Mlimbwende wa Uskochi ambaye taaluma yake iliimarika akiwa na miaka 60

Gillean McLeod

Chanzo cha picha, Gillean McLeod

Maelezo ya picha, Gillean alipiga picha ya kwanza kama mlimbwende katika miaka yake ya 50

Gillean McLeod alipiga picha ya kwanza kama mlimbwende baada ya kutimiza miaka 50 na safari yake ilianza ilianza rasmi baada ya kupiga picha akiwa amevalia vazi la kuogelea akiwa na miaka 60.

Picha hiyo iliyokua sura ya tangazo la kibiasha la H&M inamuonesha Gillean akiwa amevalia vazi la kuogelea bila kupaka vipodozi vya aina yoyote huku nywele zake nyeupe zikiwa na uonekano asilia.

Wauzaji wa vazi hilo la kuogelea walipoiweka picha hiyo katika mtandao wa Instagram ilipata maelfu ya likes kuashiria jinsi ilivyowavutia wafuatiliaji wa mtandao huo.

Vazi la kuogelea la Gillean lilioongoza kampeini ya H&M lilimpata umaarufu

Chanzo cha picha, Gillean McLeod

Maelezo ya picha, Vazi la kuogelea la Gillean lilioongoza kampeini ya H&M lilimpata umaarufu
Presentational white space

Tangu Gillean alipoanza taaluma ya ulimbwende ameshiriki kampeini kadhaa ikiwa ni pamoja Boots the chemist, vazi la jeans aina ya Levi na bidha za urembo wa nywele za Schwarzkopf .

Kabla ya kuamua kusimama mbele ya kamera, Gillean alifanya kazi kwa miaka minga kama mrembuaji.

Rafiki yake ambaye pia ni mpiga picha ndiye aliyemshawishi kupiga picha za kwanza za kitaalamu kama modo.

uda mfupi baadae picha hizo ziliwavutia maajenti wa ulimbwende, na japo aliitiwa kazi mara kadhaa alikataa kufanya baadhi ya kazi hizo.

Ni picha aliyopiga mwaka 2016 akiwa amevalia vazi la kuogelea iliyobadilisha kila kitu, anasema, Gillean mwenye umri wa miaka 63.

Modo huyo raia wa Uskochi alizaliwa nchini Indonesia. Baba yake alikua Mskochi na mzazi Mmarekani.

gillean mcleod

Chanzo cha picha, Gillean McLeod

Maelezo ya picha, Gillean anasema mamodo walio na umri mkubwa wanatumiwa zaidi

Alilelewa Borneo, na alikua akisafiri kwa ndege kwenda kusoma Penang mjini Malaysia hadi alipojiunga na shule ya upili nchini Uskochi.

"Napenda sana Borneo kwa sababu nilifuraihia mahali tulipoishi,"aliiambia BBC.

Japo alisomea St Andrews, alirejea Borneo akiwa na miaka 17 wazazi wake walipohamia Scotland.

Gillean anasema alipokua mdogo hakujichukulia kuwa mrembo.

Gillean mcleod

Chanzo cha picha, Gillean mcleod

Maelezo ya picha, Gillean anasema hakujihisi kuwa mrembo alipokua mtoto mdogo, alijiona mrefu mwembamba
Presentational white space

"Nilipotimiza umri wa kubaleghe akiwa shule ya upili nchini Scotland alipatwa na chunusi usoni, hali iliyomfanya kuwa na haya ni kujiangazia sana muonekano wake."

Katika miaka yake ya20, Gillean alihamia mjini London na licha ya kuwa, alipendekezewa suala la kuwa modo, hakuwa na ujasiri wa kujitosa katika fani hiyo.

Lakini baada ya kuishi mjini Los Angeles kwa miongo kadhaa hatimae alishawishika kupiga picha za kitaalam.

"Si kuwa na uhakika wa kupiga picha hizo kwa sababu nilikua mhaya san hasa kusimama mbele ya kamera," anasema. "Lakini niliweza"

Anasema: "Nilipata kazi mara kadha hadi nilipotimiza miaka 60 na baada ya hapo nilifanya tangazo la vazi la kuogelea ambalo liliwavutia wtu wengi."

Gillean kwa sasa ameimarika katika taaluma ya umodo, hivi karibuni amefanya kazi Ujerumani, New York na Los Angeles.

Kampeini yake ya Oliver People ilimwezesha kuwekwa kwenye mabango ya matangazo mjini New York katika ukumbi wa Times Square, ambayo Gillean alisafiri kwenda kujionea picha yake mwenyewe.

Gillean akiwa Times Square nyuma yake kuna bao la matangazo aliofanya

Chanzo cha picha, Gillean McLeod

Maelezo ya picha, Gillean akiwa Times Square nyuma yake kuna bao la matangazo aliofanya
Presentational white space

Gillean anawashauri wasichana wadogo wanaotumia mtando wa Instagram na majarida ya urembo kuwa picha wanazoona haziangazii uhalisia wa maisha.

Aneama picha hizo zinapigwa na wataalamu ambao wanatumia mwanzaza mzuri na kwamba picha hizo mara nyingi zinafanyiwa marekebisho kadhaa kabla ya kutolewa.

"Lazima ujiamini na kula vyakula vilivyo na virutubisho ili uwe na afya nzuri," anasema.

Kwa mujibu wa Gillean, kwa sasa wanawake wengi walio na umri mkubwa wanatumiwa kama mamodo.

"Sidhani ni mimi nilieanza kufanya hivyo lakini tangazo la H&M nililoshiriki liliwafanya watu wengi kubaini jinsi wanawake wanavyoweza kuwa na muonekano mzuri wakiwa na na ika 50 hadi 60," alisema.

"Nafanya kazi na shirika moja jini New York ambalo wafanyikazi wake karibu wote wana umri wa zaidi ya miaka 60 na muonekano wao ni wa kuvutia."