Uchaguzi mkuu 2019: Uongozi wa chama wakubali kuchangia katika matokeo duni ya chama

Jeremy Corbyn na John McDonnell wajishusha kwa shoka lililoangukia chama cha Leba katika uchaguzi uliofanyika Alhamisi iliyopita na kupoteza viti 59.
Bwana Corbyn ameomba msamaha kwa kupoteza viti vingi huku McDonnell akiiambia BBC kwamba anabeba lawama.
Kiongozi huyo amesema kwamba atajiuzulu mwaka ujao.
Kinyang'anyiro cha kuwarithi tayari kimeanza huku mbunge wa Wigan, Lisa Nandy akisema kwamba kwa mara ya kwanza ameanza kuliwazia suala la kuwa kinyang'anyironi.
McDonnell amesema kamati ya chama cha Leba ndio itakayoamua mchakato ukaotumiwa kumchagua kiongozi lakini anatarajia kwamba hilo litafanyika katika kipindi cha wiki 8 hadi 10.
Chama cha Leba kimepata pigo kubwa katika uchaguzi mkuu uliopita tangu mwaka 1935 huku kura zao zikipungua kwa alama nane.
Chama cha Conservative kilipata ushindi wa asilimia 80 - ushindi mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa ndani ya miaka 30 na kuchukua viti vya maeneo ambayo awali yalichukuliwa kuwa ngome ya chama cha Labour.
Pia unaweza kusoma:
Bwana Corbyn aliomba msamaha wafuasi wa chama cha Labour katika makala mbili kwenye gazeti la Sunday, na kusema ''hili lilikuwa pigo kubwa kwa kila mmoja aliyekuwa anataka mabadiliko nchini mwetu''.
Katika barua ya wazi kwenye Sunday Mirror, alisema kwamba "anachukua lawama'' lakini akaongeza kuwa bado anajionea fahari kwa kampeni zilizopigwa na chama hicho.
Alisisitiza kuwa kampeni yake ilifanikiwa kuweka misingi ya kuzingatia katika mjadala na kwamba manifesto yake itakuwa kitu muhimu katika historia.

Chanzo cha picha, Reuters
Hata hivyo, McDonnell amesema kwamba yeye ndo wa kulaumiwa wakati anazungumza katika kipindi cha Andrew Marr cha BBC.
McDonnel ameongeza kwamba anaomba msamaha kwa kushindwa kueleza kwa ufasaha ujumbe wa chama wakati wa kampeni kabla ya siku ya kupiga kura.
Hata hivyo, pia amelaumu taswira iliyojengwa na vyombo vya habari kwa kufasiri vibaya msemo wa Corbyn wakati wa kampeni.
Aliyekuwa mbunge wa chama Labour Caroline Flint - ambaye alipoteza kiti chake na kutupia lawama uongozi wa chama.
Pia alikosoa msimamo wa chama kuhusiana na Brexit kwa kushindwa kushirikisha baadhi ya wapiga kura, na kukiambia chombo cha habari cha Sky katika kipindi cha Sophy Ridge kwamba wale walioachwa nyuma kama kina Sir Keir Starmer na waziri wa mambo ya nje Emily Thornberry, walichangia kuchukuliwa kwa baadhi ya viti.

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images
Caroline Flint alimshtumu Thornberry kwa kumwambia mmoja wa wabunge anayeunga mkono Brexit kwamba: "Nafurahi watu wa eneo langu siyo wajinga kama wa eneo lako."
Hata hivyo, Thornberry amesema shutuma hizo zilikuwa ''uwongo mtupu''. Ameongeza kwamba: ''Sijasema kitu kama hicho kwa yeyote na siwezi kufikiria kitu kama hicho''.
Flint ameongeza: "siamini kwamba mtu ambaye amekuwa mwanzilishi wa sera ya Ulaya katika miaka ya hivi karibu ametosha kuwa kiongozi. Sioni kwamba wataweza tena kupata nafasi zilizochukuliwa na chama cha Conservertive."
Badala yake, akasema kuwa Nandy and waziri Rebecca Long-Bailey ni watu ambao wanafaa kufuatilia kwa karibu.
Bi. Nandy ameiambia BBC kwamba anafikiria kutafuta uongozi wa chama cha Labour baada ya kipindi hicho kushindwa kwenye uchaguzi mkuu.
"Katika miji kama wa kwangu, ardhi ilikuwa inatingishika wakati chama Labour kina poromoka chini ya miguu yetu," akaongeza.
Nandy alitoa mapendekezo kadhaa ikiwemo kuhamisha makao makuu ya chama hicho hadi mjini London kusaidia kuimarisha muungano huo na kuwa tena na chama kinachozungumza kwa niaba ya wote.
Kuna wagombea wengine ambao wanatarajia kujiunga na king'anyiro hicho wakiwemo, wabunge wa maeneo ya Salford and Eccles, Long-Bailey na Jess Phillips wa chama cha Birmingham Yardley.
Bi. Phillips ameomba wafuasi wake kujitosa uwanjani ili kukibadilisha chama cha Labour na kusema kuwa watu wengi wa daraja la wanaofanyakazi hawaamini kwamba chama hicho kinaweza kufanya vizuri kuliko chama tawala.

Chanzo cha picha, Reuters and PA Media












