Visa vya watu kutumia kiholela bidhaa bandia za urembo vimeongezeka China

Mfumo huu wa urembo ni biashara kubwa China

Chanzo cha picha, Science Photo Library

Maelezo ya picha, Mfumo huu wa urembo ni biashara kubwa China

Polisi nchini China imefanya msako mkali dhidi ya bidhaa bandia za urembo.

Bidhaa hizo zinazokadiriwa kuwa za thamani ya karibu dola milioni 4.3 zinajumuisha sindano za kuongeza makalio bandi na zile za kuongeza vitamin C miongoni mwa bidhaa zingine.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Xinhua, bidhaa hizo zimekuwa zikiuzwa na mtandao wa wafanyibiashara haramu kwa kipindi cha miezi sita.

Mamlaka imewafungulia mashataka watu watano waliyokamatwa katika msako huo.

Bidhaa bandia za urembo zinasadikiwa kuuzwa katika miji mbali mbali nchini China.

Mara ya kwanza mamlaka kubaini ukubwa wa biashara hiyo ilikuwa mwezi Septemba baada ya kufanywa kwa msako wa kushutukiza katika maduka kadhaa ya urembo mjini Changde.

Bidhaa zinazouzwa katika maduka ya urembo ziligunduliwa kuwa za mfanyibiashara mmoja aliyepo mkoa wa Jilin - kwa jina la Zuo -ambaye anaziuza kupitia mtandao wa kijamii wa WeChat.

Kilio cha uchungu baada ya upasuaji wa pua ili kunyooshwa

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kilio cha uchungu baada ya upasuaji wa pua ili kunyooshwa

Polisi walivamia bohari la bwana Zuo ambapo chupa 2,300 za kemikali ya aina ya hyaluronic acid -ambayo hutumiwa sana kutengenezea mafuta ya kupaka na bidhaa zingine bandia za urembo.

Rekodi ya usafirishaji bidhaa za bwana Zuo zinaonesha kuwa bidhaa hizo tayari zimetumiwa wateja 10 katika mikoa tofauti.

China ni moja ya soko kubwa la upasuaji wa urembo duniani na pia imekuwa na ongezeko la watu wanaotafuta matibabu mbadala.

Serikali ya China imekuwa na wakati mgumu kuwaonya raia wake kuhusu hatari inayotokana na matumizi ya bidhaa feki za urembo.

Hii ni baada ya watumiaji wa bidhaa hizo kujipata hospitali wakipigania maisha yao kufuatia upasuaji wa uremboo uliyotibuka.

Kumeshuhudiwa visa kadhaa vinavyohususishwa utumiaji holela wa bidhaa bandia za urembo ambazo huagizwa kutoka nje.

Sio China peke yake ambko biashara ya urembo bandia imenoga hata Venezuela ambako wanawake wanapenda sana makalio bandia
Maelezo ya picha, Sio China peke yake ambko biashara ya urembo bandia imenoga hata Venezuela ambako wanawake wanapenda sana makalio bandia

Korea Kusini pia inakabiliwa na tatizo la urembo bandia

Huwezi kuepuka matangazo ya mauzo kila unapotembea katika mji wa Seoul,utapata wito wa kukutaka ubadilishe umbo kwa njia ya upasuaji wa kuongeza urembo bandia.

Katika mtaa wa ukwasi wa Gangnam,kila ukuta una ishara ya kukuelekeza sehemu ya upasuaji wa aina hii.

Kwenye treni na mitaani, unaelezewa kuwa ''unaweza kurudisha uchanga usoni mwako.''kuweka ama kuondoa mikunjo usoni'' inapendekezwa kufanyiwa-''upasuaji wa matiti''

Upasuaji mwingine ni wa ''kuzuia kuzeeka'' ''kubadili kope za macho''''kupunguza nyama na ngozi inayolegea mwilini''.

Mwanamke

Pia kuna ''kupunguza taya na kuzifanya mraba''(matangazo haya hasa huashiria wanaume).Ama kubadili uso wako ''kutoka ngozi ilioangika na isiyo imara hadi ile inayojivuta na bora.'' ambayo inaelekezwa kwa wanawake.

Nchini Venezuela pia kumekuwa na ripoti za wanawake kutumia kemikali haramu kuongeza ukubwa wa makalioyao na kujiletea madhara makubwa ya kiafya

Hii ni kutokana na mtindo ambao unaonekana na wengi nchini humo kwamba mwanamke mwenye makalio makubwa ndiye anayependeza zaidi

Wanawake wengi sasa wanahatarisha afya zao kwa kutaka kuwa 'warembo'