Kanye West abadilisha jina lake kuwa YE

Chanzo cha picha, PA
Rapa Kanye West amebadilisha jina lake kuwa Ye.
Akitangaza mabadiliko hayo kwenye Twitter siku ya Jumamosi, aliandika: "Nimekuwa nikijulikana kama Kanye West. Mimi ni YE."
West, 41, amekuwa akiitwa Ye kwa muda na kulitumia jina hilo kama kichwa cha albamu yake ya nane ambayo ilitolewa mwezi Juni.
Mabadiliko hayo yalikuja kabla ya tamasha moja wa siku ya Jumamosi ambapo alitarajiwa kuzindua albamu yake mpya ya Yandhi.
"Ninaamini 'ye' ni jina linatumika sana kwenye Biblia na kwenye Biblia linamaanisha 'wewe,'" West alisema mapema mwaka huu wakati akizungumzia albamu yake na mtangazaji wa redio Big Boy.
"Kwa hivyo mimi ni wewe, mimi ni sisi, ni sisi. Albamu hii ni ishara ya vile tulivyo."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Ni mmoja wa marapa kadhaa waliobadilisha majina yao.
Sean Combs awali alikuwa akijulikana kama Puff Daddy, P. Diddy au Diddy lakini mwaka huu alitangaza majina ya Love na Brother Love.












