Andy Ruiz Junior sasa ndio bingwa mpya wa ndondi duniani baada ya kumlambisha sakafu Anthony Joshua

Anthony Joshua baada ya kurambishwa sakafu na Andy Ruiz

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Bondia wa uzani mzito Andy Ruiz Jr ameushangaza ulimwengu kwa kumshinda bingwa wa ndondi katika uzani huo Anthony Joshua.

Joshua ambaye amepigiwa upatu kumrithi bingwa wa zamani katika uzani huo Mohamed Ali aliangushwa mara nne kabla ya refa kuingilia kati na kusitisha pigano hilo kunako raundi ya saba.

Andy Ruiz Jr aliushangaza ulimwengu katika historia ya ndondi na kufanikiwa kushinda mataji ya IBF, WBO na WBA yaliokuwa yakimilikwa na Anthony Joshua.

Katika pigano lililovutia wengi katika ukumbi maarufu wa ndondi nchini Marekani Mew York Madison Square Garden , Ruiz alionekana yupo vizuri zaidi ya Joshua toka awali kwa kumzidi nguvu na maarifa.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Joshua alipigiwa upatu kushinda pigano hilo na wengi kwa urahisi huku wachanganuzi wakifananisha kilichompata bondia huyo sawa na waliyoyapitia mabingwa wa zamani Lennox Lewis na Mike Tyson ambao pia waliwahi kupigwa na wapinzani ambao hawakupigiwa upatu na kuzua mshangao mkubwa kwenye ulimwengu wa masumbwi.

Tyson alitandikwa na James 'Buster' Douglas mwaka 1990, na Lewis alichapwa na Hasim Rahman mwaka 2001.

Sio Joshua anayejulikana na Uingereza

Na haikuwa bahati mbaya kwa Joshua kwani alikuwa amepigwa kutoka raundi za kwanza alipomuangusha Ruiz.

Na baada ya kupigwa ngumi kali ya kushoto , Joshua aliangukia kamba za ukumbi wa ndondi .

Na kabla ya kukamilika kwa dakika tatu za raundi hiyo aliangushwa tena bada ya Ruiz kumshambulia kwa mchanganyiko wa makonde .

Hatua hiyo iliwashangaza wengi katika ukumbi wa Madison Square Garden,

Bingwa mpya wa ndondi katika uzani mzito duniani Andy Ruiz akimsubiri Joshua kusimama baada ya kumrambisha sakafu mara nne

Chanzo cha picha, Getty Images

Je ni nini kilichotokea?

Joshua haamini kilichompata baada ya kushindwa na Andy Ruiz

Chanzo cha picha, Reuters

Ruiz alishirikishwa katika pigano hilo baada ya raia wa Marekani Jarell Miller kupatikana na dawa za kusisimua misuli wiki sita tu kabla ya pigano hilo.

Na ilipofikia raundi ya saba , wakati Joshua alipoangushwa mechi hiyo ilikuwa imekwisha baada ya kupigwa ngumi nyingi zilizomchanganya na kulazimika kutema kifaa kinacholinda meno.

Hakuwa nacho mdomoni na refa alipoona Joshua kachanganyikiwa aliingilia kati na kusitisha pigano.

Ruiz alionekana hafifu sana kuweza kumshinda bingwa huyo wa ndondi sio tu kwa maneno bali hata kwa maungo.

Waingereza watakapoamka siku ya Jumapili alfajiri watashangazwa na matokeo haya.

Pigano la marudio kabla ya mwisho wa mwaka

Joshua alikuwa ameshindwa katika raundi mbili akishinda moja wakati alipopigwa knockout lakini atapata fursa ya kujirekebisha katika mechi ya marudio jijini London , kabla ya mwezi Disemba kulingana na promota Eddie Hearn.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Ruka X ujumbe, 3

Mwisho wa X ujumbe, 3

Ruka X ujumbe, 4

Mwisho wa X ujumbe, 4

Kwa sasa mazungumzo yoyote ya kuzipiga dhidi ya Tyson Furry ama hata Deontay Wilder yamesitishwa.

Ruiz ambaye kwa sasa ameshinda mara 33 na kupoteza mara moja aliruka ruka katika ukumbi wa ndondi wa Madison Square Garden baada ya refa kusitisha pigano hilo.

Ruiz hatahivyo alionyesha uwezo mkubwa katika pigano hilo ikimaanisha kwamba Joshua atakuwa na kazi ya ziada kumshinda katika pigano hilo linalotarajiwa kwa hamu kufanyika kabla ya mwaka kukamilika mjini London.