Fahamu hatari ya kuongeza maziwa