Afrika kwa picha wiki hii : Tarehe 5-11 Aprili 2019

Baadhi ya picha bora zlizopigwa wiki hii kutoka maeneo mbali mbali ya Afrika na nje ya bara hili:

Muandamanaji anayepinga utawala wa Sudan akimbusu askari kichwani wakati wa maandamano mjini Khartoum , Sudan - Alhamisi tarehe 11 Aprili 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muandamanaji wa Sudan akimbusu mwanajeshi siku ya Alhamisi kabla ya kutangazwa kwamba rais Omar al-Bashir amepinduliwa
Muandamanaji maarufu , Alaa Salah, ambaye amepewa jina bandia "Nubian queen", akiongea na umati wa watu mjini Khartoum siku ya Jumatano

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Siku moja kabla muandamanaji maarufu , Alaa Salah, ambaye amepewa jina bandia "Nubian queen", akiongea na umati wa watu mjini Khartoum.
Mwanamke mkongwe wa Algerian akiongea na maafisa wa usalama waliokuwa wamewazingira waandamanaji wakati wa maandamano ya kupinga utawala katika mji mkuu Algiers Aprili 10, 2019. - Waandamanaji wa Algeria walnaendelea na maandamano hadi leo dhidi ya watawala waliopo madarakanilicha ya ahadi ya kiongozi wa taifa wa mpito ya kuendesha uchaguzi wa ''wazi'' wa urais kufuatia kujiuzulu kwa kiongozi mkongwe wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Katika siku hiyo hiyo kaskazini zaidi mwa Afrika, nchini Algeria, muwandamanaji huyu alidai watawala waachie madaraka
Mwanamke wa Algeria akiwa ameshikilia bendera ya taifa karibu na vikosi vya usalama vilivyozingira waandamanaji wakati wa maandamano ya kupinga mfumo wa utawala nchini humo katika mji mkuu wa Algeria, Algiers Jumatano tarehe 10 Aprili 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanataka wale walioongoza pamoja na Abdelaziz Bouteflika, aliyejiuzulu wiki iliyopita , waandae uchaguzi ujao.
Jumapili, wanariadha wakipita kwenye shamba la maua wakati wa mbio za Rotterdam Marathon nchini Uholanzi Netherlands. Mkenya Marius Kiperem (akiwa nyuma kulia) alishinda mbio hizo, na kuweka rekodi mpya ya mbio hizo

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Jumapili, wanariadha wakipita kwenye shamba la maua wakati wa mbio za Rotterdam Marathon nchini Uholanzi Netherlands. Mkenya Marius Kiperem (akiwa nyuma kulia) alishinda mbio hizo, na kuweka rekodi mpya ya mbio hizo
Katika siku hiyo hiyo nchini Italia, Muethiopia Tebalu Zawude Heyi alishinda mbio za Rome marathon. Waethiopian , walipata medali za fedha na shaba katika mbio za wanaume na wanawake. siku ya Jumapili.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Katika siku hiyo hiyo nchini Italia, Muethiopia Tebalu Zawude Heyi alishinda mbio za Rome marathon. Waethiopian , walipata medali za fedha na shaba katika mbio za wanaume na wanawake.
Mwanamieleka mmoja alimuangusha mwenzake wakati wa tamasha la mieleka ya kitamaduni iliyofanyika katika mji mkuu wa Mali bamako siku ya Jumapili

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Makabiliano ya mieleka wakati wa tamasha la kitamaduni la mieleka Jumapili katika mji mkuu wa Mali ,Bamako.
Mkiambiaji aliyeshiriki mbio za kilomita 250 za Marathon de Sables akipita karibu na Kourci Dial Zaid na aliyeketi chini ya kivuli ni Jebel El Mraïer eneop la kusini mwa jangwa la sahara nchini Morocco, Jumanne tarehe 9 Aprili 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jumanne mwanamume mmoja wa Morocco akiwa amebarizi kwenye kivuli cha mti, huku mkiambiaji aliyeshiriki mbio za kilomita 250 za Marathon de Sables akipita karibu yake
Tukio la siku sita linalofanana na mbio za Marathon, linalinganishwa na karibu kiwango cha sita cha marathon

