Mwili watumika kujaribia vilipuzi bila idhini ya familia

Picha inayoonyesha mifumo ya kibinaadamu

Chanzo cha picha, Getty Images

Mtu ambaye alitoa mwili wa mama yake kwa kile alidhani ni utafiti wa kisayansi kuhusu ugonjwa Alzheimer (unaosababisha kupoteza kumbukumbu) baadaye alibaini kuwa mwili huo ulitumika kujaribia vilipuzi. Kwa hivyo ni nini kinachotokea wakati mwili wako umetolewa kwa ajili ya utafiti wa sayansi ya tiba?

Wiki iliyopita maelezo mapya ya kesi ya mashtaka yalitokea dhidi ya Kituo cha Rasilimali za Biolojia huko Arizona, baada ya shambulio la FBI mnamo 2014 ambapo mabaki ya mamia ya sehemu za mwili zilizopotea yaligunduliwa.

Kituo hicho, ambacho sasa kimefungwa, kinatuhumiwa kuuza kinyume cha sheria miili iliyotolewa kwa utafiti wa kisayansi bila matakwa ya wafadhili wenyewe.

Nyaraka mpya za korti zilizotolewa hivi karibuni zilionyesha kuwa familia za wale ambao miili yao ilikuwa imetolewa walisema wanaamini mabaki ya jamaa zao yatatumika kwa utafiti wa matibabu na kisayansi.

Jim Stauffer ni mmojawa washtakiwa wengi anayekishtaki kituo hicho. Alikiambia kituo cha Phoenix ABC 15 anaamini mwili wa mama yake uliyotolewa utatumika kutafiti ugonjwa wa Alzheimer's, ugonjwa ambao alikuwa nao, lakini baadaye akagundua kuwa ulitumiwa na jeshi kuchunguza athari za milipuko.

Anasema kwenye makaratasi aliyopewa na kituo hicho. aliulizwa kama yuko tayari mwili wa mama yake utumiwe kwenye majaribio ya vilipuzi na akaweka alama kwenye neno "hapana" .

Kwa hivyo biashara ya uchangiaji wa mwili iko vipi huko nchini Marekani, na watu wanatarajia nini?

Kwa nini utaratibu wa kutoa mwili kwa ajili ya utafiti haudhibitiwi Marekani?

Wakati kujitolea kwa viungo vya mwili vikidhibitiwa na Idara ya Afya na Huduma za Binadamu ya Mariekani, kujitolea mwili bado hakujasajiliwa.

Kununua na kuuza miili ni msaada lakini kinachoruhusiwa ni kutoza kiasi cha pesa kwa ajili ya gharama kuushughulikia mwili kunakohusisha kuondolewa, kuhifadhi ,usafirishaji au kuuharibu.

Wala hakuna usajili wowote wa kitaifa au wa kimataifa wa kufuatilia ni miili mingapi inayotolewa kwa utafiti wa matibabu kila mwaka.

Lakini inakadiriwa maelfu ya watu nchini Marekani hutoa miili kwa ajili ya shughuli za masomo na utafiti, wakiamini matendo yao ni ya hisani na miili itatumika kwa sayansi ya matibabu.

Madaktari wakiwa chumba cha upasuaji

Chanzo cha picha, Getty Images

Vituo vya kutoa michango ya mwili kwa vyuo vikuu vitatumia zaidi miili kufundisha wanafunzi wa sayansi ya tiba. Taasisi nyingi, kama Chuo Kikuu cha California, zimejitolea kufanya kazi kwa uwazi.

Wengine kama Chuo Kikuu cha Utafiti cha Tennessee, kinachojulikana kama "Shamba la Mwili", hufanya shughuli maalum zaidi, kama kufundisha timu za ujasusi jinsi miili inavyooza.

Brandi Schmitt, mkurugenzi mtendaji wa huduma za anatomiki katika Chuo Kikuu cha California, aliiambia BBC kwamba kile kinachotokea kwa mwili uliotolewa hutegemea aina ya kituo mwili unapokwenda.

"Mtu yeyote anayezingatia mchango wa mwili kwa ajili ya elimu na utafiti anapaswa kuhakikisha kuwa wanajua madhumuni ya mashirika ambayo wanachangia, iwe ni taasisi ya elimu, bodi ya anatomia ya serikali, kampuni ya kibinafsi, na kadhalika na kadhalika na hutoa zawadi zao kwa ajili ya msaada gani. "

Bi Schmitt anasema kanuni za sasa hazitoshi kulinda wafadhili na wale wanaofanya kazi katika sayansi ya matibabu.

Daktari akitazama kwenye darubini

Chanzo cha picha, Getty Images

"Sheria ya kujitolea ya ''The Uniform Anatomical Gift Act (UAGA) iliandikwa na Tume ya Sheria ya pamoja na ni sheria ya serikali inayoweza kurekebishwa na serikali [ya California].

"Inasimamia jinsi ya kufanya na ni nani anayeweza kutengeneza, kurekebisha na kubatilisha zawadi ya anatomiki na aina ya matumizi ya zawadi, kama vile kupandikiza na tiba ya kliniki na elimu na utafiti.

"Haizungumzii utafutaji wa ridhaa, matumizi maalum, uhamishaji, ufuatiliaji, huduma nyingi za mfano wa mwisho au mfano wa faida."

Bi Schmitt anasema "kanuni ya ziada" ni muafaka kwa muda mrefu.

"Ukosefu wa kanuni mahususi na utofauti umesababisha kuwepo na dhuluma mbaya kwa wafadhili au kufanya dhamira ya familia ya kuleta athari chanya kupitia zawadi yao isitimie.

Mbali na UAGA, pia kuna miongozo mingine kuhusu namna miili inapaswa kushughulikiwa baada ya uchangiaji, kama vile kutoka kwa Chama cha wana anga wa Marekani.

Inasema: "Programu za Mchango wa Mwili zinapaswa kuelezea wazi matumizi ya miili kwani inahusu mahitaji ya kitaasisi na ya kielimu."

Kituo cha Utafiti wa Biolojia huko Arizona hakikufikiria kuhusu kibali na pia ilifanywa kama biashara ya faida. Ilitoa huduma ya usafirishaji wa bure kuchukua miili na uchomaji wa bure, na kuifanya ifurahishe familia zenye mapato ya chini.

Mmiliki wake Stephen Gore alikutwa na hatia mnamo 2015 lakini aliwekwa kwenye uangalizi. Familia kadhaa sasa zinamshtaki yeye na kampuni hiyo kwa kutumia miili vibaya bila kufuata ahadi zilizowekwa kwenye fomu za idhini.

"Watu wanaofikiria kutoa mchango wa mwili huwa na dhamira zao , hivyo ni vibaya kuharibu dhamira zao kwa kutenda kinyume cha makubaliano''.Bi Schmitt alisema.