Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Waombolezaji wajitokeza kwa wingi kupokea mwili wa Soleimani
Maelfu ya waombolezaji wamekusanyika mitaani nchini Iran ili kupokea mabaki ya jenerali Qasem Soleimani aliyeuliwa katika shambukizi la la anga wiki iliyopita .
Mjini Avhaz, Waombolezaji wanajipiga vifua huku wakiimba "kifo cha Marekani".
Soleimani alikuwa kiongozi wa jeshi la Iran ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa katika nchi za mashariki ya kati na alikuwa anatambuliwa kama mtu wa pili anayeheshimika zaidi katika nchi yake.
Mauaji yake yameleta uhasama mkubwa kati ya Iran na Marekani.
Kiongozi wa Iran, Ayatollah Khamenei, ambaye alikuwa na uhusiano wa karibu na Soleimani, ametoa angalizo la kulipa kisasi shambulio hilo, na wachambuzi wanasema kuwa Iran inaweza kufanya shambulizi dhidi Marekani au kufanya shambuli lolote ikiwalenga wamarekani au maslahi ya Marekani.
Rais Trump, ambaye aliyeidhinisha shambulio hilo dhidi ya Soleimani siku ya ijumaa - jambo ambalo watangulizi wake Rais Obama na Bush walipinga kwa kuona kuwa ni jambo hatari sana - Trump alisema siku ya jumamosi kuwa Marekani iko tayari kufanya mashambulizi 52 katika maeneo muhimu ya Iran.
Katika mfululizo wa ujumbe wa mtandao wa kijamii wa Twitter alizungumzia suala la jinsi nchi mbili zinaweza kupitia katika vita.
Trump alisema kuwa Marekani itapambana na Iran "TUTAPAMBANA NAO HARAKA NA NGUVU ZAIDI" kama Iran imepanga kuvamia majeshi ya Marekani.
Trump alisema kuwa sehemu 52 ambazo zimelengwa zinawakilisha wamarekani 52 ambao walishikiliwa mateka kwa zaidi ya mwaka mmoja mwaka 1979 baada ya kutekwa nyaka katika ubalozi wa Marekani uliopo Tehran.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alijibu ujumbe huo wa Twitter na kusema kuwa kumuua Soleimani ulikuwa uvunjaji wa sheria za kimataifa na kama watalenga kuvamia eneo lolote la utamaduni ,itakuwa ni kuanzisha uhalifu wa kivita.
Nini kinachoendelea Iran?
Maelfu ya waombolezaji wakiwa wamevaa mavazi meusi wamekusanyika mitaani katika mji wa Ahvaz kusini magharibi mwa Iran, wakati ambao mwili wa Soleimani ulipokuwa unawasili.
Chombo cha habari cha taifa cha Irib, kimeonyesha video ya jeneza la Soleimani lililokuwa limezungushiwa bendera ya Iran likishushwa kutoka katika ndege ya jeshi huku bendi ya jeshi ikiiimba.
Vilevile kituo hicho kimeonesha umati mkubwa wa watu waliokusanyika katika makutano ya mji wa Mollavi, huku wakipeperusha bendera na wakiwa wameshika picha nyingi za Soleimani, ambaye anaonekana kuwa shujaa na watu wengi wa Iran kutokana na kazi yake ya jeshi ambayo alishiriki vita kati ya Iran na Iran mwaka 1980.
Umati mkubwa wa watu unatajwa kudhihirisha umuhimu wa kiongozi huyo wa jeshi katika taifa hilo.
Umati mkubwa wa watu unatajwa kudhihirisha umuhimu wa kiongozi huyo wa jeshi katika taifa hilo.
Siku tatu za maombolezo katika maeneo yote ya nchi hali iko hivyo.
Katika mji mkuu wa Tehran,wabunge pia wakiimba "Death to America"( Kifo kwa Marekani) dakika chache kabla ya taarifa kutoka chombo cha habari cha Isna hakijaripoti kuwa, "Trump, hii ni sauti ya wairani na taifa lake , sikiliza," msemaji Ali Larijani alinukuliwa.
Tahadhari kuhusu Kataib Hezbollah ilitolewa na jeshi la usalama la Iraqi mwishoni mwa wiki wakati majeshi ya Marekani yako umbali usiopungua 1,000m (0.6 miles) iliripoti televisheni ya , al-Mayadeen.
Marekani imeongeza vikosi 3,000 zaidi Mashariki ya kati na kushauri raia wake kuondoka Iraq haraka iwezekanavyo.
Miili ya Soleimani, al-Muhandis na wahanga wengine imerejeshwa leo kwa ajili ya shughuli za msiba.
Siku ya jumatatu, kiongozi wa taifa hilo anatarajia kuongoza ibada ya kumuomboleza Soleimani katika chuo kikuu cha Tehran , na baadae kuongoza maandamano ya kuelekea nyumbani kwake Kerama.