Mauaji ya Khashoggi: Maseneta nchini Marekani wanaamini bin Salman aliamuru mauaji, wamuita mtu "hatari" na "chizi"

Mohammed bin Salman

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Saudi Arabia inasema mwanamfalme Mohammed bin Salman hakuhusika na mauaji ya Khashoggi
Muda wa kusoma: Dakika 3

Maseneta nchini Marekani wanaamini pasi na shaka sasa kuwa mwanamfalme Mohammed bin Salman amehusika katika mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi.

Msimamo huo wa maseneta unakuja baada ya kufanya kikao cha siri na mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, Bi Gina Haspel.

Seneta wa mwenye ushawishi mkubwa kutoka chama cha Republican Lindsey Graham amesema ana "imani ya hali ya juu" kuwa Mohammed bin Salman (MBS) alipanga njama ya kumuua Khashoggi.

Seneta huyo wa jimbo la Carolina Kusini amesema bin Salman ni "chizi" na "mtu hatari".

Khashoggi aliuawa ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2. Mwanahabari huyo alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa sera za Saudia hususani mwanamfalme bin Salman.

Tayari Saudia imewashitaki watu 11 juu ya mauaji hayo, lakini wanakanusha vikali juu ya uhusika wa bin Salman.

Mkurugenzi wa CIA bi Haspel alikutana jana Jumanne na wajumbe wa Seneti wa Kamati ya Mambo ya Nje ambao hawakumung'unya maneno baada ya mkutano huo.

"Hapa hakuna bunduki inayofuka moshi - kuna msumeno unaofuka moshi," amesema Seneta Graham akimaanisha mauaji ya Khashoggi yanayodaiwa kutekelezwa kwa kumny'onga kisha kumkata mwanahabari huyo vipande kwa kutumia msumeno.

Gina Haspel

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Gina Haspel awali ilidaiwa kuwa alikasirishwa na kuvuja kwa ripoti ya CIA

Seneta huyo amesema hatounga mkono ushiriki wa Saudia katika vita vinavyoendelea nchini Yemen na pia mauzo ya silaha kwa serikali ya Saudia kama bin Salman ataendelea kusalia madarakani.

Seneta Bob Menendez wa chama cha Democrat ameunga mkono msimamo wa Seneta Graham.

Mendez anayetoka jimbo la New Jersey amesema: "Marekani lazima itume salamu za wazi bila kubabaisha kuwa vitendo kama hivyo (mauaji) havikubaliki."

Seneta mwengine kutoka chama cha Republican, akitumia jina maarufu la mwanafalme huyo la MBS amesema: "Sina hata swali moja kichwani mwangu juu ya kuwa MBS aliamuru mauaji hayo (ya Khashoggi)."

Seneta huyo meongeza kuwa : "Laiti MBS angesimamishwa mbele ya mahakama, angehukumiwa ndani ya dakika 30. Anahatia."

Seneta Corker ameonesha wasiwasi wake kuwa rais Donald Trump amepuuzia mauaji hayo kwa kushindwa kumlaani bin Salman.

Bunge la Seneti sasa linapanga kupigia kura mapendekezo ya kusitisha uungaji mkono kijeshi wa Marekani kwa Saudia na washirika wake katika vita inyoendelea Yemen. Tayari wajumbe wa vyama vyote viwili vya Democrat na Republican wameshakubaliana katika hatua ya mwanzo ya pendekezo hilo.

Seneta Chris Murphy, ambaye hakuwepo kwenye mkutano na bi Haspel ameutuhumu utawala wa Trump : "Sio kila kitu kinatakiwa kufanywa kuwa siri," ameandika seneta huyo wa jimbo la Connecticut kupitia chama cha Democrat kupitia mtandao wake wa twitter.

"Kama serikali yetu inajua kuwa viongozi wa Saudia walishiriki mauaji ya mkaazi wa Marekani (Khashoggi) kwa nini umma usiambiwe ukweli?"

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

CIA wamesema nini?

CIA wamehitimisha kuwa Mohammed bin Salman "yawezekana aliamuru" mauaji ya Khashoggi.

Shirika hilo la ujasusi lina ushahidi unaonesha kuwa bin Salman aliwasiliana kwa wa ujumbe nfupi wa simu ya mkononi na Saud al-Qahtani ambaye inadaiwa ndiye aliyeongoza operesheni ya mauaji ya Khashoggi.

Wiki iliyopita bi Haspel hakuhudhuria mkutano na kamati hiyo ya Seneti na Ikulu ya White House imekanusha kuwa ilimzuia asihudhurie. CIA pia imesema hakuna mtu aliyemwambia mkuu wao asihudhurie kikao hicho.

Katika kikao cha wiki iliyopita Waziri wa mabo ya nje wa Marekani Mike Pompeo na waziri wa ulinzi James Mattis waliwaambia maseneta kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaomhusisha bin Salman na mauaji hayo.

Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa mstari wa mbele kumtetea bin Salman akidai kuwa ripoti ya CIA haikuhitimisha kinagaubaga kuwa mwanamfalme huyo aliamuru Khashoggi auawe.

Presentational grey line

Jamal Khashoggi ni nani?

Akiwa mwanahabari mashuhuri, aliripoti habari kubwa kama uvamizi wa Usovieti nchini Afghanistan na kufanya mahojiano na Osama Bin Laden.

Saudi journalist Jamal Khashoggi in Istanbul, Turkey, 6 May 2018

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jamal Khashoggi alienda Istanbul kushughulikia mchakato wa ndoa yake

Kwa miongo kadhaa alikuwa na ukaribu na familia ya kifalme ya Saudia na pia aliwahi kuhudumu kama mshauri wa serikali.

Hata hivyo alijitenga na utawala wa sasa na kuwa mkosoaji kisha kukimbilia nchini Marekani akihofia maisha yake mwaka jana. Akiwa Marekani alikuwa akiandika makala kila mwezi katika gazeti la Washington Post ambapo aliendeleza harakati zake za kumkosoa Mohammed bin Salman.