Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Urusi yaendeleza mashambulizi ya ndege Aleppo
Ndege za mashambulizi za Urusi zimetekeleza shambulio kubwa katika maeneo yaliyoshikiliwa na waasi mjini Aleppo.
Takribani watu 12 wameuawa na kusababisha uharibifu katika maeneo mbalimbali.
Wiki iliyopita serikali ya Syria ilisema kuwa mashambulizi ya ndege yatapunguzwa ili kuleta unafuu katika wiki mbili za kampeni ya anga ambapo maelfu ya watu wamekufa na huduma za afya kuharibiwa.
Hayo yamefuata baada ya kuvunjika kwa usitishwaji wa mapigano ulioandaliwa na Urusi na Marekani.