Uber inaweza kendeshwa bila faida?

Chanzo cha picha, EPA
Wadau wa Uber wamekua wakisubiri kwa hamu kupata faida ya uwekezaji wao- lakini kulingana na ripoti ya hivi karibuni, itawabidi wasubiri malipo yao kwa muda mrefu zaidi.
Uber imekuwa ikipanua wigo wa wateja wake na kuongeza shughuli zake zaidi.
Katika robo ya mwaka 2019, mapato yalikuwa hadi 30% ikilinganishwa na mwaka uliotangulia ambapo ilipata mapato ya dola bilioni dola bilioni 3.8 -matokeo ambayo yalipiku tathmini ya kiwango cha wachambuzi .
Bado, Uber ilipata hasara ya dola bilioni $1.2, kiwango hiki kikiwa ni kikubwa kuliko kile walichopata mwaka uliotangulia cha hasara ya dola milioni 986, lakini kikiwa ni chini ya hasara ya dola bilioni 5.2 katika kipindi cha robo ya mwaka uliotangulia.
Wawekezaji waliyapa matokeo haya kiwango gani?
Teknolojia ipo kwa kila mtu
Programu shirikishi ya safari imekuwa sokoni kwa miaka kumi na huduma yake ya kuwapelekea huduma wateja nyumbani imepanuka na huweza kutumiwa na mteja mwenyewe.
Teknolojia ya kampuni, inayomuunganisha moja kwa moja mtumiaji na mtoaji huduma, ilikuwa wakati mmoja ni ya faida, anasema Adam Leshinsky, muasisi wa "Wild Ride: Inside Uber's Quest for World Domination".
Lakini kwa sasa haina tena faida hiyo?

Chanzo cha picha, Getty Images
"Baada ya muda ,teknolojia hiyo inapatikana kwa karibu kila mtu, yakiwemo makampuni ya teksi, ambayo yalipunguza faida ya Uber " Leshinsky aliambia BBC.
Kuimarika kwa Uber kwa sasa labda ni "kufikiwa na watu wengi na urahisi wa matumizi yake", aliongeza.
Lakini kuna udhaifu pale: Utaratibu ambao ulitumiwa na Uber -pamoja na mahasimu wake kama vile Lyft nchini Marekani- kukua kwake kutategema kuweka viwango vya chini vya ruzuku za safari.
Leshinsky inaamini kwamba makampuni haya yanawerza kuimarisha tu iwapo wataacha mfumo huu wa huduma zao.
Lakini hili litasababisha kupanda kwa gharama za usafiri na labda kuleta athari kwa wateja wake wanaotumia programu
Ni jambo hili linaloiweka Uber katika hali ngumu.
"Kama watapata faid , itabidi wakose ukuaji. Tayari wanajaribu kupunguza matumizi ,lakini kadri wanavyofanya hivyo, ndivyo inavyokuwa vigumu kuendeleza biashara ,"Leshinsky anasema.
"Ninawaona wakiwa katika hali ya kudumaa kibiashara kama hivyo kwa muda mrefu ."
Mzozo wa wafanyakazi

Chanzo cha picha, Getty Images
Uber imekabiliwa na changamoto kutoka kwa taasisi za udhibiti wa viwango vya biashara kote duniani juu ya malipo na, la muhimu zaidi, juu ya ikiwa madereva wake wanahaki ya kuwa na haki za wafanyakazi.
Kama wameongeza thamani ya za kazi, hilo pia litapunguza fursa za kampuni za kupata faida.
Professor Peter Morici, mchumi na mtaalamu wa biashara za kimataifa katika chuo kikuu Maryland, ameiambia BBC kuwa maeneo haya yako wazi kwa mahasimu wa kibiashara wa Uber.
"Kila mara kutakua na mtu ambaye atakuja na huduma bora, kwa madereva na wateja, jambo litakalothiri hisa za soko ," anasema.
" Ninadhani nafasi hii itabaki kuwa sehemu ngumu kupata pesa kwa muda mrefu."
Unaweza pia kutazama:
Uber pia inakabiliwa na ushindani barani Ulaya kutoka kwa Via, ambayo hutoa huduma kwa wasafiri kuchukuliwa na dereva mmoja.
Ukiachana na usafiri wa abiria , chanzo kingine cha ushindani mkubwa kwa Uber ni vitengo vingine vilivyopata hasara, mkiwemo Uber Eats, ambacho ni kitengo chake cha pili kwa ukubwa.
Huduma ya uwasuilishaji wa chakula kuiletea kampuni hiyo 17% ya mapato na imepata ukuaji wa 64% katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka - lakini hasara ilikuwa ni ya 67% zaidi ikilinganishwa na mwaka jana.
Mfumo wa Amazon

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa kampuni ya Kiteknolojia ambayo imekuwa na matatizo mengi katika kupata faida, Mkurugenzi Mkuu wa Uber Dara Khosrowshahi, alisikika kama mtu anaeelewa anachokifanya alipokuwa akitangaza mafanikio ya kampuni katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka.
"Tunajua kuwa kulikuwa na matarajio ya faida na tunatarajia kupata mafanikio mwaka 2021,"alisema.
Hiyo ni ahadi ambayo inaweza kumtia mtu matumaini, lakini kampuni nyingine zimekuwa pia zikiwekeza kiwango kikubwa kipindi kilichopita ili kupata mafanikio katika ushindani wa siku zijazo.
Mfano mzuri ni kampuni ya Amazon, ambayo ilianzishwa mwaka 1994 na haikupata faida hadi 2001.
Unaweza pia kusoma:
Hasara zake zilitokana kwa kiasi kikubwa na uwekezaji wake wa miundombinu , kama vile ujenzi wa majengo ya kuhifadhia bidhaa, pamoja na kuweka misingi ya biashara.
Lakini kwa suala la Uber, wataalamu wawili wanahoji ikiwa kampuni hiyo ilijenga uhusiano wa kudumu na wateja wake na ikiwa mtindo iliyoitumia ya kibiashara ni dhamabiti kuweza kuipatia kampuni faida.
Wote kwa pamoja Morici na Leshinsky wanabashiri kwamba makampuni zaidi yataingia katika soko la usafiri huu shirikishi siku zijazo na yote watatoa huduma zinazofanana.
" Sijui ni lini na ni vipi hili litatokea, lakini ninauhakika kabisa hii itakuwa ndio hali ya baadae," Leshinsky anasema













