Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Alexis Sanchez: Man Utd huenda ikamuuza mshambuliaji huyo iwapo hatoimarika - Ian Wright
Mshambulaiji Alexis Sanchez huenda akauzwa na Manchester United mwishpo wa msimu iwapo kiwango chake cha mchezo hakitaimarika , kulingana na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright .
Sanchez, anayeripotiwa kupata mapato ya hadi £391,000 kwa wiki hajaonyesha kiwango cha mchezo wake kama alivyokuwa Arsenal kabla ya kujiunga na United mnamo mwezi Januari.
"Iwapo ningekuwa mfanyibiashara , ningetazama hali ilivyo halafu nianze kupanga ni wachezaji gani nitawauza'' , alisema Wright.
"Ni kwa sababu ya mshahara anaopata."
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 raia wa Chile alionyesha mchezo mzuri alipoingia United , katika mechi ya FA CUP dhidi ya Yeovil mwezi Januari, lakini hadi kufikia sasa amekuwa na mchanganyiko wa viwango vya mchezo wake akifunga mabao matatu pekee kati ya mechi 23.
Wright: "Kwangu mimi kwa sasa , iwapo United imemlipa fedha hizo, kitu cha kwanza kufikiria ingekuwa ni vipi wanaweza kuzirudisha fedha hizo? Sanchez atalazimika kupunguza kiwango chake cha mshahara wa kila wiki iwapo atahamia klabu nyengine.
''Hakuna mtu anayeweza kumlipa fedha anazopata kutokana na kiwango chake cha chini cha mchezo''.
Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona ameshiriki katika mechi tano akiichezea United , lakini aliwachwa nje katika mechi ya vilabu bingwa ambapo United iliibuka mshindi kwa mabao 3-0 dhidi ya klabu ya Uswizi Young Boys ambapo mchezaji aliyechukua mahala pake Anthony Martial alifunga bao.
Sanchez alicheza mahala pake ,mshambuliaji huyo wa Ufaransa siku ya Jumamosi lakini alitolewa kunako dakika ya 63.
''Hafai kuchezeshwa katika timu wakati unapokuwa na Martial na Marcus Rashford'' , alisema Wright ambaye ndio mchezaji wa pili aliyefunga mabao mengi katika klabu ya Arsenal, aliongezea.
''Unamtazama akiichezea United , ana uhuru wote .Kiwango chake cha mchezo kitalazimika kuimarika ili kuwa na haki ya kuchezeshwa''.
Mshambuliaji wa zamani wa Blackburn na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Chris Sutton alisema kuwa Sanchez amepotea na hana motisha tena.
''Ni kana kwamba anabeba uzani wa dunia nzima katika mabega yake. Akiwa Arsenal alicheza na uhuru mwingi na furaha, kwa sasa sioni kiwango kama hicho cha mchezo iwapo hatobadilika''.