Uchaguzi India 2019: Jinsi Narendra Modi alivyobadilisha siasa nchini India

Narendra Modi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Raia wengi wa India wanaamini Bw. Modi ni masia ambaye atatatua shida zao zote

Narendra Modi ameshinda uchaguzi mkuu wa India na kujipatia muhula wa pili wa miaka mitano madarakani.

BBC inaangazia baadhi ya masuala yaliyo mpatia umaarufu mkubwa kiongozi huyo anaaminiwa kuwa mtu maarufu sana nchini India.

Bw. Modi alitmia uchaguzi huo kama nafasi yake ya kujieleza kwa makini.

Huenda angelikabiliwa na changamoto ya upinzani dhidi ya kiongozi anayegombea muhula wa pili lakini aligeuza dhana hiyo kabisa

Ongezeko la ukosefu wa ajira limefikia kiwango cha juu, mapato yanayotokana na kilimu yamepungua na uzalishaji wa viwanda pia umedorora.

Narendra Modi ameibuka kuwa kiongozi maarufu zaidi nchini India.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Narendra Modi ameibuka kuwa kiongozi maarufu sana nchini India.

Ushindi huu wa pili zaidi ulimhusu Narendra Modi

Raia wengi wa India waliathiriwa na sera yake ya kupiga marufuku baadhi ya sarafu za nchi hiyo ili kukabiliana na watu ambao hawakutangaza mali yao

Wakosoaji wake walisema mpango huo haukutekelezwa vizuri na kwamba uliwaathiri vibaya wafanyibiashara wa ndani na wa nje.

Hata hivyo matokeo ya Uchaguzi ulidhihirisha kuwa watu hawakumlaumu Modi kwa hatua hiyo.

Wakati wa kampeini yake aliwambia wafuasi wake kuwa anahitaji zaidi ya miaka mitano kurekebisha uharibifu uliyofanywa kwa ''miaka 60''.

Wapiga kura walikubali kumpatia muda kufanya hivyo.Raia wengi wa India wanaamini kuwa Bw. Modi ni sawa na mkombozi ambayea atasuluhisha matatizo yao yote.

Chini ya utawala wa Bw. Modi chama cha BJP kimepata umaarufu mkubwa katika siasa za India

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Chini ya utawala wa Bw. Modi chama cha BJP kimepata umaarufu mkubwa katika siasa za India

Utafiti uliyofanywa na Kituo cha masuala ya maendeleo ya kijami (CSDS), kilicho na makao yake mjini Delhi ulibaini kuwa thuluthi tatu ya wapiga kura wa BJP wangeliuunga mkono chama kingine ikiwa Modi hangekuwa mgombea wa kiti cha waziri mkuu.

"Hii inaashiria kuwa kura nyingi zilikuwa za Bw. Modi, kuliko za BJP. uchaguzi huu zaidi ulikuwa kuhusu uongozi wa Modi kuliko kitu kingine chochote," alisema Milan Vaishnav, mtaalamu wa masuala ya usalama kutoka chuo Kikuu cha Washington,

Mchanganyiko wa maendeleo na utaifa ulimsaidia Modi

Miradi ya maendeleo ya kijamii iliyolenga kukomesha tofauti za kidini nchini India ilimsaidia Waziri Mkuu Narendra Modi kushinda uchaguzi mkuu.

Japo kampeini ilisababisha mgawanyiko mkali Bw. Modi alifanikiwa kuimarisha uzalendo na maendeleo.

Aliangazia zaidi masuala yaliyotofautisha utaifa na uadui huku akiangazia zaidi umuhimu wa kuchagua viongozi wanaofikia kigezo hicho.

Modi mwenyewe ameonesha uwezo wake wa kulinda nchi katika muhula wake wa kwanza madarakani.

This combination of pictures taken and created on April 18, 2019 shows Indian voters showing their ink-marked fingers after casting their vote during the second phase of the mammoth Indian elections at various polling stations across India. -

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Zaidi ya 65% ya wapiga kura milioni 900 walishiriki uchaguzi huo

Ushindi wa Modi unaashiria mabadiliko makubwa katika siasa za India

Umaarufu wa Modi umeimarika zaidi kiasi haliambayo ilimfanya kuwa nembo ya matumaini kwa watu wengi.

Chini ya uongozi wake mshauri wake mkuu Amit Shah amethibitisha kuwa, chama cha BJP kimeimarika kuliko vile ilivyokuwa.

"BJP imepanuka na kupata uungwaji mkono kitaifa," anasema Mahesh Rangarajan.

Chama hicho kilijulikana kuwa na wafuasi wakuwa na wafuasi katika jamii ya watu wanaozungumza kihindi katika jimbo la Kaskazini lakini china ya uongozi wa Modi chama hicho kilishirikiana na vyama vingine katika hatua mabayo iliiongezea umaarufu.

Narendra Modi

Chanzo cha picha, Reuters

Baadhi ya wachambuzi wanahofia kuwa chini ya uongozi wa Bw. Modi India huenda ikaelekea katika siasa ya democrasia inayoegemea misingi wa kijamii amabo utahitaji kuleta pamoja jamii iliyo na kabila kubwa lakini wengine wao wanasma hoja hiyo haina msingi wowote.

Je utaifa wa unaotegemea dhehebu ya Kihindu utakuawa mfumo wa siasa za India?

Hilo haliwezekani kwasababu India - inajivunia mshikamano wa kitaifa pamoja na mchanganyiko wa madhehebu tofauti.

Demokrasia ni sehemu tu ya gundi inayoimarisha umoja wa watu wa taifa hilo.