Ni kweli kuwa serikali ya Afrika Kusini inawapokonya wakulima mashamba yao?

Chanzo cha picha, Getty Images
Madai: Serikali ya Afrika Kusini inawapokonya wakulima mashamba.
Kilichopo: Wakulima hawapokonywi mashamba kwa sasa lakini serikali imesema ina mipango ya kuchukua hatua za kugawa ardhi bila ya kulipa fidia.
Rais Trump alisema kwenye mtandao wa Twitter kuwa alikuwa amemuagiza waziri wa mashauri ya nchi za aigeni kushughulikia suala la wakulima kupokonywa mashamba na mauaji ya wakulima wengi nchini Afrika Kusini.
Alionekana kujibu ripoti ya kituo cha Fox News ikiwemo nukuu kuwa serikali ya Afrika Kusni kwa sasa inatwaa mashamba kutoka kwa wakulima wazungu.

Chanzo cha picha, Twitter
Ujumbe wa Trump ulipingwa na serikali ya Afrika Kusini ambayo nayo iljibu kwa njia ya twitter ikisema ujumbe wa Trump una nia ya kuigawanya nchi.
Ardhi ya wakulima wazungu inatwaliwa nchini Afrika Kusini na wakulima wengi wanauawa?
Maneno ya Rais wa Marekani yanakuja wakati ambapo suala la ardhi ni ajenda kuu kwenye siasa za nchi hiyo.
Mashamba mengi nchi humo na sekta nyingi za kilimo zinamilikiwa na wakulima wazungu - 72 ya asilimia kulingana na takwimu za serikali. Wazungu huchukua asilimia 9 ya watu wote nchini Afrika Kusini.
Huku suala la kutwaliwa ardhi likiwa linazungumziwa sasa halifanyiki, serikali ya Afrika Kusini imependekeza kuwa itafanyia marekebisho katiba yake na kugawa ardhi bila ya kuwafidia wenye mashamba.
Suala la ugavi wa ardhi nchini Afrika Kusini linaanzia enzi za ukoloni. Sheria ya ardhi ya mwaka 1913 iliwazuia watu weusi kutokana na kununua na kukodisha ardhi kwa nchi ya wazungu ya Afrika Kusini hatua iliyochangia kuondelewa kwa lazima watu weusi.

Mwaka 1994 baada ya kuisha kwa utawala wa ubaguzi wa rangi, Serikali ya kwanza iliyochaguliwa kidemokrasi nchini Afrika Kusini, ilisema itagawa asilimia 30 ya ardhi inayomilikiwa na wazungu kwa wakulima weusi ifikapo mwaka 2014. Lakini hadi sasa ni asilimia 10 tu ya ardhi iliyogawa kwa wazungu hadi sasa.
Chini ya shinikizo la kutekeleza ahadi za chama za kugawa ardhi, kiongozi wa ANC na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alitangaza mipango mwezi Julai mwaka huu ya kuifanyia mabadiliko katiba kufanikisha kutwaliwa ardhi bila kuifidia.
Ujumbe wa Trump unakuja wakati mwafaka. Wiki hii Bw Ramaphosa alizungumza bungeni akielezea kuhusu umuhimu wa mabadiliko hayo ya katiba.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mpango huo unahitajika ili kuleta uwiano na kumaliza uhasama wa kihistoria, alisema.
Wakosoaji wanazungumzia mabadiliko yenye utata kwenye nchi jirani ya Zimbabwe ambayo yalisababisha kuondolewa kwa lazima wakulima wazungu na kuporomoka kwa sekta ya kilimo.
Kuuawa kwa wakulima
Wakulima nchini Afrika Kusini, wakiwemo wazungu na wale weusi wamekuwa wenye wasi wasi mkubwa kuhusu usalama wao wakati huu, wengi wakichukua hatua za kujilinda pamoja na wafanyakzi wao.
Hadi Aprili mwaka 2017 polisi wanasema kuwa watu 19.016 waliuawa nchini Afrika Kusini.
Kila mwaka huripotiwa mauaji mengi kwenye mashamba ya nchi hiyo huku mamia ya mashambulizi yakiripotiwa.
Kulingana na polisi watu 74 waliuwa kwenye mashamba kati ya Aprili 2016 na Machi 2017.
Idadi hiyo ni ya wakulima waliouawa, wafanyakazi na wageni kwenye mashamba bila kujali rangi.












