Sababu ya Hamas kutohusika na mashambulio ya Israel dhidi ya Gaza

Wapiganaji wa Kiislamu wa Jihad na Israel walipigana kwa siku mbili huku kundi la Hamas la Gaza likiwa kando

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wapiganaji wa Kiislamu wa Jihad na Israel walipigana kwa siku mbili huku kundi la Hamas la Gaza likiwa kando

Wiki iliyopita ghasia za ghafla juu ya Gaza zilibainika kuwa na utofauti na mapigano yaliyokuwa mpakani: Hamas ilikuwa nje ya ghasia hizo na Israeli haikulenga mahasimu wao wa kawaida.

Ilithibitishwa kuwa Israel na Hamas - ambalo ni vuguvugu kuu la kiislamu la Gaza ni limejitolea kufikia maelewano ya kimkakati kusaidia kuilinda amani.

Mapigano yalianza wakati Israeli ilifanya kile ilichokiita mauaji yaliyolenga kamanda wa ngazi ya juu katika kikundi kidogo sana chenye itikadi zaidi cha Kiislam cha Jihad, ikidai kuwa alikuwa anapanga mashambulio yanayoweza kusababisha tisho kubwa.

Mashambulio haya tata yamekuwa ya nadra tangu vita vya Gaza vya mwaka 2014 na wapiganaji wa Jihad wa Kiislamu walijibu kwa shambulio la maroketi ya moto. Ilitarajiwa Hamas watajiunga katika makabiliano hayo ili kulipiza kisasi cha mauaji ya kamanda wao,Baha Abu al-Ata.

Hamas, kundi ambalo linatawala lilishiriki katika juhudi za pamoja na vuguvugu jingine kujadili mikakati. Lakini halikuonekana kufanya mashambulio yoyote.

Ujumbe kwa Hamas

Hii ni kwasababu ilikuwa ''ni kwa faida ya Wapalestina " kuzuwia kuchochea kuendelea kwa ghasai, afisa wa ngazi ya juu wa Hamas, Basem Naim, ameiambia BBC. Wagaza tayari wanameumia vya kutosha kutokana hali ilivyo kwa sasa katika ardhi yao, alisema, na hali ya Kikanda na kimataifa haisaidii wakati huu ".

Kwa upande wao Waisrael waliacha mtindo wao wa kawaida wa kuwawajibisha Hamas kwa ghasia zozote zinazoanzia Gaza. Na waliweka wazi kwamba wanawalenga Wapiganaji wa Kiislamu wa Jihad.

Maeneo mengi ya Israel yalifungwa huku raia wakijificha kwenye hifadhi wakati makombora ya roketi za moto yaliporushwa

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Maeneo mengi ya Israel yalifungwa huku raia wakijificha kwenye hifadhi wakati makombora ya roketi za moto yaliporushwa

Wakosoaji wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu walihusisha haraka shambulio hilo na muda wa mauaji na mapambano yake ya kisiasa . Walishutumu kujaribu kutumia tataizo la usalama ili kunadi mtizamo wake katika mazungumzo ya muunga yanayolenga kuunda serikali ya mseto ambayo itamsaidia kubakia madarakani.

Lakini vikosi vya ulinzi vya Israeli vilidai kuwa yalikuwa ni mafanikio ya kijeshi. Vilimuelezea Baha Abu al-Ata kama mchokozi ambae, kwa mujibu wa mkuu wa majeshi, Luteni Generali Aviv Kochavi, alivuruga juhudi za Israel za kufikia mkataba wa kufikia mkataba wa muda mrefu na Hamas.

Mauji yake yalitafsiriwa na na vyombo vya habari vay Israeli kama ujumbe kwa Hamas kwamba Israel ilitaka kusalia na viwango hivi makubaliano ,yaliyofikiwa baina ya Misri, Qatar na Umoja wa Mataifa mwaka mmoja uliopita.

'Maslahi ya pamoja'

Hamas na Israel ni mahasimu wa muda mrefu. Israel iliimarisha mkataba wake wa ukanda wa Gaza wakati Hamas ilipoimarisha mamlaka yake huko mwaka 2007 na tangu wakati huo imekwishafanya mashambulio mkubwa ya kijeshi ili kuzuwia mashambulio ya roketi kutoka kwenye eneo la mwambao.

Lakini imechagua pia kufanya mipango ya mkataba kwasababu Hamas imethibitisha kuwa itaendelea kubakia mamlakani.

