Polisi watawanya maandamano ya wazazi Bukavu Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ya kushinikiza kusitishwa mgomo wa walimu

wazazi Bukavu

Mamia ya wakaazi wa mji wa Bukavu wameandana na kuzingira makanisa ya kikatoliki kupinga hatua ya shule za kikatoloki kuomba ada za shule kwa wazazi na kushinikiza walimu wasitishe mgomo.

Waandamanaji wenye hasira wameyavamia majengo ya ma parokia za kikatoliki na kanisa za ki protestanti kuwataka makasisi kutoa wito kwa walimu wa shule kurudi madarasani ili kuwafunza watoto ambao wamesalia nje bila kusoma kutokana na mgomo wa walimu wanaodai malipo yao kutoka kwa serikali.

Katika kanisa kuu la kikatoliki mjini Bukavu maarufu kama Notre Dame, wazazi hao walichoma matairi mlangoni.

Kadhalika hali kama hiyo ilishuhudiwa kwenye parokia ya Cimpunda wilayani Nguba na sehemu nyingine za mji wa Bukavu.

Waandamanaji walibeba mabango yaliokuwa na ujumbe wa kuwataka waalimu warudi shuleni."Hakutakuwa na misa katika makanisa yote ya Kikatoliki na ya Kiprotestanti hadi shule zifunguliwe na kuanza kufunza watoto" Shamari Felix amemuarifu mwandishi wa BBC Byobe Malenga.

Katika kanisa kuu la kikatoliki mjini Bukavu maarufu kama Notre Dame, wazazi hao walichoma matairi mlangoni.
Maelezo ya picha, Katika kanisa kuu la kikatoliki mjini Bukavu maarufu kama Notre Dame, wazazi hao walichoma matairi mlangoni.

Hatahivyo kuna sehemu ya ambao hawakufurahishwa kwa mgomo huo akiwemo Bisafi Bitondo anayesema amekerwa na hatua hio akieleza kwamba 'haifai kuharibu ibada ya Mungu'.

Hali ilitulia kidogo wakati maafisa wa polisi walipo tawanywa katika sehemu hizo na kuutawanya umati wa waandamanaji wa kutumia gesi ya kutoa machozi.

Walimu nchini humo wanataka utekelezaji wa mkataba wa Bibwa, ambao unaeleza kuwa mwalimu wa elimu ya wastani anastahili kupata mshahara wa dola za Marekani 300 kwa mwezi.

Wanafunzi darasani Kinshasa

Mkataba wa Bibwa, ni mkataba kati ya serekali na muungano wa waalimu nchini DRC unaozungumzia mishahara wanayostahili kulipwa walimu nchini kulingana na kiwango cha elimu walio nayo.

Mwalimu wa elimu ya chini, anastahili kulipwa dola 300.

Changamoto ya elimu ya bure

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeidhinisha elimu ya bure katika shule za msingi za umma kwa lengo la kutekeleza yaliomo katika katiba ya mwaka 2005, ambao inasisitiza elimu ya bure kwa watoto wa shule za msingi.

Tangu mwaka 1993, wazazi wamekuwa wakilipa walimu ada ya mafunzo na hivi sasa serikali imeamua kuwalipa mishara.

Lakini baadhi ya walimu mpaka sasa wana shaka kuhusu utekelezaji wa hatua hiyo mpya ya serikali.

Walimu walitishia kuanza mgomo ikifika tarehe ishirini Septemba ikiwa serikali haitawalipa mshahara wa kutosha.

'Amechukuwa (Felix Tshisekedi) hatua hio ya kusema wazazi wasilete tena pesa, sisi tumemunga mkono, hapa kwani nina walimu ambao hawajawahi kupokea pesa kutoka kwa serkali, nadhani ni muhimu kulipa walimu ,kama walimu hawatalipwa haraka, itakuwa athari sana' amesema Moju.

Gharama ya elimu ya bure kwa watoto wa shule ya msinigi ni kama 40% ya bajeti ya nchi ambayo ni ya dola za Marekani karibu bilioni sita.

Wachambuzi wa uchumi wamekuwa na shaka iwapo hatua hio ya serikali itafanikiwa lakini rais Felix Tshisekedi ana matumaini mengi.

"Itakuwa hatua ambayo itakamilishwa katika miezi michache ijayo. "Mpango huu tumeukuta lakini hakukuwa na bajeti. Hili ndilo nitakalolipa kipaumbele. Congo ina uwezo wa kuongeza mshahara kugharamia elimu na tutalipa" alisema rais Felix tshisekedi.

Congo inafuata mifano ya mataifa mengine katika eneo la Afrika mashariki kama Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi katika kutoa elimu ya bure katika shule za msingi ambazo licha ya dhamira yake nzuri, imekabiliwa na changamoto si haba katika utekelezaji wake tangu kuidhinishwa katika vipindi tofuati.