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tukio la siku sita linalofanana na mbio za Marathon, linalinganishwa na karibu kiwango cha sita cha marathon . Wanariadha hawa wanaoshindana,walipigwa picha Jumatano huku wakikikabiliana na joto ambalo linaweza kufikia kiwango cha nyuzi joto 50
Mwanamke amevalia sanamu mfano wa simbaalipokuwa akishangilia mechi siku ya Jumamosi katika mji wa Afrika Kusini wa Cape Town kama ishara ya kuhamasisha watu wazuwie kutokomezwa kwa tembo na ngili

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mwanamke amevalia sanamu mfano wa simbaalipokuwa akishangilia mechi siku ya Jumamosi katika mji wa Afrika Kusini wa Cape Town kama ishara ya kuhamasisha watu wazuwie kutokomezwa kwa tembo na ngili
Mwanamke huyu alishinda awamu ya mashindano ya pamoja ya kusokota bangi katika mashindano ya tamasha la bangi mjini Cape Town, Afrika Kusini - Jumamosi 6 Aprili 2019

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Katika siku hiyo hiyo mjini Cape Town, mashindano ya kusokota bangi yalifanyika kusherehekea kukuakwa sekta ya bangi kwenye tamasha la mmea huo . Matumizi ya bangi miongoni mwa watu wazima katika maeneo maalumu yalihalalishwa mwaka jana nchini Afrika Kusini
Yinka Shonibar akiwa katika duka la London la Tate Modern Jumatatu na kitambaa chake katika makaba ya vitabu vya London, Uingereza vilivyofunikwa kwa vitenge vinavyohusishwa na fasheni za Afrika - Monday 8 April 2019

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Msanii Muingereza mwenye asili ya Nigeria Yinka Shonibare akiwa katika duka la London la Tate Modern Jumatatu na kitambaa chake katika makaba ya vitabu vya London vilivyofunikwa kwa vitenge vinavyohusishwa na fasheni za Afrika
Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel akitoa heshma zake mjini Kigali kwa askari wa Ubelgiji 10 wa kulinda amani walikufa katika mauaji ya halaiki nchini Rwanda Jumatatu tarehe 8 Aprili 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel akitoa heshma zake mjini Kigali kwa askari wa Ubelgiji 10 wa kulinda amani walikufa katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda
Mwanamke akisoma orodha ya majina ya baadhi ya watu zaidi ya 800,000 waliouawa 1994

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Alikuwa anashiriki matukio ya maadhinisho ya miaka 25 baada ya mauaji ya kimbari . Katika siku hiyo hiyo katika makumbusho ya mauaji hayo mjini Kigali mwanamke huyu alikuwa akisoma orodha ya majina ya baadhi ya watu zaidi ya 800,000 waliouawa 1994...
Watu walikuwa wameshikilia mishumaa wakati wa usiku wa kumbu kumbu ya mauaji ya kimbari na kufanya maombi ya waathiriwa katika uwanja wa taifa wa Amahoro mjini Kigali Rwanda wakati wa kumbu kumbu ya 25 ya mauaji hayo yaliyotokea mwaka 1994 - Jumapili tarehe 7 Aprili 2019

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Jumapili , ulikuwa usiku wa kuwakumbuka na kuwaombea wanyarwanda waliouawa wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, katika uwanja wa kitaifa wa a night vigil and prayers Amahoro Stadium mjini Kigali...
Watoto wakiwasha mishuma katika usiku wa kuwakumbuka na kuwaombea waliouawa katika mauaji ya mwaka 1994 katika uwanja wa taifa wa Amahoro mjini Kigali Rwanda jumapili tarehe 7 Aprili 2019

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, hata wale ambao walikuwa hawajazaliwa wakati huo waliwakumbuka waliouawa na wakaapa kuwa mauaji hayo yaliyodumu kwa miaka 100 hayatawahi kutokea tena