Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 19.01.2019: Coutinho, Higuain, Batshuayi, Jimenez, Cahill

Philippe Coutinho alihamia Barcelona kutoka Liverpool

Chanzo cha picha, Huw Evans picture agency

Maelezo ya picha, Philippe Coutinho alihamia Barcelona kutoka Liverpool

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amefutilia mbali uwezekano wa Philippe Coutinho, kurejea Liverpool mwaka mmoja baada ya kumuuza kwa Barcelona kwa pauni milioni 142. (Liverpool Echo)

Liverpool wameweka dau la pauni milioni 61 kumnunua mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 19, kutoka Benfica. (Correio da Manha - in Portuguese)

Meneja wa Monaco Thierry Henry anataka kumsajili kwa mkopo kiungo wa kati wa Manchester United mbelgiji Marouane Fellaini, 31. (RMC - in French)

Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Gonzalo Higuain, 31, yuko mjini London kutia saini mkataba wa kujiunga na Chelsea ili aweze kushiriki mechi ya kombe la Carabao Alhamisi ijayo dhidi ya Tottenham. (Sun)

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri anapania kuimarisha kikosi chake kwa kumsaini kiungo mwingine wa kati kabla dirisha la uhamisho wa wachezaji kufungwa. (Guardian)

Bayern Munich wamemkabidhi Chelsea winga Callum Hudson-Odoi kwa kadarasi ya pauni 85,000 kwa wiki. (Sun)

Callum Hudson-Odoi

Chanzo cha picha, Google

Maelezo ya picha, Callum Hudson-Odoi

Mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, 23,anakaribia kuafikiana na klabu hiyo kusaini mkataba mpya wa miaka mitano. (Sky Sports)

Meneja wa muda wa United Ole Gunnar Solskjaer anajiondaa kuondoka katika hoteli ya Lowry iliyopo Salford baada ya kupata sehemu nyingine ya kuishi mjini Manchester (Times - subscription required)

Meneja Mauricio Pochettino wa Tottenham amesema klabu hiyo haitamsaini mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Italia Giuseppe Rossi mwezi huu. (Sky Sports)

Everton wanapania kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Michy Batshuayi na wako tayari kulipa pauni milioni 40 kumnunua kiungo huyo wa miaka 25 aliyerejea Stamford Bridge baada ya kujiunga na Valencia kwa mkopo. (Sun)

Michy Batshuayi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Michy Batshuayi,kushoto

Guangzhou Evergrande anataka kumsaini mshambuliaji wa West Ham Marko Arnautovic na tayari ametoa ofa ya euro milioni 40 kumnunua mchezaji huyo wa miaka 29, raia wa Austria. (Guardian)

West Ham imeshindwa kumsajili mshambuliaji wa Torino Mtaliano Andrea Belotti, 25, kwa euro milioni 40. (Sportitalia - in Italian)

Meneja wa Paris St-Germain Thomas Tuchel amesema kuwa Adrien Rabiot, ambaye amehusishwa Barcelona na Chelsea, hawezi kuhama klabu hiyo kutokana na mzozo unaokumba kandarasi yake (Goal)

Wolves wako tayari kusubiri hadi mwisho wa msimu huu kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Benfica, Raul Jimenez,27.

Raul Jimenez

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Raul Jimenez

Nyota huyo wa kimataifa wa Mexico amefunga mabao sita katika ligi ya Primia (Daily Mirror)

Meneja wa Fulham Claudio Ranieri amesema hana uhakika ikiwa mlinzi wa Chelsea na England Gary Cahill, 33, anataka kujiunga na Cottagers, ambao wameburuzwa chini katika jedwali la msimamo wa ligi ya kuu ya England. (Football.London)

Meneja Pep Guardiola, wa Manchester City, anadai kuna upelelezi mkubwa katika kandanda ya Ulaya na kukiri kuwa aliwahi kufanya hivyo alipokua Barcelona na Bayern Munich lakini hatarudia tena kufanya hivyo nchini Uingereza. (Telegraph)

Pep Guardiola

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pep Guardiola

Mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, 27, amethibitisha kuwa atasalia Bayern Munich hadi mwisho wa msimu huu, hatua hiyo imedidimiza matumaini ya Arsenal kumsajili. (Express)

Crystal Palace wanapania kumsaini kwa pauni milioni 3 winga wa Leeds muingereza Jack Clarke wa miaka 18, ambaye ameshiriki mara 12 michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu. (Mirror)

Inter Milan wanakaribia kukamilisha shughuli ya kumsaini kiungo wa kati wa Cagliari mtaliano Nicolo Barella, 21, wambaye amehusishwa na tetesi ya kuhamia Chelsea. (Calciomercato)

Barcelona wanajiandaa kumwachilia Malcom, 21, ambaye pia ni winga wa Brazil kuondoka klabu hiyo endapo watapokea ofa nzuri kuliko euro milioni 41m waliyolipa Bordeaux kumnunua mchezaji huyo julai iliyopita. (ESPN)

Tetesi bora kutoka Ijumaa

Aaron Ramsey ametia saini makubaliano ya awali ya mkataba wa kujiunga na Juventus kutoka Arsenal msimu huu.

Aaron Ramsey

Chanzo cha picha, Huw Evans picture agency

Maelezo ya picha, Aaron Ramsey alijiunga na Arsenal kutoka Cardiff City mwezi Juni 2008

Kiungo huyo wa miaka 28 tayari amekamilisha vipimo vya afya na mabingwa hao wa Italia wanaoshiriki ligi ya Serie A, wikendi iliyopita. (Sky Sports)

Ramsey anatarajiwa kutia saini mkataba wa miaka minne wa kitita cha euro milioni 300,000 kwa wiki, ambao utamfanya kuwa mchezaji wa Uingereza anaelipwa vizuri zaidi. (Times)

Manchester United wako tayari kuongeza malipo ya Marcus Rashford kwa hadi euro 150,000 kwa wiki ili kumzuia kiungo huyo wa miaka 21 asihamie vilabu vyovyote vikuu vya Ulaya msimu huu. (Mirror)

Liverpool wanamfuatili a kiungo wa kati wa Schalke Weston McKennie ,20. (Sun)

Meneja wa Arsenal Unai Emery amekiri kuwa wamefanya mazungumzo na Denis Suarez wa Barcelona lakini hakuna uwezekano wa kiungo huyo kusajiliwa mwezi huu. (Mirror)