Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uswiss yakataa maombi ya Roman Abramovich
Mamlaka nchini Switzerland imetupilia mbali maombi ya kuishi nchini humo kutoka kwa bilionea wa Kirusi Roman Abramovich.
Bilionea huyo ni mmiliki wa klabu ya mpira ya Chelsea ambaye alituma maombi yake ya kutaka kuishi maeneo ya mapumziko ya Alpes ya Verbier, ambapo awali alikubaliwa , lakini polisi wa shirikisho la Uswisi walitoa sababu ya kukataa ombi hilo kuwa wanahisi Abramovich anaweza kuhatarisha usalama na hivyo basi ombi lake likatupiliwa mbali.
Mpaka sasa hakuna ushahidi wowote wa kihalifu alioutenda, na mwanasheria wa Abramovich amesema kwamba madai hayo wanayomshukia yote ni ya uongo.
Abramovich anatuhumiwa kwa uhalifu wa kutakatisha fedha na makosa mengine ya jinai yote hayo bado hayajathibitishwa, lakini mamlaka nchini Uswis imetamka bayana kuwa hazihitaji ithibati; hisia kidogo tu juu yake zinatosha kuwa sababu ya kusitisha maombi yake ya ukaazi.
Abramovich ni nani?
-Abramovich ana umri wa miaka 51 na ni miongoni mwa matajiri nchini Urusi.
-Biashara yake ya awali ilikuwa ni kununua wanasesere kabla hajawa tajiri kwa biashara ya mafuta miaka ya 1990 baada ya kuanguka kwa muungano wa utawala wa Urusi.
-inaarifiwa kuwa Abramovich anatajwa kuwa aliwahi kuwa mshirika wa kibiashara na mfanya biashara mkubwa Boris Berezovky, aliyekuwa mshirika wa Rais wa zamani wa Urusi Boris Yeltsin .
-Wakosoaji wanasema wafanyabiashara hao wawili walitumia uhusiano wao na "Kremlin" waliyoiita familia ili kupata makampuni muhimu makubwa kwa thamani ya chini ya soko.
-abramovich aliwahi kutumika kama gavana wa jimbo la Chukotka nchini Urusi.
-anatajwa pia kuwa na uhusiano wa karibu na raisi aliyeko madarakani Vladimir Putin
-Ni mmilili wa Klabu ya mpira wa miguu ya Chelsea