Kili Challenge: Msanii Diamond Platinumz arudia njiani

Wasanii wa Tanzania

Chanzo cha picha, The Citizen

Muda wa kusoma: Dakika 2

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu Diamond Platinumz ni mmoja wa wasanii walioshiriki kampeini ya kupanda mlima Kilimanjaro mwaka huu lakini hakufanikiwa kufika kileleni.

Licha ya hatua ya msanii huyo kuangaziwa pakubwa katika mitandao ya kijamii alirudi baada ya kufika kituo cha kwanza.

Kampeini hiyo ambayo imekua ikihamasisha baadhi ya raia kutoka nchini Tanzania, wasanii, viongozi mbali mbali na hata raia wa kawaida kujitokeza kuenda kupanda mlima kilimanjaro imekua ikiendelea kwa wiki moja sasa.

Kampeini hiyo ilikua ikiendeshwa chini ya Waziri wa Mali asili na Utalii Daktari Hamisi Kigwangala ikiwa na kauli mbiu ya Tukutane Kileleni.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Diamond alielezea sababu tofauti zilizomfanya avunje safari yake ikiwa ni pamoja na tamasha la wikendi la Arusha.

Baadhi ya wasanii kutoka nchini Tanzania akiwemo balozi wa Utalii Miss Tanzania Queen Elizerbeth walifanikiwa kupanda mlima huo kwa wakati wake wakiandamana na waziri Kigwangala.

Wasanii wa filamu za Bongo movie Steve Nyerere na Steve Jacobs pia waliojitoa kituo cha kwanza kuelekea kupanda mlima Kilimanjaro.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Msanii huyo alionekana akiwa na maumivu makali kabla ya kujiondoa katika kampeini hiyo kwa kutokana na kuchoka.

Wasanii hao walikuwa sehemu ya watu zaidi ya 130 walishiriki kampeni ya Kili Challenge, Twenzetu Kileleni iliyoandaliwa na Waziri wa Mali asili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangala.

Kampeini ya kupanda mlima Kilimanjaro imekuwa ikipewa maudhui tofauti yote kwa ajili ya kuhamasisha Watnzania masuala kadhaa ya kijamii.

Ripoti za hivi punde zinaashiria kuwa Tanzania imeorodheshwa taifa la 10 miongoni ma mataifa ya Afrika ambayo sekta yake ya Utalii inaendelea kukua kwa kasi.

Licha ya kuwa na madhari ya kuvutia imekua ikiorodheshwa nyuma ya mataifa kama vile Mauritius, Ushelisheli, Namibia, Kenya, Ethiopia na Botswana.

Kili Challenge ni mfuko ambao umeendelea kukusanya fedha nyingi kwa miaka yote, fedha ambazo zimetumika kusaidia maeneo mbalimbali na makundi ya Wajane, Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI, Watoto yatima, Vijana, pamoja na Taasisi zinazotoa huduma muhimu za UKIMWI nchini.