Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maandamano ya Georgia: Maelfu wavamia bunge baada ya mbunge wa Urusi kuhutubia
Watu wapatao 240 wamejeruhiwa katika makabiliano wakati waandamanaji walipojaribu kuvamia bunge la Georgia baada ya mbunge wa Urusi kukalia kiti cha Spika katika bunge la Georgia.
Polisi wa kutuliza ghasia waliwazuwia kuingia ndani ya jengo la bunge , kwa kutumia gesi za kutoa machozi na risasi bandia.
Ghadhabu ililipuka pale mbunge Sergei Gavrilov alipohutubia kongamano la Wabunge kutoka nchi za Wakristo wa thehebu la Orthodox .
Hali ya uhasama baina ya Georgiana Urusi iliibuka miaka , 11 baada ya nchi hizo mbili kuingia vitani kufuatia kujitenga kwa jimbo la Ossetia kusini.
Zidi ya watu 100 bado wanaendela kupata matibabu hospitalini saa kadhaa baada ya makabiliano yaliyotokea Ijumaa , wanasema maafisa wa Georgia . Miongoni mwa watu 240 waliojeruhiwa , 80 ni polisi wamesema.
Daktari ameviambia vyombo vya habari vya eorgia kuwa watu wawili wamepoteza uwezo wa kuona.
Rais wa Georgia Salome Zourabichvili camelaani kitendo cha mbunge wa Urusi Bwana Gavrilov' na kukitaja kama "uhalifu mkubwa" na ametoa wito wa kurejea kwa hali ya utulivu.
Bwana Gavrilov amelaumu "taarifa gushi " kuwa ndio chanzo cha ghasia ambapo anasema taarifa hizo zilisema kulikuwa na mapigano dhidi ya Georgia miaka ya 1990.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi ameushutumu upinzani nchini Georgia kwa kujaribu kuzuwia kuboreka kwa mahusiano baina ya pande mbili.
Ni nini kilichosababisha maandamano?
Bwana Gavrilov alikuwa anahudhuria kongamano la wabunge kutoka nchi zenye Wakristo wa Orthodoxy (IAO), lililoanzishwa na bunge la Ugiriki mwaka 1993 kwa ajili ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya wabunge wakristo wa dhehebu la Orthodox .
Mbunge wa upinzani wa bunge la Georgia akaitisha maandamano ya kupinga uamuzi wake wa kutoa hotuba akiwa katika kiti cha spika.
Aliwahutubia wajumbe wa Urusi, na kuwaudhi wanasiasa na raia wa Georgia kwa ujumla walipinga kuwepo kwa wawakilishi wa Moscow nchini mwao.
Wakitoa wito kwa spika Irakli Kobakhidze, kujiuzulu na amaafisa wengine , waandamanaji wapatao 10,000 walivunja uzio wa polisi katika mji mkuu, Tbilisi, limeripoti shirika la AFP.
Ndani ya bunge, wabunge wa upinzani waliweka uzio kwenye eneo la jukwaa anapoketi spika na kumtaka yeye, waziri wa mambo ya ndani na mkuu wa usalama wa taifa wajiuzuru kutokana na tukio hilo.
Kikao kiliahirishwa na Bwana Gavrilov ameripotiwa kuikimbia nchi.
" Lile lilikuwa ni sawa na kofi kwenye uso wa historia ya hivi karibuni ya Georgia ,"Amesema Elene Khoshtaria, mbunge wa upinzani katika bunge la Georgia .
Ni kwa nini kuna chuki baina ya Georgia na Urusi?
Wakati Georgia ilipotangaza uhuru wake kutoka kwa Muungano wa Usovieti mnamo mwaka 1991, makundi ya wanaotaka kujitenga yaliibuka katika majimbo ya Abkhazia na Ossetia Kusini.
Mwezi Agosti 2008, Georgia ilijaribu kunyakua tena jimbo la Ossetia Kusini , ambalo ililipigania katika vita vya kutaka kujitenga vya miaka ya 1990.
Urusi ilimwaga majeshi yake ndani, na kuvifurusha vikozi vya Georgia kutoka Ossetia Kusini na Abkhazia.
Kufuatia sitishaji mapigano , Urusi iliondo wanajeshi wake wengi kutoka katika ameneo yanayozozaniwaya Georgia lakini bado ina wanajeshi wake katika majimbo ya Ossetia Kusini na Abkhazia, ikiyatambua yote kuwa majimbo ''huru "
Tangu wakati huo uhusiano baina ya Urusi na Georgia haujawa mzuri.