Afrika kwa picha wiki hii: Tarehe 26 Aprili- 2 May 2019

Baadhi ya picha zilizochukuliwa kutoka maeneo mbali mbali ya Afrika wiki hii:

Mwanamume mmoja akishiriki katika kazi ya kuukarabati msikiti wa Great Mosque wa Djenne ulioko eneo la kati la Mali Aprili 28, 2019. - maelfu kadhaa ya wakazi wa mji wa kati wa Mali wa Djenne, ambao ni eneo la turathi ya dunia ya UNESCO , walishiriki katika sherehe ya mwaka ya kuukarabati msikiti huo

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Ni kazi ya kujichafua katika Mji wa kati wa Mali Djenne siku ya Jumapili huku wajenzi wakisaidia kuukarabati msikiti wa kale wa Grand Mosque kwa tope
Presentational white space
Nasasi Belinda (katikakati), mwanamke mfanyabiashara allijawa na hisia na kutokwa na machozi alipovishwa taji la mwanamke mwenye maumbo makucrowned Miss Curvy Uganda during the first edition of Miss Curvy Uganda in Kampala, Uganda, on April 26, 2019.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Ijumaa usiku ilikuwa ni siku ya sherehe kwa mfanyabiashara mwanamke wa Uganda Nasasi Belinda ambaye alivalishwa taji la mwanamke mwenye umbo makubwa zaidi mjini Kampala Uganda
Presentational white space
Mmmoja wa washiriki aliingia jukwaani namna hii katika shindano la kwanza la mwanamke mrembo mwenye umbo kubwa zaidi - lililoitwa Miss Curvy Uganda-mjini Kampala, Uganda, Aprili 26, 2019.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mashindano yalikuwa yamepangwa kusherehekea urembo wa wanawake wa Afrika wenye maumbo makubwa ya mwili
Presentational white space
Mwanamke wa Libya akiwa amejifunika sura yake kwa bendera ya Libya wakati alipohudhuria maandamano ya kudai kumalizika kwa mashambulio ya Khalifa Haftar katika medani ya iliyopo katika kati mwa mji mkuu Tripoli, Libya Aprili 26, 2019

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, nchini Libya Ijumaa, waandamanaji wanaopinga mashambulio ya wanajeshi wa kiongozi mwenye mamlaka makubwa Khalifa Haftar waliingia mitaani katika mji mkuu Tripoli...
Presentational white space
Mpiganaji wa serikali inayotambuliwa kimataifa-Government of National Accord (GNA) akicheza mchezo wa video unaofahamika kama Battlegrounds (PUBG) kwenye simu yake wakati wa mapumziko ya vita katika ngome ya kijeshi ya Tajoura, kusini mwa mji mkuu wa Libya Tripoli Mei 1

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mpiganaji aliyekuwa akiulinda mji alichukuliwa picha na mpigapicha akicheza mchezo wa video wa vita Jumatano alipokuwa akisubiri map[ambano yanayofuata
Katika siku hiyo hiyo , waandamanaji walikuwa mitaani katika mji mkuu wa Algerian, Algiers,kwa maandamano ya Mei mosi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Katika siku hiyo hiyo , waandamanaji walikuwa mitaani katika mji mkuu wa Algerian, Algiers,kwa maandamano ya Mei mosi
Presentational white space
Wavulana wa Sudan walipokuwa wakipigwa picha ndani ya mto Nile walimokuwa wakiogelea katika siku ya Mei Mosi , 2019 katika kisiwa cha wilaya ya Tuti iliyopo mjini Khartoum

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kulikuwa na maandamano nchini Sudan pia lakini mbali na maandamano hayo katika kisiwa cha mji mkuu wa Sudan khartoum cha wiliya ya Tuti, kikundi cha wavulana kilikuwa kikifurahia mawimbi ya mto Nile.
Presentational white space
Japo kulikuwa na joto kali kwenye jangwa hili la Morocco Jumatano wiki hii, waendesha baiskeli walishiriki katika mashindano ya milima ya baiskeli Mei 1, 2019

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Japo kulikuwa na joto kali kwenye jangwa hili la Morocco Jumatano wiki hii, waendesha baiskeli walishiriki katika mashindano ya milima ya baiskeli
Presentational white space
, Agiro Cavanda akiangalia uharibifu uliosababishwa na kimbunga Kenneth kwneye nyumba yao iliyopo katika kijiji cha Wimbe Pemba, baada ya kimbunga hicho kilipiga fukwe za Msumbiji , Aprili 29, 2019

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jumatatu, Agiro Cavanda akiangalia uharibifu uliosababishwa na kimbunga Kenneth kweneye nyumba yao baada ya kimbunga hicho kilipiga fukwe za Msumbiji
Presentational white space
Wanaume wa Kinigeria husherehekea tamasha la Idju Owhurie festival la Warri, tarehe 29 Aprili 2019). Utamaduni wakufanya tamasha la Owhurie husherehekewa na watu wa ufalme wa Agbarha wa Warri, katika jimbo la Delta State. Tamasha hilo huwa kama tamasha la vita na hufahamika kwa wenyeji kama “Agbassa Juju” ambalo lilitumika katika kuchumbia mabinti tangu karne 15.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Tamasha la Idju Owhurie katika eneo la Warri, nchini Nigeria, liliwavutia mamia ya wanaume Jumatatu ambapo husherehekea kama wapiganaji waliokuwa wakitafuta wapenzi katika karne ya 15
Presentational white space

Presentational white space
Licha ya umri wake na afya yake kutatizwa na magonjwa, Askofu Mkuu wa Afrika Kusini Desmond bado anaendelea kuonyesha tabasamu hapa ni katika tukio moja mjini Cape Town Jumamosi

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Licha ya umri wake na afya yake kutatizwa na magonjwa, Askofu Mkuu wa Afrika Kusini Desmond bado anaendelea kuonyesha tabasamu hapa ni katika tukio moja mjini Cape Town Jumamosi
Presentational white space

Presentational white space

Picha na : AFP, EPA na Reuters