Wanafunzi wasulubiwa na kutandikwa viboko kwa kuchelewa Nigeria

Chanzo cha picha, Punch Newspapers
Watu watatu wamekamatwa Nigeria kwa kutuhumiwa kuwafunga wanafunzi katika misalaba na kuwatandika viboko barabarani.
Watu hao watatu - akiwemo mwalimu mkuu - wanazuiwa baada ya polisi kupita na kushuhudia kisa hicho kuisni magharibi mwa jimbo la Ogun.
Picha zinaonyesha watu wawili - mmoja mvulana na miwngine msichana - waliofungwa kwenye msalaba kwa kamba ya kijani.
Msemaji wa polisi ametaja adhabu hiyo kama ya 'kiunyama'.
Taarifa katika eneo hilo zinasema walikuwa wanaadhibiwa kwa kuchelewa shuleni.
Afisa huyo - anayefahamika kwa jina moja tu Livinus - alijaribu kuingilia kati, akimtaka mwalimu mkuu awaachie wanafunzi hao .
Na wakati mwalimu mkuu huyo alipokataa afisa aliamua kuchukua hatua na aksukumwa nyuma kwa nguvu.
'Nilipo jaribu kuwafungua wanafunzi , mwalimkuu na walimu wake walinipiga, aliliambia gazeti la Nigeria Punch. 'Kabla nirudi kutoka kwenye gari langu kuchukuwa pingu , walimshikilia rafiki yangu niliyekuwa naye..... na kumchapa kwa kiboko.'
Washukiwa hao hatimaye walikamatwa baada ya afisa wa polisi kupata usaidizi kutoka kwa maafisa wengine waliowasili.
Msemajiw a polisi katika jimbo la Ogun, Abimbola Oyeyemi ameithibitishia BBC kuwa mwalimu mkuu, mmiliki na mwalimu mwingine walikamatwa na huenda wakashtakiwa.
Aliongeza: "Hiyo sio kumuadhibu mtoto tena, ni unyama uiskubalika na hatuwezi kuuvumilia."