Unaweza pia kusoma:

Yaliyomo katika mkataba huu bado yanajadiliwa. Lakini makuzungumzo yanalenga kuitaka Hamas kushusha joto lake la maandamano ya kila wiki ya waandamanaji wanaoandama kwenye mpaka wa Gaza na Israel, na kwa ajili ya Israel kulegeza msimamo wake juu ya makubaliano yaliyofikiwa.

Muhimu kwa Hamas yenye ambayo haina pesa, msada wa pesa wa kila mwezi kutoka Qatar umeidhinishwa. Kwa upande wa jeshi la Israel, inaangalia namna ya kuimarisha hali ya usalama katika eneo la Kusini mwa Israeli ili iweze kuelekeza juhudi zake katika kile inachokiona kama tisho kubwa zaidi kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Lebanon la Hezbollah upande wa kaskazini.

Kwa hivyo Israel na Hamas labda walikuwa na maslahi ya pamoja "yasiyo ya moja kwa moja "ya kuona mwisho wa kamanda wa Jihad cha Kiislamu anasema Mukhaimer Abu Saada,Mhadhili wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar University Gaza.

"Sio rahisi kwambu kama Mpalestina kusema kulikuwa na maslahi ya pamoja baina ya Hamas na Israel katika mauaji ya Baha Abu al-Ata," aliiambia BBC, "lakini ngoja niseme kwamba Hamas haikufurahia tabia zake: Alikuwa muhusika wa matukio mengi ya ukiukaji wa makubaliano ya usitishaji mapigano na Israeli kwa kuanzisha mashambulio ya roketi dhidi ya miji na vijiji vya Israel vilivyopo karibu na Ukanda wa Gaza."

Mpalestina ameketi kando ya shimo lililosababishwa na shambulio la anga la Israeli eneo la Deir al-Balah, Gaza (14/11/19)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mpalestina ameketi kando ya shimo lililosababishwa na shambulio la anga la Israeli eneo la Deir al-Balah, Gaza (14/11/19)

Ni muda tu

Licha ya hayo, Hamas ilikuw akatika msimamo unaoweza kuyumba . Uamuzi wake wa kujitenga na mzozo kulisababisha hasira kwa baadhi ya watu- hususan baada ya watu wanane wa familia moja, wakiwemo watoto kuuawa katika shambulio la ndege za Israeli - na kusababisha hali ya taharuki baina yao na wapiganaji wa kiislamu wa Jihad.

Kundi liliripotiwa wakati mmoja kutishia kujiondoa katika chumba cha harakati za pamoja. Na mashambulio ya mara kwa mara ya roketi za moto yaliyoendelea baada ya makubaliano yaliyofikiwa chini ya upatanishi wa Misri kumaliza mapigano.

Basem Naim alipuuza tofauti baina makundi mawili. Alisisitiza kuwa Hamas haijatelekeza majukumu yake ya kuweka upinzani dhidi ya uvamizi wa Israel, kundi ambalo Israel na mataifa mengi ya magharibi yanaliita kundi la ugaidi.

"Labda tulizingatia misingi ya maslahi yetu, wakati mwingine tuliamua kuahirisha au kupunguza mashambulio yetu dhidi ya ndege za Israel, lakini hilo halimaanishi kuwa hatuna haki ya kuendelea na mapambano yetu ,"alisema. "Si jukumu letu kufany akazi kama kikosi cha polisi kwa ajili ya uvamizi, na kama tumeamua ndani ya kikundi kusitisha mashambulio, hili linakua na misingi ya mazungumzo ya Wapalestina na sio jibu la matakwa ya Israeli au mipango."

Kwamujibu wa maoni katika gazeti la Israeli la Yedioth Ahronoth idara za usalama zinaamini kuwa zimeboresha fursa za kufikiwa kwa mipango ya mkataba na Hamas na wanatarajia wanasiasa wabadili "mafanikio madogo ya mapigano "kuwa mafanikio ya kidiplomasia.

Kwa mtizamo wa Hamas, anasema Mukhaimer Abu Saada, hilo linategemea ikiwa Israeli italegeza vikwazo vyake.

"Kama Israeli itarahisisha hali ya maisha ya kila siku katika Gaza ninaweza kukuhakikishia Hamas wataendelea kusitisha mapigano ,"anasema. "Lakini kama hali haitaboreka, ni muda tu na hali itakua mbaya tena."