LGBT: Simulizi za madhila ya watu wa mapenzi ya jinsia moja nchini Nigeria

Chanzo cha picha, Getty Images
Jaji wa mahakama moja nchini Nigeria ameahirisha kwa mara nyenegine kesi ya wanaume 47 nchini Nigeria wanotuhumiwa kuonyesha mapenzi ya jinsia moja hadharani baada ya ushahidi mmoja wa upande wa mashtaka kukosa kuhudhuria kesi hiyo.
Katika kesi hiyo jaji alionekana amekasirishwa kwamba upande wa mashtaka ulikuwa umeshindwa kuendelea na kesi.
Kesi hiyo imeahrishwa mara nne kutokana na maswala ya kisheria.
Jaji alionya upande wa mashtaka kwamba katika kikao kijacho atafutilia mbali kesi hiyo iwapo upande wa mashtaka utashindwa kuendelea.
Hivi karibuni, nchi imeshuhudia juhudi mpya ya kuwaadhibu watu wa jinsia moja.
Mnamo Januari 7, 2014, Rais wa wakati huo wa Nigeria, Goodluck Jonathan, alisaini muswada wa sheria wa kupiga marufuku ndoa za jinsia moja.
Wanaharakati wanasema sheria imezidisha ubaguzi dhidi ya makundi hayo katika nchi hiyo inayozingatia maadili ya kidini.
Wanadai pia kumekuwa na kuongezeka kwa matukio ya unyang'anyi na ulaghai dhidi ya watu wa mapenzi ya jinsia moja yanayodaiwa kufanywa na vikosi vya usalama.
Mwandishi wa BBC wa Nigeria Mayeni Jones alizungumza na watu 3 kuhusu maana ya kuwa watu wa kundi hili magumu wanayopitia. Majina yao yamebadilishwa kuzuia utambulisho wao.
Kumwagiwa mafuta
Apunanwu anasema aliamua mwenyewe kwenda kunakoitwa ''tiba ya kuondokana na hali waliyonayo''
Hivi ndivyo anavyosema kuhusu yanayofanyika wakati wa tiba hiyo.

''Nilinyanyua miguu yangu kisha wakamwagia mafuta kwenye sehemu zangu nyeti.''
''Sasa sijui kilichopo ndani ya mafuta hayo kwa sababu yalikuwa kama yanawasha, yalikuwa yananifanya nijihisi sina utulivu.''
Hakuwa akishawishika kama kuwa hilo lingesaidia chochote.
'' Kwangu mimi niliona ni suala la kuudhi kwa sababu sehemu zangu nyeti zinauhusiano gani na utakaso?''
''Lakini kwa wakati huo sikujua lolote , hivyo kwangu nilikuwa tayari kufanya chochote kuondoa ile hali ya kuvutiwa na watu wa jinsia kama yangu, nilikuwa tayari kufanya chochote kuondokana na hali hiyo.''
Kuchapwa siku tatu

Kila mtu ananiona kama laana, kuwa sikuwa mtu niliyepaswa kuendelea kuishi.''
''Nilikulia katika familia ya kikristo, iliyoshika dini sana inayoamini mahusiano ya jinsia moja ni ushetani.''
Kaka yake alishampeleka ''nabii'' aliyemlazimisha kuingia kwenye tiba ya kumbadilisha tabia.
''Alikuwa akifika mara kwa mara kwa ajili ya 'mambo ya kiroho'', ambapo pia alinivua nguo na kubaki mtupu kisha akanichapa.''
''Siku ya kwanza, alinifanyia hivyo mara saba, kwa nyakati tofauti mara saba. Akafanya hivyo siku ya pili, ikawa mara 14.''

Chanzo cha picha, BBC
Alishindwa kuvumilia, uvumilivu wa maumivu ulitoweka kisha akaishiwa nguvu.
''Kisha siku ya tatu, kutokana na kuchoshwa na maumivu niliyokuwa nayapitia, Nilizimia.''
''Mimi ni binadamu''
''Ni jambo la kuogofya kuwa mtu wa mapenzi ya jinsia moja nchini Nigeria.''
Gabriel anaeleza alivyokumbana na polisi.
''Hauna haja ya kukubali kuwa wewe ni mtu wa mapenzi ya jinsia moja, lakini unapaswa kuelewa (unavyojisikia) kusimamishwa ukiwa kwenye pikipiki ukijaribu kwenda mahali kwa haaka, kisha unakamatwa kwa nguvu na kusukumiwa kwenye gari.
Wanaharakati wanasema baada ya sheria ya mwaka 2014 kumekuwa na namna ya wazi ya kushtaki na kupata fedha kutokana na kosa la kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja.

''Sikujua kama walikuwa polisi, kwa kuwa wote hawakuvaa sare ya kazi. walivaa mashati meusi. Kusukumwa kwenye basi na kutishiwa kubakwa haikubaliki kabisa.
Huna haja kuwapenda watu wa undi hili, lakini unapaswa kuelewa, kama mtu uliyestaarabika hupaswi kuvuka mstari.''
Gabriel anaomba jamii ibadilike.
''Sihitaji zaidi. Ninaomba tu masuala ya msingi, tafadhali elewa mimi ni binaadamu. Na kama wewe, nina haki muhimu za kibinadamu.''













