Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 25.09.2018: De Jong, Herrera, Mourinho, Pogba
Manchester United na Real Madrid wana mipango ya kumsaini kiungo wa kati wa Ajax Mholanzi mwenye miaka 21, Frenkie de Jong, anayewekewa thamani ya pauni milioni 72. (De Telegraaf - in Dutch)
Kiungo wa kati wa Uhispania Ander Herrera, 29, angetaka kubaki huko Old Trufford licha ya Barcelona kumzea mate. (ESPN)
Arsenal wanamwinda mchezaji wa Rennes raia wa Senegal mwenye miaka 20 Ismaila Sarr, ambaye pia anatazamwa na Inter Milan.(Mirror)
NewCastle watafanya mkutano na meneja Rafael Benitez kuhusu bajeti ya mwezi Januari kujaribu kumwezesha Mhispania huyo kusalia kwenye klabu baada ya mwisho wa msimu. (Telegraph)
Paris-St Germain wanammezea mate beki wa Juventus mwenye miaka 27 Mbrazil Alex Sandro, ambaye awali amehusishwa na Manchester United. (Le10 Sport - in French)
West Ham wako kwenye hatari ya kumpoteza mlinzi wa miaka 19 raia wa Ireland Declan Rice baada ya kukataa nyongeza ya mshahara wa pauni 12,000 kwa wiki. (Mail)
Arsenal, Manchester United, Liverpool, Chelsea na Newcastle ni kati ya vilabu 18 ambavyo vimewatuma maajenti kumtazama kipa wa Benfica Mjerumani Odisseas Vlachodimos, 24. (Record - in Portuguese)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alimlaumu kiungo wa kati Paul Pogba, 25, kwa bao lilifungwa na Wolves huko Old Trafford siku ya Jumamosi. (Sun)
Meneja wa zamani wa England Sven-Goran Eriksson yuko njiani kukiongoza klabu ya Iran ya Tractor Sazi, kilichomfuta kocha wa Wales na Real Madrid John Toshack mapema mwezi huu. (Sun)
Aston Villa wako tayari kuanza mazungumzo na mlinzi wa Wales James Chester, 23, kuhusu mkataba mpya. (Telegraph)
Bayern Munich wanammezea mate mlinzi mwenye miaka 22 wa RB Leipzig mjerumani Lukas Klostermann. (Sport Mediaset - in Italian)
Mtoto wa Meneja wa Cletic Brendan Rogers, Anton atashinda mkataba na klabu yenye matattizo ya Falkirk kufuatia majaribio. Kiungo huyo wa katu wa Northen Ireland alicheza dhidi ya St Mirren reserves wiki iliyopita na Dundee United siku ya Jumatau. (Falkirk Herald)
Bora zaidi kutoka Jumatatu
Mlinzi wa Manchester United Chris Smalling anataka kusaini mkataba mpya huko Old Trafford. Mchezaji huyo wa kimataifa mwenye miaka 28 wa England ana chini ya miezi 12 iliyobaki mkataba wake wa sasa kukamilika. (Star)
Kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Mjerumani Mario Gotze, 26, ameshuriwa kujiunga na meneja wake wa zamaniaJurgen Klopp huko Liverpool. (Sky Sports)
David Beckham anafanya mazungumzo na mchezaji mwenzake wa zamania huko Real Madrid Zinedine Zidane kuhusu kukisimamia klabu yake ya Inter Miami katika ligi ya MLS. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 27, anasema anahisi kuwa katika hali nzuri asilimia 200 licha ya kupumzishwa na meneja Maurizio Sarri kati kati ya wiki. Alirudi uwanjani akiwa kikosi cha kwanza wakati wa mechi iliyomalizika kwa sare siku ya Jumapili na West Ham. (Sky Sports)
Kipa mwenye miaka 25 wa Besiktas Loris Karius -ambaye yuko kwa mkopo huko Liverpool anasema anapata motisha kutoka kwa kipa wa zamani wa Ujerumani Olivier Kahn. (Bild - in German)
Wachezaji wa Everton wanaamini wanafanya maandalizi mengi wanapojiandaa kwa mechi za Ligi ya Primia chini ya usimamizi wake Marco Silva. (Sun)